RSS

Kristiane Backer

16 Nov

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Alizaliwa katika jiji zuri salama la Hamburg huko Ujerumani mnamo tarehe 13 Disemba 1966. Maisha yake ya kikazi yalianza akiwa na umri wa miaka 21 pindi alipojiunga na Redio Hamburg kwa mafunzo ya kujitolea ya miaka miwili ya uandishi wa habari. Miaka miwili baadae, Kristiane alichaguliwa kuwa mtangazaji wa kwanza kutoka Ujerumani katika kituo cha muziki cha MTV, huku akiwashinda wengine elfu. Hatimaye mwaka 1989, alihamia London. Akiongelea maisha yake ya huko alikuwa na haya ya kusema:

“Ilikuwa ni raha, nilikuwa na miaka ishirini na, niliishi Notting Hill, nilikuwa mwanadada mgeni pale na nilialikwa kila mahali, nikipigwa picha na Mapaparazi. Nilikutana na watu mashuhuri wengi (kuanzia Robbie Williams hadi Lenny Kravitz), na nilifurahia sana muda wangu kule. Nilitumia kiasi kikubwa cha mshahara katika mavazi. Nilisafiri karibia ulaya nzima, nikitembelea sehemu nzuri nzuri kama Barcelona, Istanbul, Paris; na kuna kipindi nilienda hadi Boston kuwahoji Rolling Stones, na nilikuwa sambamba na mtoto wa mfalme kwa takriban wiki nzima. Nilikuwa mwanadada namba moja katika MTV na nadhani nilikuwa nikionekana kwa televisheni muda wote. Nilitangaza kipindi cha Coca cola Report na kile cha Top 20 za Ulaya. Nilihoji vikundi vingi vya sanaa na mamilioni ya watu walinijua Ulaya nzima. Katika moja ya maonyesho ya muziki wa roki (rock), nilisimama jukwaani mbele ya watu 70,000.”

Backer  alishawahi kupokea tuzo nyingi za televisheni, zikiwemo The Golden Camera na mbili za Golden Ottos. Pamoja na kutembea sana Ulaya, pia alipata nafasi ya kutembelea Mashariki. Baadhi ya nchi alizotembelea ni Morocco, Misri, Uturuki, Pakistan, Syria na Saudi Arabia. Anasema, “Safari zangu nyingi katika maeneo ya Waislamu kumenifanya nilime mengi kutoka katika jamii hizo ambapo ikaniwezesha kuvuna maarifa makubwa ya dini na maisha yao.’

Mwaka 1992, alikutana na Imran Khan, nahodha wa timu ya kriketi ya Pakistan. Hiyo ndio ilikuwa mara yake ya mwanzo kukutana na Muislamu na kujadili mengi kuhusu dini hiyo. Alimpatia vitabu kadhaa vya dini na Kristiane akajitolea muda wa kuvisoma. “Nilianza kuhoji maoni na chuki zangu ziso sababu na vichwa vya habari dhidi ya dini hii, nikaanza kuisoma Qur’an na ikaanza kuniingia kichwani,” Alisema.  “Nikagundua kuwa Uislamu ni wa wote, wanawake na wanaume; katika Uislamu wanawake walikuwa na haki ya kuchagua tangu mwaka wa 600. Wanaume walivaa kiheshima, na wanawake pia, hakuna aliyetumia macho yake vibaya [kwa kutongozana] bali kila mtu [kwa ajili ya kutaka stara, haya, heshima na uchaji Mungu] aliinamisha shingo yake chini.”

Alipoulizwa kuhusu zana alizotumia kuujua Uislamu, Kristiane alisema ukiachana na Qur’an pia amesoma vitabu vilivyoandikwa na wasomi kama Martin Lings, Dkt. Seyyed Hossein Nasr, Lei Gai Eaton, Annemarie Mould, Dkt. Zaki Badawi, Murad Hofmann, Muhammad Asad, na wengine wengi. Pia alidiriki hata kuwatafuta wengine kwa kujifunza zaidi. Akiathiriwa na sababu zenye mantiki katika Uislamu, Baker alikubali kuubeba mzigo huo na baada ya kugundua heshima aliyoikosa siku zote, alisema: “Niliacha kuvaa nusu uchi na nikaanza kuvaa sketi ndefu katika TV…Nashangazwa na wanawake wengi wanaopunguza nguo zao ili watolewe katika vichwa vya habari tena katika kurasa za mbele- kusema kweli ni kujishusha thamani yako.

