RSS

Author Archives: muerevumno

Balqis Chelang’at Chepkwony

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

“Nilipatwa na ugumu kweli kuamini kuwa Yesu hakufa msalabani”

~ Maneno ya Balqis baada ya kusoma kitabu cha Ahmed Deedat (kiitwacho Crucifixion or Cruci-fiction [Ni Kweli Yesu Kasulubiwa au ni Ubunifu tu!])

Hakukuwa na kikomo kwa Caroline Chelang’at Chepkwony, alikuwa mwanafunzi mwenye juhudi sana na siku zote alikuwa akishika nafasi ya juu katika maisha yake ya shule ya msingi. Baba yake alitaka awe daktari lakini mzungu mmoja, rafiki wa baba yake alishauri Caroline awe mtakwimu bima (Actuary). Wakafata ushauri ule. Ni wanafunzi wafanyao vizuri tu kitaifa ndio wanaoweza kupata nafasi katika shule chache za serikali, Kenya na Caroline Chelang’at alikuwa mmoja wa walioteuliwa. Alichagua Shule ya Sekondati ya Alliance (Alliance Girls High School). Shule inayotambulika kwa kutoa elimu nzuri na kufaulisha watoto sana inayotawala vichwa vya vyombo vya habari katika redio, televisheni na magazeti ifikapo kipindi hiko. Wanafunzi wa hapo wanapenda kuiita shule yao kama “bush (kichaka)’ na wanafunzi kama ‘busherians (wanakichaka)’. Jina hilo lisilo rasmi limetokana na msitu mkubwa uliozunguuka shule. Na wala jina hilo halihusiani na rais mstaafu wa Marekani aliyekoswa na kiatu. Shule hiyo mara kwa mara imekuwa ikifanya vyema katika mitihani ya taifa kidato cha nne, ikiwa ni kawaida kuingia kumi bora katika shule za Kenya.

Baada ya kufanya vizuri katika mitihani hiyo ya elimu ya sekondari  ambapo alipata wastani wa A- kwa masomo yote akipata daraja la juu  (A) katika somo la Hisabati, Fizikia, Kemia, Komyuta na Jiografia, Caroline moja kwa moja aliweza jinyakulia nafasi katika vyuo vya elimu ya juu vya serikali. Chuo kikuu cha Nairobi (UoN), chuo kikubwa zaidi Kenya, kilimchukua na chini ya kitivu cha Hisabati akisomea Utakwimu Bima (Actuarial Science). Na Chuo Kikuu hicho cha Nairobi ndiyo chuo pekee Kenya nzima, kwa wakati huo, kitowacho shahada ya Utakwimu Bima. Mwaka huo 2002, Chuo cha Nairobi kilikuwa kikichukua wanafunzi 16 tu Kenya nzima waliochaguliwa na serikali na Chelang’at alikuwa mmoja wa waliostahili.

Akiwa mwaka wa pili wa masomo, Caroline alikutana na Salim, mwanafunzi katika hiko chuo kikuu aliyekuwa akichukua masomo yake katika Kitivo cha Fani (Faculty of Arts). Moja ya vipaumbele vya Salim katika maongezi ilikuwa ni mazungumzo ya dini. Alimchokoza Chelang’at kuhusu imani yake ya dini. Salim alimuomba Chelang’at afanye ufatiliaji mzuri kuhusu dini na yeye akamsikiliza. Bila kupoteza muda, Salim alimkabidhi Chelang’at baadhi ya vitabu na makala yanayoongelea linganishi ya dini mbalimbali, na kumtajia orodha ya tovuti ambazo zinachambua masuala ya dini vyema tena kwa kutumia akili ya kawaida.

Baadhi ya vitabu ambavyo Caroline alivisoma vya Ahmed Deedat ni:

►Is the Bible the Word of God? (Je Biblia ni Neno la Mungu?

►Crucifixion or Cruci-fiction! (Kusulubiwa Kweli au Kusulubiwa kwa Kubuniwa?)

►Resurrection or Resuscitation? (Kufufuka au Kurudishiwa Fahamu?)

►What Was the Sign of Jonah? (Ipi ilikuwa Muujiza wa Yunus?)

►Who Moved the Stone? (Nani Aliyesogeza Jiwe?)

►Qur’an Miracle of Miracles (Qur’an ni Muujiza wa Miujiza)

►What the Bible Says About Muhammad (pbuh)? (Biblia Inasema Nini Kuhusu Muhammad?)

►Christ in Islam (Kristo Ndani ya Uislamu)

►Combat Kit (Zana za Mapigano)

Vitabu hivyo na venginevyo vya Ahmed Deedat vilivunja kabisa imani ya Kikristo ya Caroline na hatimaye alibaki na moja tu la kufanya, nalo ni kuingia katika Uislamu. Hiyo ilikuwa mnamo tarehe 14 Aprili 2005 akiwa na miaka 22 ndipo Caroline alipoamua rasmi kuwa Muislamu na kuliacha jinale la Kikristo na kuchukua la kiislamu akibakisha majina yake ya Kikalenjin (Kalenjin ni moja ya kabila za Kenya). Sasa amekuwa akiitwa Balqis Chelang’at Chepkwony. Kabla ya kusilimu, akili yake ilijaa mawazo mgando na hasi kuhusu Uislamu na Waislamu. “Nilikuwa nikiwachukulia Waislamu kama watu wa ajabu na waliopotea kweli kwani walikuwa wakimuamini Mtume ambaye amekufa,” Alisema. Vitabu vyengine alivyosoma kabla ya kusilimu ni Let the Bible Speak (Wacha Biblia Izungumze) cha Abdul Rahman Dimishkiah, Oneness of God: The Ultimate Solution to the Trinitarian Controversy (Umoja wa Mungu: Suluhisho Thabiti ya Ubishani wa Utatu) cha Marmarinta Umar P. Mababaya na Pillars of Faith (Nguzo za Imani) cha Jaafar Shaikh Idris. Sanjari na hayo, Balqis baada ya kusilimu ameangalia video za Ahmed Deedat akifanya midahalo na wanateolojia mashuhuri wa Kikristo. Dah! Ilimchukua mwezi mmoja na nusu tu, kuhifadhi juzuu Amma, juzuu ya mwisho katika Qur’an iliyo kwa lugha ya Kiarabu (Qur’an ina juzuu 30, Juzuu moja ikiwa na kurasa 20 na Qur’an nzima ina kurasa 604). Japo alibanwa sana na ratiba za masomo shuleni na projects (miradi ya majaribio) bado alithubutu kuhifadhi juzuu nzima ya mwisho ya Qur’an. Hii inaweza kuwa sawa na kuiweka kichwani injili ya Mathayo, neno kwa neno! Msikiti mkubwa zaidi Kenya, Jamia Mosque una kitengo maalumu kwa ajili ya wanaosilimu kikiwa mahususi kuandaa madarasa ya kuwasaidia waliongia katika Uislamu kuijua dini yao. Naye Balqis baada tu ya kusilimu, aliweza kufika hapo, alisoma na kuhitimu masomo hapo katika Taasisi hiyo ya Jamia.

Balqis alifatilia masomo ya Kiislamu kwa dhati, akiendana na aya, “…Kishike Kitabu [yaani dini] kwa nguvu!…” [Q 19:12]. Baada ya kupata shahada yake ya kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi mwaka 2006, na kama ilivyo ada kwa mhitimu yeyote, Balqis naye aliingia katika michakato ya kutafuta kazi. Familia na rafiki zake walimsaidia pia katika hilo. Mzazi wake wa kiume, ambaye alikuwa ni mhasibu mkuu (Chief Accountant) wa Chuo Kikuu cha Moi (Moi University),  bila shaka atakuwa anajuana na wafanyabiashara wengi au makampuni mengi. Hii ingetosha kumpatia kazi nzuri yenye hadhi Balqis. Tena kwa shahada aliyokua nayo, alikuwa na asilimia 100 ya kuchukuliwa na mabenki makubwa makubwa au mashirika ya bima.*

Hii lilidhirika ukweli wake pale makampuni mbali mbali yalipoanza kumgombania, wakianzia na kima cha chini cha mshahara cha Kshs 40 000 (takriban 482 $ au Tshs 748,300) kwa mwezi. Ingawa alikuwa hayupo sawa kifedha wakati huo, Balqis alikataa kazi zote hizo kwa sababu kufanya kazi makampuni ya bima na mabenki hayo ya kibiashara yalikuwa ni haram kwa sheria za Kiislamu. “Kha! Atakuwa kashaanza kuwa mwehu!,” Hivyo ndivyo rafiki na ndugu walivyobaki wakisema. Lakini kwa upande wake, ilikuwa ni makosa na kinyume cha maadili (unethical) kufanya kazi katika mashirika yanayoendekeza riba yakipingana na maneno ya Mwenyezi Mungu: “Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na ameiharimisha riba.…”[Q 2:275].

Alikuwa na yakini kuwa akijitenga na kitu kwa ajili ya Allah basi Mwenyezi Mungu atamfidia na kitu kingine bora kuliko alichokiacha. Alifata maneno ya mtume Muhammad kwa nguvu zote: “Huwezi kuacha chochote kwa ajili ya Allah, aliyetukuka, ila atakupa kengine bora badala yake.”[1] Balqis alipozwa moyo na mafundisho ya Uislamu yaliyompa faraja, tumaini na nguvu: “Enyi watu, muogopeni Mola wenu, na muwe na kiasi katika kutafuta maisha ya dunia, kwani hakuna roho itakayoondoka bila kupokea vyote ilivyokadiriwa, hata kama vinachelewa. Hivyo muogopeni Allah na mumche, muwe na kiasi katika kutafuta rizki; chukua lile lililoruhusiwa na uwache lililokatazwa.”[2]

Badala yake, Balqis akaamua kufanya kazi katika kampuni ya ukaguzi wa mahesabu iliyoko huko Nairobi, karibu na barabara iitwayo Mombasa Road. Hapo alikuwa akilipwa Kshs 10,000 (takriban 120 $ au Tshs 187,000) kwa mwezi. Kutoka katika mshahara huo, alitenga Kshs 2500 (takriban 30 $ au Tshs 46,760) kulipia chumba kilicho kama gereza la Guantanamo huko Eastleigh, sehemu iliyopo kiunga cha jiji la Nairobi. Chumba alichokodi kilikuwa na eneo la mita za mraba 2.5 kwa 1.5, kusema kweli ni kidogo sana hata kwa kitanda tu. Alikuwa na godoro tu ambalo alilliegemeza dirishani wakati wa mchana ili ageuze chumba kuwa cha kukaa (sitting room), na kulitandika chini wakati wa usiku  ili afanye sehemu ya kupumzishia ubavu wake (bedroom). Gharama zake za usafiri kuelekea kazini kwake zilikuwa ni Kshs 3 000 (takriban 36 $ au Tshs 37,407) na chakula kilimgharimu Ksh 3 000 kwa mwezi nayo. Ukiachilia mbali gharama nyengine kama matibabu, mshahara wa Balqis haukuwa ukimtosha ila yeye aliendelea kuvumilia.

Baada ya mwezi, akapata kazi nyengine kama msarifu (bursar) wa Shule ya Sekondari ya WAMY (WAMY High School)  akipokea kiasi cha shilingi za Kenya 20 000 (takriban 241 $ au Tshs 374,000). Alifanya kazi hapo kwa miezi miwili kabla ya ahadi ya Mungu kutimia kwake. Alipokea simu asiyoitegemea. “Naongea na Cheleng’at?…,” Mpigaji alihoji, “je unaweza kujipanga kwa ajili ya usaili (interview) wa kazi ofisini kwetu.” Akapata kazi nzuri hapo akiwa mhasibu wa kampuni ya mafuta ya Hass (Hass Petroleum Company) hapo Nairobi. Kampuni hiyo imestawi Afrika Mashariki nzima na maeneno ya maziwa makuu na inazidi kupanua huduma zake sehemu nyenginezo. Balqis anaiita kampuni hii kama baraka kutoka kwa Allah kwani ndio kampuni pekee Kenya inayotenganisha wafanyakazi wake wa kiume na wa kike na inaruhusu wanawake kuvaa mavazi yao ya kidini ikiwemo niqab (kuziba uso). Kampuni pia, imetenga nafasi kwa ajili ya swala na katika nyakati hizo wafanyakazi wanaruhusiwa kusimamisha kazi zao ili waende kuswali. Mshahara wa kuanzia ulikuwa mara dufu ya alichokuwa akipokea katika shule ya WAMY. Sanjari na hilo, kampuni imempa mkopo usio na riba ambao amenuia kuutumia kwa ajili ya kununua mahali pa kuishi Nairobi. Kwa sasa, mshahara wake wa kila mwezi si chini ya Kshs 130 000 (takriban 1,546 $ au Tshs 2,431,510). Sasa anaelewa vizuri zaidi ule usemi wa Mtume kuwa “Huwezi kuacha jambo kwa ajili ya Allah, aliyetukuka ila Yeye atakupa lengine bora badala yake.  Amekana kufanya kazi katika mashirika yanayoenda kwa riba, kwa ajili ya khofu kwa Allah na sasa anafanya kazi katika kampuni yenye mazingira ya kiislamu. Kifupi, dada huyu ana ushujaa wa kumuingiza peponi kwa kumtambua Mungu pale alipokataa biashara haram. Ibn Maood, swahaba wa Mtume na mwanachuoni mkubwa, alitafsiri uchamungu kama ifuatavyo: “….Kumtii Mungu na katu kutomtii Yeye, kumkumbuka Yeye na kamwe kutomsahau, kumshukuru Yeye na kutojaribu kutoonesha shukrani zako kwake.” Na kulingana na msomi mkubwa aitwae Shaykh Muhammad Swaleh al-Uthaymeen, anatoa taarifa ya Ucha Mungu kama: “Al-Muttaqun (Wachaji Mungu) ni wale ambao wanajilinda na adhabu ya Allah kwa kufanya yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu na kujiepusha na yale aliyoyakataza.”[3]

Kwa sasa, si vibaya kama tukitoka nje ya kisa cha Balqis na kujikumbusha kuwa mahitajio yetu yote yamegawanyika katika vifungu viwili: Ima 1) mazuri ambayo tunayatafuta au 2) mabaya ambayo tunayojiepusha  nayo. Jawabu la mahitajio hayo linapatikana katika aya mbili katika Qur’an. Kama unafanya kazi kuepuka hofu ya magonjwa, kutokua na kazi, mawazo, shida….Mungu anasema: “Na anayemuogopa [anayemcha] Mwenyezi Mungu, (Mwenyezi Mungu) humtengenezea njia ya kuokoka (katika kila balaa).”[ Q 65:2]. Njia ya kutokea kutokana na matatizo yako, mashaka na ugumu unaokupata, hofu ya kufilisika, kutokua na kazi, kuharibu hadhi yako, mabalaa, magonjwa, mgogoro, umasikini, na bila kusahau la muhimu zaidi adhabu kubwa akhera.

Wenye bidii watapata njia ya kufanikisha ndoto zao kwa uwepesi kama wakimtegemea Mungu (sio kumtegea). Vitu unavyotaka kuwa navyo kama kazi nzuri, nyumba nzuri, gari zuri, mke mwema, utajiri na mengineyo yanapatakana kiurahisi iwapo utajiegemeza kwenye uchamungu. Qur’an haikuacha hilo: “Na anayemwogopa [anayemcha] Mwenyezi Mungu, (Mwenyezi Mungu) humfanyia mambo yake kuwa mepesi.”[Q 65:4].  Hata njia yako kuelekea peponi itafanywa rahisi na huu ndio ufanisi mkubwa na wa kweli.

Mafanikio kwa hivyo yanafikiwa kwa daraja ya kumtambua Mwenyezi Mungu na kufuata maamrisho yake. Ndoto zako zote zitatimia kama unamtumaini Yeye kupitia uchamungu wako, na Yeye atakusahilishia njia yako na hofu na mashaka yote yatakuondoka kichwani mwako. Ili kujenga daraja kati ya mafanikio na wewe, uchamungu lazima uzingatiwe. Kuwa mchaMungu kunamaanisha kuitafuta dini ya haki, kujua maamrisho (halal na ya haram) ya Mungu yaliyopo katika maandiko matakatifu ya hiyo dini ya kweli, na kuyafanyia kazi. Kuna ambao wamepata mafanikio bila ya kuwa wachamungu.  Haya “mafanikio” ya kidunia hayatamsaidia akhera. “Mafikio” yao yatakuwa Jahannam (motoni). “Je, kuna faida gani mtu kuupata ulimwengu wote na kuyapoteza maisha yake?” [Marko 8:36].

Balqis sasa ameolewa, na kwa kuongezea katika hazina yake ya baraka, tarehe 2 Septemba, mwaka wa 2008, Mwenyezi Mungu alimjaalia mtoto (wa kiume). Wakiendeshwa na maneno ya mtu mwenye mafanikio zaidi[4]: “Wapeni jina langu watoto zenu…”[5] wanandoa hao walifurahi kumpa mtoto wao jina la Muhammad. Wakipata mtoto mwengine wakiume wana niya ya kumwita Ahmad.* Jina jengine la Mtume lililotajwa na hata Yesu:

“Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad! Lakini alipo waletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio dhaahiri!” [Q 61:6]

“Vuta pumzi kidogo,” Mtu anaweza kuuliza, “Kweli Yesu alimtabiri ‘Roho mtakatifu’ au huyo mnaemwita Ahmad?” Jawabu litategemea na vipi tuna uhakika na maneno ya Biblia.

Kama kiliandikwa kama wahyi (maneno yaliyokuwa yakimshukia Yesu) au yaliandikwa tu na watu wasiokua na uhusiano wowote. Au labda maneno hayo yalihifadhiwa au yalibadilishwa! Kiukweli jibu linapatikana kwa jinsi tulivyoisoma Biblia. Je tunaisoma Biblia kupitia Historical-Critical Approach (njia ya kuhakiki/kukosoa na ya kihistoria) au Devotional-Approach (ile njia ya kishabiki ya kuamini na kukubali kila kitu katika Biblia hata bila kusaili). Ujinga ulioje kwa mtu ambaye hajasoma hata kitabu kimoja cha kisomi kinachotoa ushahidi kuwa Biblia haifai kuitwa neno la Mungu na yeye aendelee kupayuka kwa ubishi na kusema Biblia itaendelea kuwa neno la kweli la Mungu. Dkt. Lawrence B. Brown ambaye amefanya utafiti mwingi kuhusu usahihi wa maandiko ya biblia ni mmoja wa watu anayepaswa kusikilizwa kwa kusema kauli hii: “Tunajidanganya wenyewe na kualika shutuma na dhihaka kama bado tukiendelea kuamini kuwa Agano La Kale au Jipya ni maandiko yasiyochafuliwa ya Mungu.[6]  Kabla ya kutia shaka swala hilo au kukwepa maneno ya msingi ningeshauri, jawabu lolote la kisomi la kujibu kauli ya Dkt Brown, lingetangulizwa na kusoma kitabu chake chochote kama Mis’Goded au kazi nyengine yoyote inayoleta shutuma hizo kwa Biblia kama kitabu Misquoting Jesus: The Story Behind Who Changed the Bible and Why? (Kumnukuu Vibaya Yesu: Kisa Kinachozungumzia Aliyebadilisha Maandiko ya Biblia na Kwanini Alifanya Hivyo) kilichotungwa na msomi mashuhuri duniani wa Biblia, Bart D. Ehrman. Bart D. Ehrman ni profesa wa Taasisi ya James A. Gray na ni mweneyekiti katika kitivo cha masomo ya dini cha Chuo Kikuu cha North Carolina huko Chapel Hill. Alipokea Tuzo mwaka 1994 ya Philip and Ruth Hettleman (Phillip and Ruth Hettleman Prize for Artistic and Scholarly Achievement) kwa tasnia yake ya sanaa ya uandishi na mafanikio yake. Kwa maelezo zaidi kuhusu Ehrman, tembelea tovuti, http://www.bartdehrman.com. Kutoka katika kitabu cha Jesus Interrupted, Bart D. Ehrman anasema:

“Wasomi wamepiga hatua kubwa kuielewa Biblia kwa miaka mia mbili ilyopita na matokeo ya kusoma kwao yanafunzwa kwetu kila siku, kwa wahitimu wa elimu ya juu na mapadri mbalimbali wanaosomea kuja kufanyia kazi upadri wao. Lakini bado jambo hili limekuwa adimu mno katika vichwa vya wengi. Na matokeo yake, sio tu Wamarekani wengi wanazidi kuwa ‘vihio’ (wajinga) kwa yale yaliyoandikwa katika Biblia, lakini pia wako kizani, hawana  utambuzi wa yale ambayo wasomi waliyasema na waliyoyagundua kwa karne hizi mbili zilizopita.[7]

 

Kauli nyengine itakayotuma mawimbi makali ya hofu ni ya yule Profesa John Rogerson wa Chuo Kikuu cha Sheffield, iliyochapishwa na  The Expository Times, jarida la muda mrefu la masomo ya Biblia, na uchungaji. Inasema kwamba “Majumuiko mengi [ya Wakristo] wanawekwa kizani na huwa  hawafahamishwi zile gunduzi za ubatili wa maandiko ya Biblia [zinazogunduliwa na wasomi wa Biblia].”[8]

Tukizungumzia aya ya Qur’an inayothibitisha utabiri wa Injil kuhusu kuja kwa Muhammad, ni vyema tukajifunza kuwa ndani ya Biblia, kuna neno Paraclete (kutoka katika lugha ya Kigiriki parakletos) lenye maana ya ‘Msaidizi’. Inaweza ikawa bahati tu au imepangwa kuwa hivyo kuwa neno Paraclete limetokea mara tano tu katika Biblia, na mara zote tano limesemwa na Mt. Yohana: Waraka (Barua) ya kwanza yohana 2:1; na Yohana 14:16, 14:26, 15:26, 16:7.”[9] Uchunguzi wa kina unaotuacha tukipigwa na butwaa unatuonesha kuwa hata katika Qur’an, Mtume ametajwa kwa jina mara tano tu (Q 3:144; Q 33:40; Q 47:2; Q 48:29 na Q 61:6). Basi tusitafakari?!!

Balqis sio mpenzi pekee wa Muhammad, Mtume wa Mungu. Gazeti la The Times linaripoti kuwa “Muhammad kwa sasa ni jina la pili maarufu baada ya Jack kwa kupewa watoto wa kiume Uingereza na linatazamiwa kushika namba moja ifikapo mwanzoni mwa mwaka kesho, uchunguzi wa The Times umegundua.”[10] Na Januari 2005, makala ya The Guardian ilisema kwamba: “Huko Brussels, Mohammed limekuwa jina maarufu zaidi kwa watoto wote wanaozaliwa kwa miaka minne iliyopita.”[11] Pamoja na hilo, katika kitabu Religion on the Rise, Hofmann anasema: “…kwa miaka kadhaa sasa, ‘Muhammad’ limekuwa jina linalopewa kwa watoto wengi Ufaransa.”[12]

Tukirejea katika kisa cha Balqis. Nilisahau kusema kuwa Balqis amesomea Kifaransa, Alliance Francaise hapo Nairobi. Balqis alisoma Kifaransa kupitia  Alliance Française, Nairobi. Vile vile, anayo shahada ya CPA (K), ambayo inapatikana kwa kufaulu sehemu sita zote za mitihani hiyo ya wahasibu wataalamu iliyo  chini ya usimamizi wa Bodi ya Wahasibu Wataalamu wa Kenya na Sekretarieti za Mitihani ya Taifa (Kenya Accountants and Secretaries National Examination Board, KASNEB). Pamoja na kusoma masomo ya dini ya Kiislamu amekuwa akijituma kujifunza Kiarabu anapokuwa peke yake. Na ameendelea kwa hilo kwani sasa ameweza kuthubutu kusema, “Hakuna anayeweza kunisema kwa kiarabu nikiwa hapo hapo.”

Tarehe 30 Januari 2010, Nairobi, alizaliwa mtoto mwingine. Balqis alibarikiwa kuwa na mtoto wa pili na siku 7 baada ya kujifungua, mtoto akaitwa rasmi jina la Ahmad. Balqis Chelangat kwa sasa ameshakuwa mama wa watoto wawili, Muhammad na Ahmad.

Njia ya Mawasiliano:

P.O. Box 102489 – 00101

Nairobi,

Kenya.

Barua pepe: balqischepkwony@yahoo.com

simu: +254722941896

REJEA


[1]. Ahmad # 22565. Imethibitishwa kuwa swahih na Albaaani katika al-Silsilah al-Da’eefah, hadith na.5

* Tazama katika Fataawa al-Lajnah al-Daa’imah li’l-Buhooth al-‘ILmiyyah wa’l-Ifta’, 15/9: {“Bima ya maisha ni aina ya bima ya biashara, ambayo ni haram, kwani ina kamari, kubahatisha, riba na kuchuma mali kusikofaa. Hairuhusiwi kufanya kazi katika makampuni ya bima, kwa sababu unajumuika kuiendeleza dhambi jambo amablo pia Allah amelikemea, kama asemavyo: “…Na saidianeni katika wema na uchamngu. Wala msisaidiane katika dhambi na uadui. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Q 5:2]}

[2]. Ibn Maajah # 2144, imethibishwa kuwa swahiih na Al-albaani katika Saheeh Ibn Maajah.

[3]. Al-Uthaimin, Al-Allamah Muhammad bin Salih. Commentary on Shaykh Al-Islam Ibn Taymiyyah’s Al-Aqidah Al-Wasitiyyah. Riyadh: Darussalam, 2009. Vol. 1. p. 302.

[4]. Dkt. Michael H. Hart aliandika kitabu alichokiita The 100: A Ranking of the Most Influential Persons in History (Orodha ya Watu 100 Mashuhuri Walioacha Athari ya Mafanikio Katika Ulimwengu Huu) na akiwashangaza wengi, aliona ni mtu mmoja tu aliyefaa kushika nafasi ya juu kabisa katika orodha hiyo naye si mwengine bali ni Mtume Muhammad. Tazama Hart, Michael H. The 100: A Ranking of the Most Influential Persons in History. New York: Kensington Publishing Corp., 2000.p.3.

[5]. Muslim Bk. 25, No. 5325. Tazama pia Bukhari Vol. 8, Bk. 73, No. 207; Bukhari Vol. 8, Bk. 73, No. 216; Bukhari Vol. 8, Bk. 73, No. 217.

* Pamoja na hivyo, Mtume alishasikika akisema: “Mimi nina majina mengi, Muhammad, pia naitwa Ahmad, Maahi (aliyefuta) ambaye Allah akafuta ukafiri kupitia yeye. Mimi pia ni Haashir ambaye atafufuliwa mwanzo siku ya Qiyama. Mimi pia ni ‘Aaqib (wa mwisho katika kuja Mitume na pia hakutakuwa na Mtume baada yake).” Angalia Tirmidhi Chapter 51, Hadith No. 1 (360).

[6]. Brown, Laurence B. MisGod’ed: A Roadmap of Guidance and Misguidance in the Abrahamic Religions. USA: BookSurge Publishing, 2007.p. 219.

[7]. Ehrman, D. Bart. Jesus Interrupted. Front Flap. New York: HarperCollins Publishers, 2009. ; Also see “Cover Content From the Publisher.” bartdehrman.com. Retrieved on 25 Nov. 2009. <http://www.bartdehrman.com/books/jesus_interrupted.htm&gt;

[8]. Professor John Rogerson of Sheffield University, in The Expository Times, 113/8, p.255.

[9]. New Catholic Encyclopedia. Vol 10, p. 989.

[10]. Nugent, Helen and Nadia Menuhin. “Muhammad is No 2 in boy’s names.” The Times 6 June 2007.

[11]. Browne, Anthony. “The Triumph of the East.” The Guardian 27 Jan. 2005.

[12]. Hofmann, Murad Wilfried. Religion on The Rise: Islam in the Third Millennium. Maryland: Amana Publications, 2001.p. 183.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on November 16, 2012 in Waliosilimu

 

Tags: , , , , ,

Michael Wolfe

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

“Muda wowote utakaochukulia dini mzaha, basi wewe ndio utakayechekwa.”

~ Michael Wolfe

Pamoja na kuwa Rais na prodyuza mkuu wa mfuko wa Unity Productions, Michael Wolfe (aliyezaliwa 3 Aprili 1945, Marekani) ni mtunzi wa vitabu vya kishairi, hadithi za kubuni, za masafa na historia. Pia ni mhadhiri wa masuala ya kiislamu katika vyuo vikuu nchini Marekani, vikiwemo kile cha Harvard, Georgetown, Stanford, SUNY Buffalo, na cha Princeton. Ana shahada ya fani ya fasihi (sanaa)  kutoka Chuo Kikuu cha Wesleyan.

Ana asili ya dini mbili, Uyahudi kutoka kwa baba na Ukristo kutoka mama yake. Hivyo alikuwa na fursa ya kusherehekea sikukuu zote Hanukkah na Krismasi. Anaandika:

“Baba yangu ni Myahudi, mama ni ni Mkristo. kutokana na uchotara wangu, mguu mmoja upo katika Uyahudi na mwengine upo katika Ukristo. Imani zote zilikuwa hazina mashaka kwangu. Hata hivyo, ile iliyokuwa inahamasisha ‘wao wao tu’ (waliobarikiwa) [Uyahudi] niliiona haiungani mkono nami, na ile nyengine iliyojaa mafumbo [Ukristo] haikunifurahisha

Kutembea kwake kwingi na kupenda vitabu kulimfanya kuufahamu Uislamu ambao kani (nguvu  ya uvutano) yake ilishindwa kuzuiliwa na Michael. Moja ya sababu iliyomfanya akubaliane na Uislamu ni kukuta katika Uislamu mambo yanayoendana na matakwa yake. Hivyo anasema:

“Sikuweza kuorodhesha mahitajio yangu yote, lakini angalau nilikuwa najua kipi nikifatacho. Dini niitakayo mimi ni dini itakayoweza nieleza kuhusu metafizikia (falsafa ya kuchunguza chanzo cha uhai na maarifa) kwani metafizikia ndiyo sayansi. Sitaki ile inayopongeza utumizi duni wa akili, au iliyojaa mafumbo ili kuwaridhisha wachungaji. Isiyokuwa na wachungaji (viongozi), isiyokuwa na tofauti kati ya uasili na vitu vyake vilivyobarikiwa. Ambapo kutakuwa hakuna vita na nyama. Tendo la ndoa liwe ni la asili tu na sio eti kutokana na laana waliyopewa viumbe. Mwishowe, nilitaka ibada ya kila siku itakayoongoza nidhamu yangu. Zaidi ya yote, nilitaka jambo lililo wazi na uhuru wa kweli. Sikutaka niwe katika mkumbo wa kufata vitu kibubusa.* Na kila nilivyokua nausoma Uislamu, ndivyo ulivyokuwa ukiafikiana na matakwa yangu.”

Michael wolfe amekuwa Muislamu akiwa na miaka 40, baada ya kushindana na imani tofauti tofauti kwa miaka 20. Ingawa inatosha kwa mtu kufanya Hijja mara moja tu katika maisha, Bw. Wolfe katika kugombania kwake kupata radhi za Mwenyezi Mungu, amehiji si chini ya mara tatu, Hijja yake ya mwanzo ikiwa mwaka 1991. Akiuona ukweli wa Uislamu na ujinga wa baadhi ya watu katika faida ya Uislamu, Michael aliona haja ya kuandika haya:

“Rafiki zangu walioathiriwa na siasa hawakuridhishwa na chaguo langu jipya. Wote walichanganya Uislamu na viongozi madhalimu wa Mashariki ya Kati waliodhaniwa kutaka kufanya mapinduzi ili watawale. Vitabu walivyosoma, habari walizotazama vyote vilichukulia dini hii kama mpango wa kisiasa tu. Halikuwapo linalosemwa kuhusu ibada zake. Napenda kumkariri Mae West kwao pale alivyosema: “Muda wowote utakaochukulia dini mzaha, basi wewe ndio utakayechekwa.” Kihistoria, Muislamu anaiona dini kama ni hitimisho, mmea uliopevuka ambalo ulipandwa tangu wakati wa Adam. Imejengwa kwa msingi wa kuabudu Mungu mmoja kama Uyahudi, ambayo mitume wake Uislamu unawachukulia kama ni ndugu waliotoka kumoja na kilele chao kikiwa Yesu na Muhammad. kusema kweli, Uislamu umefanya kazi kubwa katika hatua ya kuirudisha ladha ya maisha kwa mamilioni ya watu. Kitabu chake, Qur’an kilimfanya Goethe kusema, “Mnaiona hii, mafundisho yake hayashindwi abadan; pamoja na mifumo yetu yote ya kibinaadam, hatuwezi kufika, na huo ndio ukweli hakuna mfumo wa kibinaadamu utakaofanikiwa”.

Akiongea na mtangazaji Bob Faw kuhusu imani yake mpya. Faw ‘alimpiga’ bwana Wolfe kwa swali hili: “Kwa kuwa ushakuwa muislamu, je kuna tofauti yoyote kwako labda!?” Wolfe akajibu: “Bila shaka ipo, umbile nilokuwa nalikosa zamani maishani mwangu lipo sasa nami. nalihisi kabisa.” Wolfe alivutiwa sana na mafundisho ya Uislamu kuwa kila mtu azungumze na Mungu mwenyewe, bila kuwa na kizuizi katikati:

“Hili jambo la kufanya mazungumzo na Mola wako mtukufu bila kuwa na balozi katikati, kusikohitaji jengo fulani au mtu maalum, kunanipendeza mno.”

Michael Wolfe anajulikana zaidi kwa filamu yake katika kipindi cha Nightline cha ABC iliyorushwa Aprili 18, 1997 ikijulikana kama An American in Mecca (Mmarekani Akiwa Makkah). Kipindi hiko kikateuliwa kuwemo katika tuzo za Peabody, Emmy, George Polk na National Press Club. Filamu ilishinda tuzo ya mwaka kutoka katika Baraza la Waislamu (Muslim Public Affairs Council). Michael Wolfe alishiriki kutengeneza, na kusimamia uhariri wa filamu ya masaa mawili iliyohusu maisha ya Mtume Muhammad iliyoitwa Muhammad: Legacy of a Prophet. Filamu hiyo ilioneshwa nchi nzima na PBS na baadae kuonyeshwa kimataifa na National Geograpghic International. Filamu ilituzwa na Cine Special Jury Award kwa filamu bora izungumziayo watu au mahali. Wakati wakutengeneza filamu hiyo, washiriki walihitaji kuperuzi kwingi katika maisha ya Mtume. Michael Wolfe mwenyewe anakiri kusoma Ibn Kathir na vitabu vyengine vya seerah (mwenendo wa Mtume). Kiukweli, kukawa na Wamarekani wengi ambao walisilimu baada ya kuona filamu hii. Katika mahojiano, Islam Online walimuuliza alichovuna  baada ya zoezi hili kubwa la kuandaa filamu hii ya Muhammad na alijibu kama ifuatavyo:

“Nimemjua Mtume vyema zaidi kuliko mwanzo kabla hatujaanza kutengeneza filamu hii japokuwa kumsoma kwangu ndio kwanza kulianza. Kuna mengi ya kujifunza. Wakati tunatengeza filamu hii, niliweza kuona na kufahamu hali ya Waislamu wa Marekani. Najua sasa wepi ni Waislamu na vipi tunafanya. Ni kifungua jicho kwangu mimi kama Mmarekani niliyezaliwa hapa, ni jambo la faraja sana kukutana na watu kutoka sehemu mbalimbali, watu wenye lugha tofauti na mengineyo. Ni moja ya hazina za kuwa Muislamu.”

Katika mahojiano tofauti, Michael Wolfe kama mmoja wa waandaaji wa filamu ya Muhammad: The Legacy of a Prophet, alisema:

Kwa Wamarekani wengi kutokuwa na uelewa wa imani yangu kunanishangaza sana. Japokuwa Uislamu ni dini inayokua kwa kasi zaidi, bado tabia nyingi za Wamarekani kuhusu Uislamu zimekuwa zikitawaliwa na chuki, kuelewa vibaya na hata wakati mwengine uhasama wa wazi. Wana uelewa mdogo tu kuhusu Mtume aliyefundisha dini hii na ipi ni misingi ya ibada zetu. Siasa na mila za watu wa mashariki ya Kati, gumzo la  ugaidi vyote vimeshiriki kukandamiza uelewa wao mzuri wa dini. Ukichukulia kwamba kundi kubwa la Waislamu haliko hata Mashariki ya Kati bali Indonesia, utambuzi huu sema kweli uanapotosha.”

Filamu nyengine alizoshiriki Wolfe katika uandaaji ni Cities of Light: The Rise and Fall of Islamic Spain (Miji ya Muangaza: Kupanda na Kuporomoka Kwa Dola ya Kiislamu Hispania) na Prince Among Slaves (Mfalme Miongoni Mwa Watumwa). Sanjari na hilo, Wolfe ameshiriki katika vipindi mbalimbali vya redio. Anaandika makala maalumu iitwayo “From A Western Minaret” kwa ajili ya jarida la mtandaoni Beliefnet.com.

Kazi zilizochapishwa za Wolfe ni pamoja na The Hadj: An American’s Pilgrimage to Mecca. (New York: Atlantic Monthly Press, 1993. Kina kurasa 352); One Thousand Roads to Mecca: Ten Centuries of Travelers Writing about the Muslim Pilgrimage, (New York: Grove Press, 1997. Kina kurasa 656) ; na Taking Back Islam: American Muslims Reclaim their Faith, (Rodale Press, Pennsylvania, 2003. Kina kurasa 256). Baadhi ya tuzo alizopokea ni pamoja na Lowell Thomas Award, “Best Cultural Tourism Article, 1998”; Marin County Arts Council Writers Award, 1990, na 1983; California State Arts Council Writers Award, 1985. Michael Wolfe alitangazwa mshindi wa Tuzo ya  2003 ya Wilbur Award kwa kitabu bora cha mwaka kuhusu dini. Anaishi mwishoni mwa mtaa salama, uliofungwa, huko Santa Cruz.

[* Kamusi ya TUKI imetafsiri neno ‘dogma’ (ububusa) kama imani inayofundishwa katika  kanisa unayotakiwa kuikubali bila kuisaili (kuhoji).]

Njia ya Mawasiliano:

Anuani:

Unity Productions Foundation (UPF)
P.O. Box 650458
Potomac Falls, VA 20165-0458
Fax (703) 738-7044

info@upf.tv

 

Tovuti:

http://www.michaelwolfeauthor.com

http://www.upf.tv/

REJEA

[Wolfe, Michael. The Hadj: An American’s Pilgrimage to Mecca. New York: Atlantic Monthly Press, 1993; “I Had Not Gone Shopping for a New Religion.” Turkish Weekly 10 May 2007; Marquis Who’s Who in America. 40th Edition; Stanley, Alessandra. “The TV Watch; A Portrait Of the Prophet Behind Islam.” The New York Times 18 Dec.2002; “Profile: Muslim Converts.” Religion & Ethics Newsweekly. Pbs.org. 8 Oct. 2004,   Episode no. 806 <http://www.pbs.org/wnet/religionandethics/week806/profile.html#&gt;; Wolfe, Michael. “Interview: Michael Wolfe, co-producer of Muhammad: Legacy of a Prophet.” Islamonline.net <http://www.islamonline.net/servlet/Satellite?c=Article_C&cid=1158658340050&pagename=Zone-English-ArtCulture%2FACELayout&gt;; Michael Schwarz, Michael Wolfe and Alex Kronemer. “Muhammad: Legacy of a Prophet: Interview with the Filmmakers.”kqed.org <http://www.kqed.org/press/tv/muhammad/interview.jsp>%5D

 
Leave a comment

Posted by on November 16, 2012 in Waliosilimu

 

Tags: , , , , ,

Sarah Joseph

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Huyu anatokea katika familia ya Kikatoki ya Uingereza ambayo mizizi yake inatokana na uvamizi wa Norman (Norman Conquest). Mama yake alianzishaa uwakala wa kwanza wa mitindo Uingereza na Joseph anadai kuzunguukwa na watu wazuri zaidi hapo katika ofisi za mitindo mtaani kwao.

Mtoto huyu Mkatoliki babake akiwa mhasibu na mamake aliyekuwa mwanamitindo anakumbuka alivyokuwa na umri wa miaka 14 akimkimbilia Naomi Campbell akiwa na kadi ya biashara ya mama yake. Na katika kipindi kifupi baadae, kaka yake akawa Muislamu. Akijilazimisha kupingana na chuki zake kwa Waislamu, Sarah akaanza kusoma dini. “Taratibu, Uislamu uliendelea kunijibu maswali yangu ambayo yalinitatiza mpaka pale nilipoutaka Uislamu wenyewe,” anasema. Na alivyotimu miaka 17, Sarah alibadili dini kuwa muislam, akiukana Ukatoliki aliolelewa nao. Akaamua kuwa mvaaji hijab, vazi lililompa ukombozi na taadhima. “Nataka nihukumiwe kwa kile ninachosema, na sio kwa vile ninavyoonekana,” alishawahi kusema hivi.

Katika mahojiano na Gabrielle Procter, Sarah Joseph alisema:

“…Kuwa Muislamu kunakupa haiba nzuri lakini kubwa zaidi sasa ni binaadamu kikwelikweli. Nimeishi miaka 16 nikiwa sio muislam, sasa hivi mimi kama mwanadamu, mwanamke, mama, mhariri, na mwenyeji wa London- vyote hivi vinanisaidia. Lakini jukumu langu kama mama linanyooshwa na kuwa Muislamu; kazi yangu kama mhariri, na ufahamu wangu kama mmoja wa wanajamii vyote vinanyooshwa na falsafa yangu hii mpya… mimi ni mtu wa imani na naamini mtu wa imani yapasa awe na matumaini. Nawaona vijana wengi wanaojumuika katika jamii mbali mbali za kiengereza wakiwa waerevu, fasaha, wenye msukumo wa kuleta tija katika jamii yao na wakiwa sehemu ya jamii ya kiislamu. Nadhani Waislamu wana uwezo wa kuchangia pakubwa katika jamii. Na kama watu ikatokea wauone uislam ni sehemu ya utatuzi badala ya kuuona ni sehemu ya tatizo, wataishi kwa raha mustarehe.”

Sarah amepata shahada yake ya kwanza katika masomo ya dini kutoka Chuo Cha King cha London. Alifanya utafiti kuhusu Waingereza Wanaosilimu akisomea shahada yake ya pili. Pamoja na hilo, amekuwa mshindi wa 1999-2000 wa shani ya kusomeshwa bure kutoka katika mfuko wa King Faisal Foundation/ Prince of Wales Chevening. Ni mhariri wa jarida la Emel (jarida la kiislamu linalosomwa zaidi Uingereza- jina lake linasomeka M na L likisimama badala ya Muslim Life (Maisha ya Muislam), likimaanisha ‘tumaini’ kwa lugha ya Kiarabu). Pia ni mtangazaji wa British Muslims, na ni mwandishi. Sasa, akisomea shahada nyengine amekuwa akifanya kazi kwa muda kama mwalimu wa chuo ambaye amekuwa akifanya mihadhara mingi na sehemu  nyingi inayohusiana na masuala ya dini na wanawake. Mwaka 2004, alitunukiwa OBE (Tuzo ya Uingereza inayosimama badala ya Order of the British Empire), kwa mchango wake katika midahalo ya dini. Sarah kashajumuika katika vipindi vingi vya televisheni za Uingereza vikiwemo –Panorama na Johnathan Dimbleby. Pamoja na kufanya kazi kama mtafiti mzoefu katika kitengo cha kujifunza cha BBC 2001 Islam Series. Pia amekuwa mhariri mkuu wa kwanza mwanamke wa gazeti kubwa la Waislamu: Trends. Sara Joseph ni mhariri muanzilishi wa baraza la Waislamu la Uingereza The Common Good Consultant on Islamic Affairs– likishughulika na utafiti na mafunzo kwa wale wanaoihitaji kuajiriwa, kusoma, kuwa na afya bora, polisi n.k. katika misingi ya Kiislamu.

Ameolewa na Mahmud ar-Rashid,  mwanaharakati wa haki za binadam. Miongoni mwa vyama vya vijana na jamii ambavyo ar-Rashid anaongoza ni: the Muslim Council of Britain (MCB), baraza kuu la kutetea Waislamu Uingereza na ni pia mwenyekiti Islamic Society of Britain. Wana watoto watatu tayari: Hasan, Sumayyah na Amirah.

Akiongelea kuhusu makundi ya watu wanaoingia katika Uislamu kila kukicha, hususan kwa kutumia makadirio ya watu 10,000 mpaka 50,000 wanaoingia katika Uislamu kila mwaka Uingereza, Sarah anadhani kufikia mwaka 2020, Uislamu itakuwa ndio dini inayofatwa zaidi Uingereza, “Sisi ni wa pili kwa kuwa na idadi ya wafuasi wengi Uingereza ila ifikapo 2020 tutakuwa tunaongoza rasmi kwa kuwa na waumini wengi wahudhuriaji ibada zao kama ukitumia uhudhuriaji wa kanisa na msikiti kama kigezo,” Alisema hayo kuiambia GDN.

Njia ya Mawasiliano:

Anuani: Studio 8,

The Whitechapel Centre,

Myrdle Street,

London E1 1HL

Tovuti:

http://www.emelmagazine.com

http://www.emelmagazine.co.uk

Barua pepe: info@emelmagazine.com

REJEA

[Wavell, Stuart. “Putting a good glossy on the Muslim lifestyle.” The Sunday Times 9 Oct. 2005; Joseph, Sarah. “Interview: Sarah Joseph, Emel magazine.” By David Rowan. Evening Standard 20 July. 2005; Joseph, Sarah. “The freedom that hurts us.” The Guardian 3 Feb. 2006; “Being Muslim shapes you, but first and foremost I’m a human being.” The Guardian 30 Nov.2004; “Emel’s Hope.” Saudi Aramco World. March/April 2004.]

 
1 Comment

Posted by on November 16, 2012 in Waliosilimu

 

Tags: , , , ,

Musa Cerantonio

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

“Nakumbuka baba yangu alinifundisha nichukulie maisha kama mchezo wa “chess”. Usifikirie kete moja tu ndiyo isongayo mbele, fikiria kete 10 zinaenda na ujanja huu utakuokoa, usizame kwenye mitego.”

~ Musa Cerantonio

Alizaliwa na kukulia Melbourne, Australia. Anatoka katika familia ya watoto 6. Alisilimu 2002 mwezi wa Ramadhani akiwa na miaka 17. Amesomea Historia na Mawasiliano (History and Communication) chuoni na baadae akajiendeleza kwa kusomea Historia ya Kiislamu. Amekuwa Rais ( Mwenyekiti ) wa Jumuiya ya Waislam wa Chuo Kikuu cha Victoria, hukohuko Melbourne. Ni baba wa watoto wawili, Aisha na Swafiyah. Musa ana asili ya Italia kwa baba, na mama mwenye asili ya Ireland. Italia likiwa taifa kiongozi kwa kufuata ukatoliki, kama ilivyotarajiwa, hata Musa Cerantonio naye alilelewa Kikatoliki. Alikuwa akiamini bila shaka kuwa kama Ukristo ndiyo dini yenye wafuasi wengi, na ukatoliki ambao yeye yumo ndani ndiyo kundi kubwa la Ukristo, bila shaka hiyo ndiyo dini ya kweli.

Sasa vipi alisilimu? Kama alivyojibu katika mahojiano, “ilikuwa safari ndefu iliyonichukua miaka miwili ya kusoma na kufuatilia Uislamu.” Na sasa twende tupite njia alizopitia yeye. Musa alisoma shul ya Msingi ya kikatoliki na kuingia shule ya sekondari ya kijamaa. Rafiki zake ambao wengine walikuwa waislam, walikuwa watumizi wa madawa ya kulevya na mengineyo ya kihuni, ila yeye alijilinda. Shule ya sekondari aliyoenda ilikuwa imejengwa kwa itikadi ya Kijamaa na hata katika midahalo ya shule, Musa alikuwa ‘akiwaka’ dhidi ya itikadi hizo za Kijamaa. Musa alipinga vikali mawazo ya kina Karl Marx aliyesema “dini ni kasumba tu ya watu” au “Mungu amekufa” ya Friedrich Nietzche. Ili Cerantonio aitetee dini yake, ilimpasa aisome na punde akaanza kusoma Biblia, alishtushwa na aliyoyakuta. “Baadhi ya visa vya Biblia ni vya kiasherati, ni vya kiponografia (matusi yenye kutia ashiki),”alisema, na kama mfano, Musa alitoa kisa cha Lut aliyeleweshwa na watoto zake wa kike. Sijui nimalizie!? Dah! Wacha niseme tu! Watoto wale wakafanya mapenzi na baba yao  kwa masiku mawili ili kulinda nasaba ya baba yao (Mwanzo 19:30 – 36). Alishangaa inakuwaje visa kama hivyo viitwe Neno la Mungu? Hii ndiyo sababu ya Dkt. Lawrence Brown, mchungaji, hakuamini ile kauli inayosema ati “Maandiko yote Matakatifu yameandikwa kwa uongozi wa Mungu, na yanafaa katika kufundisha ukweli, kuonya, kusahihisha makosa, na kuwaongoza watu waishi maisha adili” [2 Timotheo 3:16, Biblia-Habari Njema (Good News)] ya visa hivyo. Katika kitabu chake, MisGoded, Dkt. Brown aliandika kuwa, katika Biblia:

“….Kuna hadithi za walevi walio uchi, kujamiiana kwa maharimu (au ndugu) na umalaya ambao hamna mwenye haya anayeweza kumsomea mama yake, au kwa watoto wake. Na bado, moja ya tano ya kundi la watu duniani linakiamini kitabu kinachosema Nuhu “akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.”( Mwanzo 9:22 ) na kile cha,

“Lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani, na binti zake wawili pamoja naye, kwa sababu aliogopa kukaa katika Soari. Akakaa katika pango, yeye na binti zake wawili.  Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna mtu mume katika nchi atuingilie kama ilivyo desturi ya dunia yote.  Haya, na tumnyweshe baba yetu mvinyo, tukalale naye, ili tumhifadhie baba yetu uzao. Wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka huyo mkubwa akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.  Ikawa siku ya pili, mkubwa akamwambia mdogo, Tazama, nimelala jana na baba yangu, tumnyweshe mvinyo tena usiku huu, ukaingie ukalale naye.  Wakamnywesha tena baba yao mvinyo usiku ule, akaondoka mdogo akalala naye, wala yeye hana habari alipolala wala alipoondoka.  Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao.” [Mwanzo 19:30-36]

Kwa maelezo kamili na ushahidi kuhusu hadithi zenye uasherati na kupotoka kama ukahaba na zinaa angalia (Mwanzo 38:15 – 26), kuhusu ukahaba (Kitabu cha Waamuzi 16:1), mkengeuko (2 Samweli 16:20 – 23), umalaya (Ezekiel 16:20 – 34 na 23:1 – 21), uzinzi (Methali 7:10 – 19), ubakaji baina ya ndugu kama ule aliofanyiwa Tamari katika 2 Samweli 13:7 – 14 inaonesha maadili ya ajabu, na Tamari (aliyebakwa) alishauriwa kwa kuambiwa, “sasa tulia, dada,” kwani, “[Huyo mbakaji, Absalomu] ni nduguyo; usilitie moyoni jambo hili.” (2 Samweli 13:20). Mh! Mbakaji akiwa kaka yako hakuna tatizo!!? Je ni kweli tuendelee kuamini “Hekima” hizi ni matendo ya uteremsho kutoka kwa Mungu?, au ndoto chafu tu?[1]

Mshituko mkubwa kwa Musa ulikuja pale alipogundua kuwa sheria za Biblia hazifuatwi na Wakristo. Mathalan, aligundua kutoka katika Biblia kuwa wanaume wanapaswa kufuga ndevu lakini Papa na Wakristo wengi wananyoa. Biblia inaelekeza watu waepuke mvinyo lakini kanisani Jumapili, mchungaji anawapa wanywe; Biblia inakataza kula nyama ya nguruwe lakini wengi wa Wakristo wanaifanya nyama ya mnyama mchafu huyo na mwenye magonjwa mengi kuwa chakula chao kipenzi. Musa akaamua kufuata amri za Biblia, akaanza kufuga ndevu na kuacha pombe na nguruwe. Familia ilipomuuliza akajibu, “Biblia ndivyo inasema.” Wakawa wanamuwakia kumwambia, “hilo ni Agano La Kale.” Na yeye akashangaa inakuwaje wakataze maneno ya Mungu na kufuata baadhi! Musa Cerantonio akaamua kuwapa changamoto kwa kuwauliza, “Mnakubali ndoa za Jinsia moja?.” Bila shaka jibu ni  “hapana” ndipo Musa akawambia kuwa kupigwa marufuku kwa ndoa hizo zatokana na Agano La Kale. Akaona huu ni unafiki kufuata baadhi ya sheria na kuacha nyengine. Musa hakuwa na furaha kwa kitendo kile cha kuchagua ya kufuata na mengineyo ya kuyaacha, ndiyo sababu wakati mwingine alichukulia Ukristo kama mgahawa, ambapo unaenda unaagiza chakula ukitakacho na kwa vile usivyotaka vinakuwa havikuhusu. Katika mahojiano yake na Saudi Gazette, aliombwa ahadithie alivyopita katika njia mpaka akaufikia Uislamu, Musa alijibu kwa kusema:

“ Nilikuwa nikisoma Biblia na nikagundua nguruwe ni haramu, lakini Wakristo cha kushangaza wanakula. Nikashangaa kuona Wakristo wasivyoifuata Biblia. Nikajiona nasogea karibu na uislam na hapo nikaamua kusoma. Niligundua kumbe hadi Waislamu wanamuamini Yesu (Amani iwe juu yake). Nikajiambia, inaonekana Uislamu ni mzuri ngoja niusome zaidi.

Kwa hamu yake ya kuujua ukweli, Musa alitembelea Vatican  mwaka 2000. Jiji la Vatican ni dola huru iliyo ndani ya jiji la Rome, Italia. Ulikuwa ni mwaka wa Jubilii (Sikukuu ya Ukumbusho) ambayo kwa ukatoliki ulikuwa ni mwaka maalumu wa kutolewa dhambi na kuomba msamaha. Aliambiwa, mtu akiingia kupitia “ mlango mtakatifu” (unaojulikana kama Porta Santa kwa lugha ya Italia), madhambi yake yote yanapukutika. Musa hakulimezea hilo bali aliuliza, “Jambo hili limezungumzwa wapi katika Biblia!?” na hakupata majibu ya kumridhisha. Na alipoamua kuingia kupitia mlango ule, alishituka kuona mwili uliokaushwa wa mapapa wa zamani na chakushangaza zaidi, watu walikuwa wakiuabudu. Aliona pia watu wakifuta miguu ya sanamu na kuomba waliyoyataka. Akaingia hadi chumba cha Papa (Capella Sistina) na akaona kwenye dari kuna michoro mbalimbali ikiwemo picha ya Mungu mwenyewe (alieonekana kama kikongwe na mwenye ndevu zenye mvi) na Adam! Hakuweza kushabihisha  alichoona na amri ya pili ya Biblia: “Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.” [Kutoka 20:4]. Musa Cerantonio alipinga  yote hayo na akaanza kujiita Mkristo asiye na dhehebu lolote, mtu fulani anaye amini Mwenyezi Mungu na asifate kanisa lolote. Na ilikuwa ni katika kipindi hiki ndipo alipoanza kusoma dini nyingine kama Uhindi, Ubudha, Shinto, lakini kamwe hakufikiria Uislam.

Baada ya kipindi fulani, alijitokeza Muislamu aliyemwambia, “Naona faraja kukutana na wewe, jina langu ni fulani, je ungependa kuwa muislam?” Hili lilifungua milango kwa yeye kujifunza uislam kwani kwa chochote Musa alichotaka kujua katika uislam alimuuliza mtu huyo. Muislam huyu alimpatia Musa Qur’an, lakini Musa hakuisoma. Musa aliipokea tu Qur’an na akaihifadhi pahala, kaka yake alipoigundua kuwa ni Qur’an, aliichukua na kuichoma. Kuna wakati alikutana na marafiki zake Waislamu, miongoni mwa hao waislam, mmoja wao alikuwa haujui uislam vizuri. Katika maongezi yao na Musa, alikuwa akimtusi Yesu bila ya kujuwa kuwa alikuwa mmoja wa Mitume wakubwa wa Allah. Hili lilimjaza wahaka Cerantonio na akaamua kidhati kuusoma uislam ili kuishambulia imani hiyo ya waislam. Katika kusoma kwake, cha kwanza alichogundua kilikuwa ni waislam wanamuamini Yesu Kristo. Lingine aligundua kuwa Waislam wanaamini Mungu Mmoja na hawamshirikishi. Kila alivyousoma zaidi, ndivyo alivyotaka kuujua zaidi. Kwa vile alivyokuwa ameusoma Uislamu kiundani na kuuelewa, ilifika kipindi hadi baadhi ya rafiki zake Waislam walikuwa wakimfuata na kumuuliza maswali mbalimbali ya kiislam (wakitaka wapewe Fatwah kuhusu hayo maswala yao). Kipindi muhimu kilicholeta athari kubwa ni pale rafiki yake mmoja alipompa DVD ya Abdul-Rahim Green (Mzungu aliesilimu vilevile), inaonesha jinsi alivyosilimu. Baada ya kuangalia video ile, Musa akajitangazia kuwa yeye si Mkristo tena, sio Mkristo na sio Muislam. Ila alianza kufuata matendo ya kiislam kama kuswali kwa kusujudu. Alikuwa bado hajasilimu, na mwezi wa Ramadhani ulipowasili, aliwauliza rafiki zake waislam kama watafunga, alishangazwa kusikia kuwa baadhi yao hawatafunga. Ila yeye alisema, “ Mimi siyo muislam, ila nitafunga mwezi mzima.” Na ukweli ukawa kama alivyo ahidi, kwani mwezi mtukufu ulipowasili, alifunga na kufuturu nyumbani kwa rafiki zake. Alichopendelea zaidi ni “misosi” (vyakula) vilivyopikwa na kupikika vya Waislamu. Hapo nyumbani kwa rafiki yake, alikiona kitabu kimoja kiitwacho “A Brief Illustrated Guide To Understanding Islam” (Mwongozo Mfupi Wa Kuuelewa Uislamu) kilicho haririwa na I.A Ibrahim kilichoongelea miujiza ya Qur’an Tukufu. Musa hakujizuia kukisoma kitabu kile. Na alipomaliza tu , alitamka shahada, “Ash-hadu anlaa ilaaha ila LLah, wa Ash-hadu anna Muhammadan Rasuulullah”, ikimaanisha kuwa, “ Nashuhudia (nakiri) hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah, na Muhammad ni Mtume Wake.”

Musa Cerantonio amesafiri sehemu nyingi za dunia. Na mwaka 2005, alitembelea mji mtukufu wa Madinah. Alikwenda kuishi Misri, na akafanya kazi katika chaneli ya televisheni ya kiislamu inayotumia lugha ya Kiingereza. Katika mahojiano fulani, Yosra Mmarekani aliyesilimu, alimuomba Musa, “………elezea jambo moja lililokuvutia hapa Misri hata ukadiriki kutosita kutamka neno ‘SubhaanAllah’ na Cerantonio alijibu,

“Nakumbuka siku niliyowasili nyumbani kwangu, nilimuuliza mlinzi wapi kuna msikiti uliokaribu na hapa. Aliniambia kuwa, kama nikienda kushoto ipo miwili, nikienda kulia upo mwingine, nikienda moja kwa moja, nitakutana na miwili, pembeni ya gorofa ninalokaa kuna masjid nyengine. Na yote ilikuwa haikuchukui zaidi ya dakika 1. Nimetoka sehemu yenye msikiti mmoja katika eneo zima, nimekuja sehemu  nayochagua msikiti upi niswali katika minane iliyopo karibu!”

Mara ya kwanza kwenda kuhiji ni 2006, na mara ya pili ni 2011. “Sina maneno kuelezea hilo,” Musa alijibu kuhusu alivyojisikia alivyokuwa akihiji, “kwa ujumla ilikuwa faraja. Haikuwa kama nilivyotarajia. Nimejifunza kuhusu umoja wa umma wa Kiislam. Hija pia inakufundisha kuwa mvumilivu. Nimerudi nikiwa mtu mwengine hata familia yangu na marafiki waliligundua hilo.” Katika mahojiano yaliyochapishwa na  The Saudi Gazette, Musa aliulizwa ushauri wake kwa vijana wa Kiislamu, ambapo alisema,

“ Unaona jinsi Magharibi inavyokuwa ya Waislamu; wanamuziki, matajiri na watu wengine mashuhuri wote wanaingia katika Uislamu. Vijana wa kiislamu inapaswa wajiulize inakuwaje watu hawa walioyashinda maisha wawe na pupa hivi kuingia katika Uislamu. Ni kwa sababu ni dini ya haki na wanataka pepo pia. Tambeni kwa kuwa Waislamu.”

Akiongozwa na shauku ya kutaka radhi na thawabu za Allah kwa kuwaita watu katika uislam, Musa Cerantonio amejumuika katika majukwaa tofauti kutangaza Uislamu. Ni mara mbili kashawahi kuhudhuria Kongamano kubwa la Amani la Kiislamu (Islamic Peace Conference) lililofanyika Mumbai mwaka 2007 na 2009, vile vile ameweza kuhudhuria Kongamano kama hilo la Dubai (Dubai Peace Conference) la mwaka 2010. Amefanya mihadhara kuhusu Uislamu katika hafla mbalimbali sehemu nyingi kama Australia, India, UAE, Ufilipino, Kuwait na Qatar. Amefanya kazi Iqraa International, chaneli ya televisheni irushwayo katika satelaiti.katika moja ya vipindi vyake vinavyorushwa na Iqraa International, Musa alimuhoji Lauren Booth, shemeji wa aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza, Tony Blair. Lauren Booth ambaye naye ni mtangazaji, aliingia katika dini hii ya Kiislamu katikati ya mwezi Septemba 2010 na alipania kwenda kuhiji mwaka 2011. Katika mahujiano hayo yaliyofanyika Madinah Al-Munawwarah, Cerantonio alitaka kujua jinsi alivyosilimu na aliuliza pia anavyojisikia akiwa na dini mpya. Kama unatatizwa na swali lolote ambalo unahitaji jibu lake, basi usisite kumuuliza Cerantonio kwani yuko tayari kulijibu papo kwa papo kupitia kipindi chake “Ask the Sheikh” (Muulize Sheikh) kinachorushwa na Iqraa International.

Musa pia ametokea katika chaneli ya muda wote ya bure, Peace TV. Katika moja ya kipindi chake, Musa alitoa “Ushari kwa Waislamu Kutoka kwa Waliosilimu” na anakiri baadhi ya waislamu ndio sababu ya kuzuia watu wasiingie katika Uislamu. Kwa mfano Musa anahadithia kuwa kabla hajasilimu, rafiki yake Muislamu alimsihi Musa asisilimu. Kisa na maana ni kuwa, endapo Musa atasilimu, wazazi wake watakereka na kukasirika, wakitaka kujua, “Nani aliyemsababisha mpaka mtoto wetu akasilimu, nani aliyemvuta katika Uislamu, nani aliyesababisha mwenetu atengane na familia yake na mila zake…” Musa akasema, Waislamu wanawazuia wasio Waislamu kuingia katika dini yao. Na hili linasababishwa na matendo yao. “Kumbuka tabia yako ndio Daawah yako” kwa hivyo Waislamu inabidi watumie tabia zao njema kutangaza dini. “Wengi wa Waislamu niliokutana nao,” Alikiri, “walikuwa na tabia mbaya, wanakuibia, wanaongopa, walikuwa wanafanya kila kitu ambacho Muislamu hatakiwi  kukifanya.” Cerantonio aliwaonya watu wasiwe na tabia ya kulaumu gari katika ajali bali walaumu dereva . “Kwa bahati nikaelewa labda haya ni yale wanayofanya Waislamu lakini kuna lile ambalo Uislamu unalifundisha wacha nilisome hilo.” Musa anaona tabia ya mtu ni njia bora ya kuusambaza Uislamu hivyo anawausia Waislamu wajipambe na tabia hizo njema. Anasema unaweza kufanya jitihada ya kumgaia asiye Muislamu kitabu lakini asikisome, unaweza kumpa CD ya mawaaidha na bado asiisikilize, pia unaweza mkabidhi DVD ya kiislamu na bado asiangalie, sasa ufanyeje ukifikiwa na ugumu huu? Basi jitahidi uwezavyo kutoa Daa’wah kupitia tabia zako. Ushauri huu wa Cerantonio unawafikiana na ule wa mwanazuoni wa kiislamu aliyewaambia wanafunzi wake, “Waiteni watu katika Uislamu huku  mkiwa kimya.” Wanafunzi walishtuka, wasijue ni kwa vipi wanaweza waita watu katika Uislamu bila kunyanyua ndimi zao, naye akawajibu, “Kwa kutumia tabia zenu.”

Cerantonio anaelekeza kuwa, jirani yako, rafiki yako ni Muislamu mtarajiwa kwa hivyo usidharau juhudi zao za kuwabadili watu. Yeye mwenyewe alivutika na Uislamu pia kwa kujua Yesu anameremeta kwa Waislamu. Alishasema, ikiwa utamueleza anayejiita mfuasi wa Kristo kuwa sisi waislmu tunampenda Yesu kuliko yeye basi anaweza kuvutika kujifunza Uislamu. Katika kipindi kimoja cha Peace TV: “My Choice”, Musa alifunga kipindi hicho kwa dua ifuatayo: “Namuomba Allah atufanye tuwe waumini wa kweli wa Tauhiid (kumfanya Mola kuwa mmoja kikweli kweli), tuwe miongoni mwa wale wasiomshirikisha na lolote, na tusimsifu yeye Mungu kwa sifa ambayo hajajisifu nayo Yeye Mwenyewe.”

Njia ya Mawasiliano:

Barua pepe: ask@iqraa.com

REJEA 

[“From Darkness to Light : How the Bible Led Me to Islam? – Musa Cerantonio” 26 Jan 2010. YouTube.com. Online video clip. Accessed on 18 March 2012. <http://www.youtube.com/watch?v=qFuZCL_NbXE&gt;; “How I came to Islam :: talk by musa cerantonio::Part 1” 3 March 2011. YouTube.com. Online video clip. Accessed on 18 March 2012. <http://www.youtube.com/watch?v=Vf2mH-CGQFc&feature=related&gt;; “Advice To Muslims By A Revert 1 – 2 Br. Musa Cerantonio” 4 Nov 2010. YouTube.com. Online video clip. Accessed on 18 March 2012. <http://www.youtube.com/watch?v=3102QDtoqCo&feature=related&gt;; “Pilgrims Reporting on Hajj 2011.” 3 Nov. 2011. YouTube.com.  <http://www.youtube.com/watch?v=Ki8e3cLTUiI&gt; Online video clip. Accessed on 24 March 2012; “Musa Cerantonio, Ex-Catholic, Australia” 5 April 2010. islamreligion.com. Online video clip. Accessed on 18 March 2012. <http://www.islamreligion.com/videos/3551/ >; Bajaeifir, Qais. “Hold your heads high, new Muslim tells youth”. The Saudi Gazette Accessed on 18 March 2012. <http://www.saudigazette.com.sa/index.cfm?method=home.regcon&contentID=20111106111747&gt;; Cerantonio, Musa. “After Hardship There is Ease” Interview by Yosra . 15 March 2012.< http://afterhardship.blogspot.com/2012/03/musa-cerantonio.html&gt; ; CNN iReport, iReporter: MusaAbuAisha.  ireport.cnn.com <http://ireport.cnn.com/people/MusaAbuAisha>%5D


[1]. Brown, Laurence B. MisGod’ed: A Roadmap of Guidance and Misguidance in the Abrahamic Religions. USA: BookSurge Publishing, 2007. pp. 230-231

 
Leave a comment

Posted by on November 16, 2012 in Waliosilimu

 

Tags: , , , , , ,

Kristiane Backer

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Alizaliwa katika jiji zuri salama la Hamburg huko Ujerumani mnamo tarehe 13 Disemba 1966. Maisha yake ya kikazi yalianza akiwa na umri wa miaka 21 pindi alipojiunga na Redio Hamburg kwa mafunzo ya kujitolea ya miaka miwili ya uandishi wa habari. Miaka miwili baadae, Kristiane alichaguliwa kuwa mtangazaji wa kwanza kutoka Ujerumani katika kituo cha muziki cha MTV, huku akiwashinda wengine elfu. Hatimaye mwaka 1989, alihamia London. Akiongelea maisha yake ya huko alikuwa na haya ya kusema:

“Ilikuwa ni raha, nilikuwa na miaka ishirini na, niliishi Notting Hill, nilikuwa mwanadada mgeni pale na nilialikwa kila mahali, nikipigwa picha na Mapaparazi. Nilikutana na watu mashuhuri wengi (kuanzia Robbie Williams hadi Lenny Kravitz), na nilifurahia sana muda wangu kule. Nilitumia kiasi kikubwa cha mshahara katika mavazi. Nilisafiri karibia ulaya nzima, nikitembelea sehemu nzuri nzuri kama Barcelona, Istanbul, Paris; na kuna kipindi nilienda hadi Boston kuwahoji Rolling Stones, na nilikuwa sambamba na mtoto wa mfalme kwa takriban wiki nzima. Nilikuwa mwanadada namba moja katika MTV na nadhani nilikuwa nikionekana kwa televisheni muda wote. Nilitangaza kipindi cha Coca cola Report na kile cha Top 20 za Ulaya. Nilihoji vikundi vingi vya sanaa na mamilioni ya watu walinijua Ulaya nzima. Katika moja ya maonyesho ya muziki wa roki (rock), nilisimama jukwaani mbele ya watu 70,000.”

Backer  alishawahi kupokea tuzo nyingi za televisheni, zikiwemo The Golden Camera na mbili za Golden Ottos. Pamoja na kutembea sana Ulaya, pia alipata nafasi ya kutembelea Mashariki. Baadhi ya nchi alizotembelea ni Morocco, Misri, Uturuki, Pakistan, Syria na Saudi Arabia. Anasema, “Safari zangu nyingi katika maeneo ya Waislamu kumenifanya nilime mengi kutoka katika jamii hizo ambapo ikaniwezesha kuvuna maarifa makubwa ya dini na maisha yao.’

Mwaka 1992, alikutana na Imran Khan, nahodha wa timu ya kriketi ya Pakistan. Hiyo ndio ilikuwa mara yake ya mwanzo kukutana na Muislamu na kujadili mengi kuhusu dini hiyo. Alimpatia vitabu kadhaa vya dini na Kristiane akajitolea muda wa kuvisoma. “Nilianza kuhoji maoni na chuki zangu ziso sababu na vichwa vya habari dhidi ya dini hii, nikaanza kuisoma Qur’an na ikaanza kuniingia kichwani,” Alisema.  “Nikagundua kuwa Uislamu ni wa wote, wanawake na wanaume; katika Uislamu wanawake walikuwa na haki ya kuchagua tangu mwaka wa 600. Wanaume walivaa kiheshima, na wanawake pia, hakuna aliyetumia macho yake vibaya [kwa kutongozana] bali kila mtu [kwa ajili ya kutaka stara, haya, heshima na uchaji Mungu] aliinamisha shingo yake chini.”

Alipoulizwa kuhusu zana alizotumia kuujua Uislamu, Kristiane alisema ukiachana na Qur’an pia amesoma vitabu vilivyoandikwa na wasomi kama Martin Lings, Dkt. Seyyed Hossein Nasr, Lei Gai Eaton, Annemarie Mould, Dkt. Zaki Badawi, Murad Hofmann, Muhammad Asad, na wengine wengi. Pia alidiriki hata kuwatafuta wengine kwa kujifunza zaidi. Akiathiriwa na sababu zenye mantiki katika Uislamu, Baker alikubali kuubeba mzigo huo na baada ya kugundua heshima aliyoikosa siku zote, alisema: “Niliacha kuvaa nusu uchi na nikaanza kuvaa sketi ndefu katika TV…Nashangazwa na wanawake wengi wanaopunguza nguo zao ili watolewe katika vichwa vya habari tena katika kurasa za mbele- kusema kweli ni kujishusha thamani yako.

Ilikuwa ni mwaka 1995 ambapo aliuacha Uprotestanti na kusilimu. Sasa anaswali swala tano na kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhan. “Nilikuwa nikitumia vilevi katika sherehe kila siku usiku, lakini sasa sio kuntokuywa tu bali hata kugusa.” Na mwaka 2001, alikwenda Makkah, “Ilikuwa safari nzuri sana, nilirudi nikiwa nafuraha tele na amani moyoni.”

Baadae alijiunga katika Chuo Kikuu cha Westminster na kusomea elimu ya tiba ikiwamo miti shamba, mafuta ya miti, dawa za kichina, uasili wa maua na homeopathy. Mwaka 2002 alifaulu kuwa mtaalamu wa tiba ya homeopathy na Septemba mwaka uliofatia alianzisha kliniki yake kupitia mtandao wa intanet, http://www.energy-for-health.com. Kwa sasa anayo kliniki yake ya homeopathy huko Ujerumani. Pia kajumuishwa katika mpango wa kutengeneza vya kujipambia na vyakula vitokananvyo na dawa za kiasili na mafuta ya miti yanayopatika nchi za Kiarabu.

Ukiachilia masuala ya tiba za kiasili, Kristiane amesomea masomo ya dini ikiwemo dawa za Kisunnah na sanaa ya kiislamu, na elimu ya jamii na siasa kutoka Chuo Kikuu cha Islamat Birkbeck. Anazungumza vizuri Kifaransa na Kiarabu.

Anaendelea kuandaa matukio mengi Ulaya. Amekuwa muandaji mzuri wa mikutano na makongamano. Baadhi ya makongamano yaliyoandaliwa naye ni kama Islamophobia (lilioandaliwa na Islam Channel, Copenhagen), Sage Software Awards (Wiesbaden), Tuzo za Biashara za Ulaya (European Business Awards, Barcelona), European Electronic Awards (Munich), Royal Mail Awards (Berlin), Infineon Supplier Awards 2004 (Munich), Pirelli Calendar 2004 launch “The making off” London, PR Report Awards (Berlin), VW Nick Nickel Gala and awards ceremony, GE Capital IT Solutions for Compuserve European Kick- Off Meeting/ Awards.

Mara kwa mara amekuwa akiandika makala tofauti kuhusu masuala ya afya kwa magazeti ya Kiengereza na ya Kijerumani na pia wakati mwengine akiongelea masuala hayo katika vipindi vya televisheni na redio. Baadhi ya kazi zake zipo katika magazeti kama Time Out, The Daily Express, Compass na Red magazine, BBC Radio The Sadie Nine Show, LBC Jules Eden show, Sky News, ARD TV na NTV. Tangu 2004, Kristiane amekuwa mtangazaji wa tiba za kiasili kila jumatano saa 6:40 mchana (kwa saa za ulaya ya kati) katika muda wa kipindi cha chakula cha mchana Punkt 12 katika kituo kikubwa zaidi cha Televisheni Ujerumani, RTL. Na miongoni mwa vipindi vyake katika PRESS TV ni World Week Watch– mapitio ya matukio ya dunia kwa dakika 23 kitangazwacho na Oscar Reyes pamoja na yeye Kristiane Backer.

Uislamu ndio uliomletea maisha mapya. “Ni zawadi kubwa kuliko zote niliyowahi kupokea.” Alikiri mwenyewe. Tarehe 14 Aprili 2006, aliolewa na mwandishi wa habari Rashid Jaafar.

Njia ya Mawasiliano:

Anuani

Sherif Code 82466573

9 Burnaby Street

London SW 10 OPR

020 73574344

Simu: +44 (0) 20 7351 4344;

Barua pepe:

homeopathy@energy-for-health.com

info@kristianebacker.com

Tovuti:

http://www.kristianebacker.com

 REJEA

[Backer, Kristiane. “Islam is very accessible.” By Sausen Rahal Moussa. Islamic Newspaper 11Oct.2006; http://www.kristianebacker.com.]

 
Leave a comment

Posted by on November 16, 2012 in Waliosilimu

 

Tags: , , , ,

Dkt. Gary Miller

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

“Hakuna mwandishi yeyote hapa duniani mwenye ujasiri wa kuandika kitabu na kusema hakina makosa, lakini Qur’an imediriki kusema haina makosa na inakushajihisha ujaribu kutafuta kama utapata hata moja.”

~ Dkt. Gary Miller

Huyu ni mwanahisabati na mwanatheolojia wa kutokea Canada. Alikuwa akijitolea kufanya kazi za kimishenari za Kikristo katika maisha yake lakini akaja kugundua mambo mengi yenye mashaka katika Biblia. Mwaka 1978 alianza kuisoma Qur’an akitaraji atakutana na mchanganyiko wa ukweli na uongo pia.

Aligundua kwa mshangao kuwa ujumbe uliobebwa katika kitabu hiki cha Qur’an unaendana vilivyo na ule ujumbe uliopatikana katika Biblia baada ya kuchujwa. Akawa Muislamu na tangia hapo amekuwa ni mwenye kufanya mihadhara mbali mbali ya umma kuhusu Uislamu akitokea katika redio na televisheni pia. Vile vile ni mtunzi na wa makala nyingi za kiislamu. Akiwa na mtaalamu wa hisabati katika Chuo Kikuu cha Toronto, aghalabu amekuwa ni mwenye kuchambua jambo kwa utaalamu wa hali ya juu. Na hivyo, Gary Miller akafanya uchanganuzi wake kwa aya za Qur’an na matokeo yakawa ni kujisalimisha kwa mtunzi wake. Hii ni moja ya aya za kitabu hiko:

“Hawaizingatii nini, hii Qur’ani? Na kama ingelitoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu bila shaka wangalikuta ndani yake khitilafu nyingi.” [Q 4:82]

Akiongelea aya hii, Dkt. Miller anasema:

“Moja ya kanuni kubwa ya kisayansi ni ile kanuni ya kutafuta makosa, au kuangalia dosari katika nadharia mbalimbali mpaka itapowekwa sawa (Falsification Test). Cha kushangaza kitabu hiki cha Qur’an tukufu kinawauliza Waislamu na wasio Waislamu wajaribu kutafuta makosa ndani yake na kuwahahkikishia kuwa hawatapata hitilafu hata kidogo…Hakuna mwandishi yeyote hapa duniani mwenye ujasiri wa kuandika kitabu na kusema hakina makosa, lakini Qur’an imediriki kusema haina makosa na inakushajihisha ujaribu kutafuta kama utapata hata moja.

Mwaka 1977, Profesa Miller (akiwa bado Mkristo) alifanya dahalo wa kidini na mwanazuoni mashuhuri wa kiislamu Ahmed Deedat. Na ilipotimu 1978, baada ya kupokea dalili nyingi zaidi zioneshazo ukweli wa Uislamu, Professa Miller aliamua kuwa Muislamu na kuchukua jina la Abdul-Ahad likimaanisha ‘Mja wa Aliye Mmoja (yaani mja wa Mungu)’. Amefanya kazi kwa miaka kadhaa katika Chuo Kikuu cha Mafuta na Madini, Saudi Arabia na kujitolea maisha yake katika kuuhubiri Uislamu kupitia vipindi vya televisheni na mihadhara ya wazi. Gary Miller ametunga makala mbali mbali kuhusu masuala ya dini. Baadhi ya makala zake ni:

►A Concise Reply to Christianity – A Muslim View (Jibu Fupi la Ukristo Kutokana na Muono wa Kiislamu).

►Followers of Jesus (Wafuasi wa Kweli wa Yesu).

►The Amazing Qur’an (Qur’an Yenye Kustaajabisha).

►Some Thoughts on the ‘Proofs’ of the Alleged Divinity of Jesus (Fikra Zetu Katika Yale Yanayoonekana ni Ushahidi wa Uungu wa Yesu)

►The Basis of Islamic Belief (Msingi wa Imani ya Kiislamu)

►The Difference Between the Bible and the Qur’an (Tofauti ya Qur’an na Biblia)

►Missionary Christianity – A Muslim Analysis (Umishenari wa Kikristo – Uchambuzi wa Kiislamu)

►What the Gospels Mean to Muslims (Waislamu Wanaichukuliaje Injili)

Na miongoni mwa mihadhara aliyofanya ni:

►A Concise Reply to Christianity [Jibu Fupi kwa Ukristo, Dakika 34].

►Amazing Qur’an [Qur’an Yenye Kustaajabisha, Saa 1 na dakika 59].

►Communicating Islam to Non-Muslims [Kuuwasilisha Uislmau kwa Wasio Waislamu, Saa 1 na dakika 21].

►History of Religion [Historia ya Dini, dakika 58].

►Islam and Christianity I- Thinking [Uslam na Ukristo Sehemu ya Kwanza- Kwa Kutumia Fikra, Saa 1 na dakika 43].

►Islam and Christianity II- Scripture [Uislamu na Ukristo Sehemu ya 2 – Kwa Kutumia Maandiko, Saa 1 na dakika 53].

►Islam and Christianity Snippets [Mazungumzo Kuhusu Uislam na Ukristo, Saa 1 na dakika 13].

►Islam and Christianity Symposium [Kongamano Kuhusu Uislam na Ukristo, Masaa 2 na dakika 7].

►Islam and Christianity [Uislamu na Ukristo, Saa 1 na dakika 31].

►Muslims Misguided or Misunderstood [Waislamu Wamepotea au Wanaeleweka Vibaya?! Saa 1 na dakika 43].

►Reason and Revelation [Kutumia Akili na Maandiko, Saa 1 na dakika 22].

►Christian Evengelism [Ulokole wa Kikristo, dakika 58]

►Basis of Muslim Belief [Msingi wa Imani ya Muislam, Dakika 53].

►Dialogue: Is the Qur’an or Bible God’s Word Gary Miller, Yusuf Buccas and Walt Stroker [Majadiliano – Kipi ni Maneno ya Mungu Kati ya Qur’an na Biblia, Gary Miller, Yusuf Buccas na Walt Stroker]

►Introduction to Christianity [Utangulizi wa Ukristo, Saa 1 na dakika 32]

►Modern History of Christianity [Historia ya Ukristo, Saa 1 na dakika 17]

►Dialogue: The Place of Scriptures in Christianity and Islam- Gary Miller and Jimmy Swaggart [majadiliano: nafasi ya maandiko katika Uislamu na Ukristo, masaa 2 na dakika 18].

►Impressions on Muslim-Christian Dialogue [Mazingatio Katika Majadiliano ya Ukristo na Uislam].

►What the Gospels Means to Muslims [Waislamu Wanaielewaje Injili, Saa 1 na dakika 20].

Katika moja ya mihadhara yake, alitamka maneno yafuatayo: “Kama ni ukweli, itakusaidia wewe na sio mwengine, kama akili yako iko sawa”. Yawezekana Ukristo haukumsaidia na Uislam umeweza. Tazama video zake kupitia Youtube.

Njia ya Mawasiliano:

Anuani:

King Fahd University of Petroleum & Minerals

P. O. Box 192, Dhahran 31261,

Kingdom of Saudi Arabia.

Simu (Res.): 8606915

Simu (Off.): 8602810

Nukushi: 8602340

Barua pepe: gmiller@dpc.kfupm.edu.sa

REJEA

[<http://www.youtube.com/watch?v=tt473Gk1vOs&gt;; <http://www.thetruereligion.org/priests.htm#miller&gt;; “The Man who Challenged the Quran.” rasoulallah.net <http://www.rasoulallah.net/subject_en.asp?hit=1&parent_id=764&sub_id=7631>Last retrieved 12/05/2009.]

 
Leave a comment

Posted by on November 16, 2012 in Waliosilimu

 

Tags: , , ,

Marry Fallot

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Ni dada mdogo mwenye umbo dogo, mtulivu anayejiheshimu, mzungu wa kifaransa ambae alisilimu mwaka 2002, baada ya kujiuliza maswali mengi ya kiroho ambayo hakupata majibu yake tangu akiwa mdogo akiwa Mkatoliki. “Kwangu mimi, Uislamu ni dini ya ujumbe wa upendo, kuvumiliana na amani,” Fallot alikiri hilo.

Fallot alicheka pale alipoulizwa na mfanyakazi mwenzake kama ana rafiki wa kiume (boyfriend) wa kiislamu ambaye kasababisha yeye kusilimu. “Hawakuamini kama nimefanya hivyo mimi mwenyewe bila ya kuathiriwa na yeyote.” Mary alielezea kuwa aliingia katika Uislamu kupitia majibu ya maswali Uislamu uliyompatia. Aliweka bayana kuwa alipenda njia hiyo kwa kusema: “Uislamu unakukurubisha kwa Mungu. Uislamu ni mrahisi, sahihi na safi. Ni mrahisi kwa sababu uko wazi. Nilikuwa nahitaji muongozo siku zote, kwani mtu anahitaji sheria na tabia za kufata. Ukristo haukunipa hilo.”

REJEA

[Ford, Peter. “Why European Women Are Turning to Islam.” The Christian Science Monitor 27 Dec. 2005.]

 
Leave a comment

Posted by on November 16, 2012 in Waliosilimu

 

Tags: , ,