Ilikuwa ni mwaka 1995 ambapo aliuacha Uprotestanti na kusilimu. Sasa anaswali swala tano na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan. “Nilikuwa nikitumia vilevi katika sherehe kila siku usiku, lakini sasa sio kuntokuywa tu bali hata kugusa.” Na mwaka 2001, alikwenda Makkah, “Ilikuwa safari nzuri sana, nilirudi nikiwa nafuraha tele na amani moyoni.”

Baadae alijiunga katika Chuo Kikuu cha Westminster na kusomea elimu ya tiba ikiwamo miti shamba, mafuta ya miti, dawa za kichina, uasili wa maua na homeopathy. Mwaka 2002 alifaulu kuwa mtaalamu wa tiba ya homeopathy na Septemba mwaka uliofatia alianzisha kliniki yake kupitia mtandao wa intanet, http://www.energy-for-health.com. Kwa sasa anayo kliniki yake ya homeopathy huko Ujerumani. Pia kajumuishwa katika mpango wa kutengeneza vya kujipambia na vyakula vitokananvyo na dawa za kiasili na mafuta ya miti yanayopatika nchi za Kiarabu.

Ukiachilia masuala ya tiba za kiasili, Kristiane amesomea masomo ya dini ikiwemo dawa za Kisunnah na sanaa ya kiislamu, na elimu ya jamii na siasa kutoka Chuo Kikuu cha Islamat Birkbeck. Anazungumza vizuri Kifaransa na Kiarabu.

Anaendelea kuandaa matukio mengi Ulaya. Amekuwa muandaji mzuri wa mikutano na makongamano. Baadhi ya makongamano yaliyoandaliwa naye ni kama Islamophobia (lilioandaliwa na Islam Channel, Copenhagen), Sage Software Awards (Wiesbaden), Tuzo za Biashara za Ulaya (European Business Awards, Barcelona), European Electronic Awards (Munich), Royal Mail Awards (Berlin), Infineon Supplier Awards 2004 (Munich), Pirelli Calendar 2004 launch “The making off” London, PR Report Awards (Berlin), VW Nick Nickel Gala and awards ceremony, GE Capital IT Solutions for Compuserve European Kick- Off Meeting/ Awards.

Mara kwa mara amekuwa akiandika makala tofauti kuhusu masuala ya afya kwa magazeti ya Kiengereza na ya Kijerumani na pia wakati mwengine akiongelea masuala hayo katika vipindi vya televisheni na redio. Baadhi ya kazi zake zipo katika magazeti kama Time Out, The Daily Express, Compass na Red magazine, BBC Radio The Sadie Nine Show, LBC Jules Eden show, Sky News, ARD TV na NTV. Tangu 2004, Kristiane amekuwa mtangazaji wa tiba za kiasili kila jumatano saa 6:40 mchana (kwa saa za ulaya ya kati) katika muda wa kipindi cha chakula cha mchana Punkt 12 katika kituo kikubwa zaidi cha Televisheni Ujerumani, RTL. Na miongoni mwa vipindi vyake katika PRESS TV ni World Week Watch– mapitio ya matukio ya dunia kwa dakika 23 kitangazwacho na Oscar Reyes pamoja na yeye Kristiane Backer.

Uislamu ndio uliomletea maisha mapya. “Ni zawadi kubwa kuliko zote niliyowahi kupokea.” Alikiri mwenyewe. Tarehe 14 Aprili 2006, aliolewa na mwandishi wa habari Rashid Jaafar.

Njia ya Mawasiliano:

Anuani

Sherif Code 82466573

9 Burnaby Street

London SW 10 OPR

020 73574344

Simu: +44 (0) 20 7351 4344;

Barua pepe:

homeopathy@energy-for-health.com

info@kristianebacker.com

Tovuti:

http://www.kristianebacker.com

 REJEA

[Backer, Kristiane. “Islam is very accessible.” By Sausen Rahal Moussa. Islamic Newspaper 11Oct.2006; http://www.kristianebacker.com.]

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on November 16, 2012 in Waliosilimu

 

Tags: , , , ,

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: