RSS

Category Archives: Dini Inayokuwa kwa Kasi

Nzi Bilioni Moja Hawawezi Kuwa Makosani

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Ukweli kuwa makundi kwa makundi ya wasio-Waislam kuingia kuukubali nakuingia katika Uislam hakuwezi bado kuthibitisha kama Uislam ndio dini ya kweli. Je tunatakiwa kuchukulia kinyesi kuwa ni mlo mzuri na wa kipekee eti kwa kuwa nzi bilioni hawawezi kuwa makosani?! Au yatupasa tumuamini yule muathirika wa uvutaji sigara ambaye kwa majigambo anatamba kwa kusema: “uvutaji wa sigara ni jambo zuri kiafya kwani mamilioni ya watu wanavuta” mwengine anaweza kuchekesha kwa kuamua kusema kuwa Ukristo ndio dini ya kweli kwa kuwa ndio yenye wafuasi wengi zaidi duniani, lakini kutokana na takwimu na kweli tulizoziona hapo mwanzo kuwa Uislam utakuja karibuni kuupiku Ukristo na hapo tena imaanishe Uislam ndio itakuwa dini ya kweli?! La hasha! Hata watu wangapi waingie katika dini fulani kitakachojalisha ni eidha upo au hamna ukweli utakaowavutia watu wengi. Kweli idadi ni jambo la msingi na kiuhalisia kuna usalama kupitia idadi hasahasa idadi kubwa ya watu kama hao ikawa inaunga mkono ukweli na sio kufata mkumbo wa kufanya kila jambo ambalo unaona watu wanalifanya. Hata hivyo, wengi kama sio wote wa wale waliosilimu walifanya uchunguzi wa kutokuwa na upendeleo kabla ya kuukubali Uislam. Sema kweli jambo hili la Uislam kukua hasahasa kupitia watu kusilimu linahitaji umakini wa fikra zetu na linamuhitaji yeyote yule anayemtambua Mwenyezi Mungu aungalie tena Uislam kwa jicho la moyoni bila upendeleo wowote.

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on November 13, 2012 in Dini Inayokuwa kwa Kasi

 

Tags: , , , ,

Uislamu Unakuwa kwa Watu Kusilimu

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Ni muhimu kuelewa kuwa Uislam haukui kwa kiasi cha kuzaliana sana Waislam tu bali vile vile kwa watu kuupokea na wakaukubali. Marekani pekee, kutokana na gazeti la St. Petersburg Times, “Kila mwaka Marekani, takriban watu 20, 000 wanaingia katika Uislam, ukiachia wale wanaosilimia katika gereza…, halafu hawa wanaosilimu, wengi wao ni wanawake, na tena wengi katika hao ni vijana ambao bado hawapo katika ndoa….”[1] Shirika la habari la NBC liliripoti idadi hiyo hiyo ya wafuasi wa dini zengine wanaoingia katika Uislam mwaka hadi mwaka. Na kutokana na gazeti la New York Times, “Karibia asilimia 25 ya Waislam Wamarekani ni waliosilimu.”[2] Uingereza, gazeti la The Times liliripoti, “. . . katika idadi isiyo na kifani ya Waingereza, wengi wao wakiwa wanawake, wanaingia katika Uislam . . . .”[3] Na mwaka 2004, The Sunday Times lilisema, “…zaidi ya wazungu (waingereza) 14,000  washaingia katika Uislamu. . . .”[4] japokuwa, kutokana na utafiti wa kina uliofanywa na Kevin Brice wa Chuo Kikuu cha Swansea, inakadiriwa kuwa mwaka 2010, kulikuwa na Waingereza (wazungu) 100,000 waliosilimu Uingereza “. . . kukiwa na zaidi ya watu 5,000 wabadilikao, kila mwaka kitaifa.”[5] Utafiti huo ulifanywa na the inter-faith think-tank, iitwalo Faith Matters. Kusema kweli takwimu hizi zinatuhabarisha jambo fulani kuhusu muelekeo wa Uislam mbeleni..

Tugeukie Ulaya katika uchunguzi wetu, tutashuhudia vyanzo vya habari vikikiri Uislam utakuja kuwa dini itawalayo barani ulaya. Kutokana na The Washington Quartely:

“…Waislam watafanikiwa kujumuisha sio chini ya asilimia 20 ya wana ulaya wote ifikapo mwaka 2050. Baadhi washaanza kutabiri kuwa robo ya Ufaransa itakuwa ni Waislam ifikapo mwaka 2025 na kama mwenendo huu utaendelea, Waislam watawapiku wasio-Waislamu kwa idadi huko Ufaransa na hata Ulaya Magharibi yote ifikapo 2050.”[6]

 Patrick Buchanan ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa Marekani, mwandishi, mwanasiasa na vile vile ameshafanya kazi kama mshauri wa Rais (wa Marekani) Richard Nixon, Rais Gerald Ford, na Rais Ronald Reagan. Katika hotuba yake aliyoitoa tarehe 7 Desemba 2001, Buchanan alisema: “Msisahau kuuhesabu Uislam, kwanza ndio imani inayokuwa kwa kasi zaidi barani Ulaya na pia imeshaupiku Ukatoliki duniani. Na kama tunavyoona Ukristo unavyokufa katika mataifa ya magharibi, makanisa yanazidi kupoteza watu na misikiti lukuki kuzaliwa na kujaa.”[7] Mwaka 1999, ukaguzi wa Umoja wa Mataifa ulionesha kuwa kati ya mwaka 1989 na 1998, idadi ya Waislam barani Ulaya imekuwa kwa aslimia zaidi ya mia moja.[8] Kwa sasa, Waislam wanawakilisha karibu asilimia 10 ya watu wa Ulaya yote na tabiri zinaonesha ifikapo mwaka 2025 Waislam watakuwa washafikia asilimia hizo (kumi).[9] Cha kufurahisha sasa! Amsterdam na Rotterdam ndio majiji yanayotazamiwa kuwa wakwanza kwa idadi kubwa ya Waislam ifikapo 2015 tu.[10] Katika makala iliyobeba kichwa cha habari “Ulaya, usimamaji wa magorofa marefu yanaakisi kuinuka kwa Uislam” iliongelewa katika The Christian Science Monitor, Isabelle de Pommereau anaeleza: “Ulaya, Uislam kama dini ikuayo kwa kasi zaidi kuliko zote unajijengea nafasi yake wazi wazi sasa baada ya milongo ya kuswali na kuabudu kwa kujifichaficha kwenye uga na sehemu za nyumba zilizo chini ya ardhi (basements), na sasa unafanikiwa sio tu kabadilisha sehemu zao za kijamii bali pia mandhari ya majiji.”[11] Akijadili mwelekeo wa kubadili mienendo ya dunia, William Van Wishard anatoa taswira akisema, “Kanisa Katoliki linakumbana na uwezekano mkubwa wa kufunikwa na Uislam kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi barani ulaya kwa miaka inayokuja.”[12] Kuna sababu kubwa tatu zifanyazo bara la ulaya kuwa bara lenye Waislam wengi kuliko wafuasi wa dini nyengine, nazo ni 1) Uhamiaji 2) Kuzaliana sana kwa Waislam 3) Wanaosilimu.

Hapa tunavutika na sababu ya tatu kwa kuwa ndio sababu inayotokea kwa haraka na wepesi zaidi. Utabiri maarufu wa Bernard Lewis*unasema bara la Ulaya litakuwa la Kiislam ifikapo mwisho mwa karne hii.[13]

Mwaka 2005, The Christian Science Monitor lilisema: “Japokuwa hakuna takwimu za uhakika, ila kwa mchunguzi makini atagundua tu kuwa maelfu ya wanaume na wanawake wanasilimu mwaka hadi mwaka.[14]  Waislam waliokuwa Ulaya watawabadili wasio-Waislamu wa ulaya kuingia katika Uislam. Eidha Waislam watafanya jitihada kuzishinda roho za wasio-Waislam au watu wa bara la Ulaya watasilimu kufuatia lile shauri la “Nimeamua kubadili dini kutokana na kuvutiwa na tabia njema na nidhamu ya Waislamu” au wanaweza kusilimu ili waweze funga ndoa na Muislamu. Au uwepo wa Waislamu nchi za Magharibi, kutachokonoa wasio Waislamu waweze kujifunza yaliyo katika mila ya Uislamu na vipi waweze kuishi na Waislamu hawa wakali. Hivyo baadhi watatafuta vitabu kama  The Complete Idiot’s Guide to Understanding Islam cha Yahiya Emerick kinachoweza kumsaidia asiye Muislam kujifunza misingi ya Uislamu na kuishi nao. Vile vile, miongozo inayopatikana katika vitabu visivyowatisha kama Islam For Dummies pia vinaweza kuwasaidia wasio Waislamu kutambua misingi na masuala mengine ya Kiislamu. Wengine wanaweza kutumia vitabu vyengine vya kisomi zaidi vya Kiislamu na matokeo yake, wasio Waislamu watakuja kuuelewa Uislamu halisi, ambao ni tofauti kabisa na ule unaofundishwa kupitia vyombo vya habari na mwishowe waukubali kwa kuingia ndani yake. Hapa tunapata ile kanuni ya ‘Uwepo-wako-unavuta-fikra-zangu’. Pengine hii sababu ya tatu ndio iliyojumuishwa katika moja za hotuba za marehemu Gadhafi: “Tuna Waislam wapatao milioni 50 barani Ulaya. Kuna kila dalili zioneshazo Allah karibuni ataupatia ushindi Uislam katika bara hilo tena bila upanga, bila mtutu, na wala uvamizi. Waislam milioni 50 hao watabadilika kuwa bara la Kiislam miongo kadhaa baadae.”[15]

 Ulaya, Uislam unashika nafasi ya pili kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi.[16] Kutokana na mazoea yetu maishani, mwanafunzi shuleni, kama kazoea kupata D anauwezo wa kupanda hadi C na halafu daraja la B. Na kama akiongeza juhudi na kujituma, bila shaka anao uwezo wa kufikia daraja la juu (A). Hivyo, katu haitashangaza kuona Uislam ukiusambaratisha Ukristo na dini zengine zote katika bara hilo la Ulaya. Kama Uislam ni dini ishikayo nafasi ya pili kwa sasa, bado ina nafasi ya kuwa dini itakayoshika nafasi ya kwanza hapo baadae. Katika mahojiano na balozi wa Sweeden nchini Uturuki; Ingmar Karlsson ambaye pia ni dokta wa kitaaluma katika masomo ya dini ya Kikristo katika Chuo Kikuu cha Lund. Pia ni dokta wa Falsafa katika Chuo Kikuu cha Vaxjo na ni mtunzi wa vitabu zaidi ya 10 ameuelezea Uislam kama dini ya nyumbani Ulaya. Alisema katika mahojiano yake hayo: “Wakati nilipokuwa nakua kule Sweeden baada ya vita kuu ya pili ya dunia, kulikuwa na Waislam watatu tu nchini mwetu, watatu huwezi amini!… Sasa hivi Waislam wanawakilisha asillimia 5 mpaka 6 ya wananchi wa Sweeden wote. Na inavyoonesha hii idadi inakuwa siku hadi siku, naamini punde watu watakubaliana nami kuwa Uislam ndio na utakuwa ndio dini ya ulaya.”[17] Pia alishangazwa na wale wasioona mabadiliko ya Uislam barani humo kwa kusema, “Eti watu bado hawajaujua Uislam! Inashangaza watu bado hawajangundua kuwa Uislam ndio dini ya ulaya…”[18] aliongezea.

Kutoka kwa mwanahabari wa Chicago Tribune Evan Osnos ambae alisema: “Kwa Ulaya,…swala sio kipikitakachotawala kati ya umagharibi na Uislam, lakini lipi kati ya madhehebu mengi ya Uislam ndio yatakayo tawala.”[19] Wengine wanaweza wakachukulia yafuatayo kama dalili ya zao la Uislam kushinda barani Ulaya: Bara la Yuropa (Ulaya) litakuwa na misikiti na minara yake mingi kuliko makanisa na majengo mengine ya dini hiyo; Adhana, wito kuwaita watu kufanya ibada ya swala, itavuma kutoka Paris mpaka Rotterdam, hadi Brussels na London; vijana wa Kiislamu wenye ndevu watafurika mitaani; Waislamu wawe viongozi wa nchi katika dola zote za bara hilo; Wakristo sasa wapiganie haki zao za wachache; uhuru wa kujieleza (freedom of expression) kiholelaholela uwe mashakani maana Shariah za Allah zitatawala; maduka ya nguo yanayouza nguo za kike yatakuwa hayakosi Niqaab (hijab ya kufunika uso), hijaab na nguo nyengine nzuri za Kiislamu; wanasesere waliovalishwa hijab nao kujaa masokoni kwa ajili ya watoto kuchezea; wafanyabiashara wanaopenda kuchunguza mahitajio ya wateja wao watashindana kufungua migahawa inayowapatia pizza halali; kuanzishwa kwa taasisi zinazowafikiana na Uislamu kama vyuo vikuu vya wanawake tu (na wala sio ule wa mchanganyiko baina ya wasichana na wanaume); wazungu kutoka Ulaya wengi wawe wazungumzaji Kiarabu kama lugha yao ya pili na pia lugha hiyo ya Kiarabu kufundishwa mashuleni; Madrasah (shule za kufundisha dini ya Kiislamu) za kisasa zitaenea kila kona ya mtaa…

REJEA


[1]. Wiener, Jocelyn (Times Staff Writer). “Young, Female and Muslim.” St. Petersburg Times 7 Oct. 2002.

[2]. Elliott, Andrea. “Muslim Converts Face Discrimination.” New York Times 30 April 2005.

[3]. Berrington, Lucy. “Why Are British Women Turning to Islam?” The Times 9 Nov. 1993.

[4]. Hellen, Nicholas and Christopher Morgan. “Islamic Britain lures top people.” The Sunday Times 22 Feb. 2004.

[5].Taylor, Jerome. Morrison, Sarah.  “The Islamification of Britain: record numbers embrace Muslim faith.” The Independent 4 Jan 2011. Also see: Brice, Kevin. A minority within a minority: A report on converts to Islam in the United Kingdom. Faith Matters, 2011.

[6]. Savage, Timothy M. “Europe and Islam: Crescent Waxing, Cultures Clashing.” The Washington Quarterly Summer 2004. p.28.

[7]. Buchanan, Patrick J. “Coming Clash of Civilizations? Theamericancause.org 7 Des 2001. http://www.theamericancause.org/patcomingclashprint.htm.

[8]. Allen Jr., John L. “Europe’s Muslims Worry Bishops.” National Catholic Reporter 22 Okt 1999.

[9]. “The Intergration of Muslims In Europe.” Oxford Analytica 24 Feb 2009. http://www.forbes.com/2009/01/23/france-uk-muslims-business_oxford.htmllast iliyopitiwa tena 29 Aprili 2009.

[10]. Pipes, Daniel. “Europe or Eurabia?” Australian 15 Aprili 2008.

[11]. Isabelle de Pommereau. “In Europe, skylines reflect the rise of Islam.” The Christian Science Monitor 26 Julai 2007.

[12]. Van Wishard, William. “Major Trends Reshaping The Global context.” Worldtrendresearch.com  http://www.worldtrendresearch.com/major-trends.php baada ya kupitiwa tena 12/09/2009.

[13]. Lewis, Bernard. “Europe and Islam”. American Enterprise Institute. 7Machi 2007 (katika hafla ya chakula cha jioni ya AEI, alipofanya muhadhara Irving Kristol: Washington). Pia tazama Machils, David na Tovah Lazaroff. “Muslims about to take over Europe.” The Jerusalem Post 29 Jan 2007.

* Profesa Bernard Lewis alipokea tuzo ya AEI’s Irving Kristol mwaka 2007. Alifanya utabiri wake hapo juu mwaka 2004.  Hundley,Tom. “Article of Faith for some: Europe Goinng Muslim.” Chicago Tribune 25 Juni 2006

[14]. Ford, Peter. “Why European Women Are Turning to Islam.” The Christian Science Monitor 27 Des 2005.

[15]. Edwards, Ruth Dudley. “Will Britain one day be Muslim?” The Daily Mail 5 Mei 2007. Pia tafuta kupitia Al Jazeera Television. 10 aprili 2006.

[16]. Esposito, John L. “Introduction John L. Esposito.” Katika historia ya Uislamu Oxford. Ed. John L. Esposito. Oxford Islamic Studies Online. 11 machi 2009. Pia angalia: “Observing Islam.” Online Newshour. Pbs.org. 16 Nov.2001. http://www.pbs.org/newshour/bb/religion/july-dec01/islam_11-16.html

[17]. “Islam is and will be Europian religion” Today’s zaman 12 Machi 2007.

[18]. “Islam is and will be Europian religion” Today’s zaman 12 Machi 2007.

[19]. Osnos, Evan. “Islam shaping a new Europe.” Chicago Tribune 19 Des 2004

 
Leave a comment

Posted by on November 13, 2012 in Dini Inayokuwa kwa Kasi

 

Tags: , , , ,

Takwimu Zitaongea Kwa Sauti Zaidi

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Tunaamini takwimu nyingi zitaongea kwa sauti yenye kusikika zaidi kuliko maneno tu ambayo tuliyokuwa tunayatumia. Kama ilivyonukuliwa kutoka katika Kamusi-elezo ya Kikristo ya Dunia (World Christian Encyclopedia: A Comparative Study of Churches and Religions in the Modern World) ikielezea tafiti ya makanisa na dini katika dunia hii ya sasa inasema:

“…Ukristo umepata upungufu mkubwa wa wafuasi katika pande la magharibi mwa dunia na katika nchi za kikomonisti kwa miaka 60 iliyopita. Katika Muungano wa Kisovieti (sasa Urusi), Wakristo wamepungua kutoka asilimia 83.6 mwaka 1900 mpaka kufikia asilimia 36.1 leo hii. Ulaya na Marekani ya Kaskazini, usaliti kutoka Ukristo kuingia katika dini nyengine au kutokuwa na dini kabisa zimefikia 1,820,500 kwa mwaka.  Hii ni hasara na upotezaji mkubwa….”[1]

Kulingana na jarida la Kikristo, The Plain Truth,[2] ambalo vyanzo vyake ni World almanac na Book of Facts 1935, Reader’s Digest Almanac na Yearbook1983, linatutanabaisha kuwa katika kipindi cha miaka hamsini (1934-1984):

Kutokana na takwimu tulizozipata katika jarida hilo, kama tukachukua dini tatu tu jedwali litakuwa kama ifuatavyo:

Makala iliyokuwa katika jarida la The Plane Truth la mwaka 1984 ilisema, “Kinyume na kupungua kwa waumini makanisani huku Magharibi, habari zinaripoti mwenendo na maendeleo ya Waislam yaliyo kinyume kabisa na sisi. Uislam unaweza kuwa ndio dini itakayokua na kuenea zaidi duniani….”[3] Na ni kweli kama ilivyotabiriwa, Uislam sasa ndio dini yenye kukua kwa kasi zaidi duniani. Hata Vatikani wanaukubali ukweli huo kuwa sasa Uislam umeupiku Ukatoliki, “Kwa mara ya kwanza katika historia, hatupo tena juu; Waislam washatupiku,” haya yalisemwa na Monsignor Vittorio Formenti katika mahojiano yake na gazeti la vatikani L’Osservatore Romano. Formenti ambaye ndiye mkusanyaji na mpangaji makala katika kitabu cha Vatikani cha kila mwaka alisema Wakatoliki wamefikia asilimia 17.4 ya watu wote duniani- asilimia isiyoongezeka- wakati Waislam washafika asilimia 19.2 sasa.[4]

Sanjari na hilo, The World Christian Database (WCD) na wale watangulizi wao World Christian Encyclopedia (WCE – Kamusi Elezo ya Kikristo Duniani) walifanyia utafiti wa idadi ya watu katika masuala ya kidini na kuachia matokeo ya chunguzi zao kwa mara kadhaa. Kutoka katika majedwali ya matokeo yao, malingano ya Ukristo na Uislam katika ukuaji yalikuwa kama ifuatavyo:

[Rejea za takwimu zilizotolewa fatilia katika: Barrett, David B., George Thomas Kurian, and Todd M. Johnson. 2001. World Christian Encyclopedia: A comparative survey of churches and religions in the modern world. New York: Oxford University Press. p 4. Pia pitia, “The List: The World’s Fastest-Growing Religions.” Foreign Policy 14 May 2007.]

Akielezea dini zisizikuwa za Kikristo, msimamo wa mtunzi wa WCE ni: “…tunaweza amini kuwa dini hizo ni za uongo na hazifai na tukajaribu kuzivuta katika imani ya Yesu Kristo….”[5] tukiamini kuwa takwimu hizi za ‘dini pingaji’ hazina upendeleo na haziko kwa ajili ya kuwashinda kuwavuta kuingia katika imani ya Yesu Kristo, wacha sisi tuzitumie katika uchambuzi wetu. The World Christian Encyclopedia inatupa idadi ya wote Waislam kwa Wakristo ya mwaka 1900 na ya mwaka 2000. Idadi ya Wakristo mwaka 1900 ilikuwa na 558 056 332 na mwaka 2000 ikawa 2 019 921 366 na idadi ya Waislam katika miaka hiyo hiyo ilikuwa 200 102 284 na 1 200 653 040.[6]

Kanuni rahisi ya kukokotoa asilimia ya ongezeko katika vipindi hivi ni hii ifuatayo:

Sasa, tukitumia takwimu tulizopewa kutoka WCE, tutapata ongezeko la Wakristo kiasilimia litakuwa:

Na baada ya kukokotoa,  ongezeko la Wakristo litakuwa 262%

Tukifanya mahesabu hayo hayo kutumia idadi ya Waislam katika vipindi hivyo.

Tutapata ongezeko la Waislam kuwa ni 500%

Bado, Uislam unaongoza kwa kuwa na asilimia 500% na Ukristo kuwa na 262%. Mwaka 1997, mwanatakwimu kutoka US Center for World Mission alisema kuwa kiujumla idadi ya wafuasi wa Kikristo inaongezeka kwa asilimia 2.3 kila mwaka.[7] Kutokana na Ontario Consultants on Religious Tolerance Uislam unakuwa kwa asilimia 2.9 kila mwaka ambaye ni kasi kubwa kuizidi kasi ya ongezeko la idadi ya watu duniani ambayo ni asilimia 2.3 tu kwa mwaka.[8] Tukichunguza na kufikiri kwa makini, hakuna ugumu utakaibukia katika kukubaliana kuwa kwa mwenendo huu wa Uislam, karibuni kitafika kipindi ambacho Uislam utakuwa ushazivuka dini zote ulimwenguni. Mnamo mwezi Oktoba 2009, gazeti la Kenya The Standard liliibuka na makala ilobeba ujumbe: “Mmoja katika kila wanne ni Muislam katika kipindi hiki ambapo wafuasi washafikia bilioni 1.57 duniani.[9] Takwimu hizi ziliwekwa hadharani na Pew Forum on Religion & Public Life katika ripoti yao ambayo inaheshimika kwa machangunuo ya kinagaubaga kuliko zote inazofanana nazo. Kama mwaka 2000, WCE walisema Waislam walikuwa bilioni 1.2 na baada ya miaka tisa tu Pew Forum waseme Waislam washafika bilioni 1.57. vipi idadi ya Waislam itakuwa baada ya miaka hamsini?! Na tusubiri tuone.

 REJEA


[1]. Barrett, David B. World Christian Encyclopedia: A comparative study of churches and religions in the modern world, AD 1900-2000. New York: Oxford University Press, 1982.p. 7.

[2]. Stump, Keith. W. “A Crucial Half Century of Religion.” The Plain Truth Feb. 1984 p.11.

[3]. Stump, Keith. W. “A Crucial Half Century of Religion.” The Plain Truth Feb. 1984 p.20.

[4]. Richard Owen. “Islam overtakes Catholicism as world’s largest religion.” Times 31 March 2008; also see Kington, Tom. “Number of Muslims ahead of Catholics, says Vatican.” The Guardian 31 March 2008; “Muslims outnumber Catholics.” PRESS TV. 30 Mar 2008 < http://www.presstv.ir/detail.aspx?id=49503&sectionid=3510212&gt; ; Rizzo, Alessandra (Associated Press Writer). “Muslims More Numerous Than Catholics.” ABC News 30 March 2008; CBS News 30 March 2008.

[5].  Barrett, David B. Preface. World Christian Encyclopedia: A comparative study of churches and religions in the modern world, AD 1900-2000. By Barrett. New York: Oxford University Press, 1982.

[6]. Barrett, David B. World Christian Encyclopedia: A comparative study of churches and religions in the modern world, AD 1900-2000. New York: Oxford University Press, 1982.p. 6.

[7]. Greg H. Parsons, Executive Director, U.S. Center for World Mission, Pasadena, CA; quoted in Zondervan News Service, 21 Feb. 1997.

[8]. Robinson, B.A.  “Growth Rate of Christianity & Islam.” religioustolerance.org. 6 Nov. 2001. <http://www.religioustolerance.org/growth_isl_chr.htm&gt;; Pia tazama, Khan, Arshad. Islam, Muslims and America: Understanding the Basis of Their Conflict. Algora Publishing, 2003.p.29.

[9]. Gorski, Eric (AP Religion Writer). “One in every four is a Muslim as followers hits 1.57 billion worldwide.” The Standard 9 Oct. 2009. Pia tizama, Greene, Richard Allen. “Nearly 1 in 4 people worldwide is Muslim, report says.”CNN 8 Oct. 2009; <http://edition.cnn.com/2009/WORLD/asiapcf/10/07/muslim.world.population/index.html&gt;; Beaumont, Peter. “One in four people is Muslim, says study.” Guardian 8 Oct. 2009; Pew Forum on Religion & Public Life. “Mapping the Global Muslim Population: A Report on the Size and Distribution of the World’s Muslim Population.” 8 Oct. 2009.

 
Leave a comment

Posted by on November 13, 2012 in Dini Inayokuwa kwa Kasi

 

Tags: , , ,

Kuyakataa Mabaya na Kuyachagua Mema

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Wengi ya hawa waliorudi*katika Uislamu wanayo taarifu katika Biblia yao isemayo “…kuyakataa mabaya na kuyachagua mema”. [Isaya 7:15], lakini bado wameuchagua Uislam. Kitakachojalisha kama chaguo lao ndio bora na jema ni kina cha utafiti walichochimba na mashiko waliyoyashika ambayo kwa kebehi kubwa yanadharaulika na wengine. Ukifikiria kama walitumia sababu, dalili na uwazi wa akili katika tafiti zao basi bila shaka watakuwa wamechagua chaguo zuri kama alivyosema Thomas Jefferson “Sababu na uchunguzi wa wazi ndio njia pekee za kushinda makosa”. Waliupata ukweli kwa kufatilia na kuudadisi au waliamua kukubali (shingo upande) kurithishwa dini na wazazi kama tu vile alivyokuwa mtoto akifyonza maziwa ya mzazi (mama) basi naye akafyonza kila kitu mpaka dini ya mzazi (mama) pia!!? Ni kweli usiopingika kuwa, ukweli siku zote ndio utakaokuweka huru lakini ukweli huo lazima uwe unaokubalika na wengi, hata kama kwa wakati mwengine uko nje ya mipaka ya dini au jamii. Hi ndio sehemu ngumu zaidi kama asemavyo Galileo, “Ukweli wote huwa ni rahisi kuuelewa pale utapogundulika, tatizo ni hapo katika kuugundua”. Inawezekana hawa waliosilimu waliweza kumpata Mungu baada ya kuufata ushauri wa Biblia, “Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.” [Yeremia 29:13], katika hii sehemu ya mwisho ya mstari yaani “mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote”, ni kumaanisha kutafuta dini ya kweli kwa utulivu, umakini, juhudi na ari ukiondoa upendeleo . . . kama vile kusoma Qur’an aya baada ya aya, na kusoma vitabu vilivyoandikwa na wanazuoni waheshimiwa Wakiislam….Lakini kwa bahati mbaya hitajio la ukweli ni dogo kuliko usambazaji wake.Lazima utashangaa, sasa vipi mtu anaweza kuwa huru katika kuujua na kuufata ukweli? Wale ambao wanaamua kwa furaha na majigambo kukana kufanya uchunguzi wa ukweli wa Uislam, inabidi angalau wayafikirie maneno ya Joanne Kathleen Rowling, mwandishi wa Kiengereza na mtunzi wa Harry Potter, “Kutofautiana na kutelekezwa kwa dharau huwa inaleta madhara makubwa kuliko hata kutopenda (chuki) kabisa”. Labda hawa waliosilimu walikuwa na aina ya uhuru iliyozungumziwa na C. Wright Mills wakati aliposema, “Uhuru sio kabisa ile nafasi ya kuchagua kile utakacho, wala pia sio ile nafasi ya kuchagua baina ya pande mbili bali uhuru ni kwanza kabisa ni ile nafasi ya kujitengenezea machaguo, kuyajadili na halafu ndio uchague.

Wakati tukisema watu wanazidi kuupokea Uislam siku hadi siku huwa tunamaanisha na kuongelea wasomi wa Ukristo, matajiri, watu maarufu, watu wenye nguvu, wasomi wakubwa, masista wa kanisani, wachungaji, wenye kushawishi watu kuingia Ukristo (evangelicals), marabi, na wale wachaji Mungu katika dini tofauti tofauti bila kuwasahau wale wasio na uwezo katika jamii.* Kuongezea nguvu yaliyosemwa hapo juu, tafiti Fulani ya waliobadili dini kuingia katika Uislam kama ilivyoripotiwa na gazeti la The Sunday Times la 22 Februari 2004 inaonesha wamiliki ardhi wakubwa wa uengereza, watu mashuhuri na watoto wa wakubwa wameupokea Uislam baada ya kuvunjwa moyo na maadili ya kimagharibi.[1] Kiufupi, watu kutoka nyanja zote za maisha, huwa wanaamua kuukubali Uislam bila jitihada kubwa wala shughuli kubwa za kimishenari.

Kiuhalisia, ni Waislam wachache mno wanaoweza kuuacha Uislam kwa ajili ya Ukristo au dini nyengine. Wengi wa hawa waasi wa Uislam, huwa ni ama wazaliwa katika Uislamu lakini wasioijua dini ya Kiislam (wajinga) na hawajajifunza; wafuasi wa madhehebu potofu ya Kiislam; waliotawaliwa na kushawishika na vitu vya kidunia; wasio na mazingira ya kuusoma Uislam; masikini ambao hawana jinsi ila kuvutika kupitia msaada wa msamaria wa Kikristo; wale ambao “…Mwenyezi Mungu ameziziba nyoyo zao na masikio yao na macho yao. Na hao ndio walio ghafilika.” [Q 16:108] na wale wanarubuniwa kiakili. Kwa kulinganisha, wasio Waislam ndio wengi wanaoingia katika Uislam kuliko hao Waislam ambao ni nadra kuwaona wakiaacha dini yao na kuingia nyengine. Cha kushangaza sasa, huwezi kusikia mcha Mungu, mfuasi, sunni wa Kiislam aliyeshiba maarifa ya Uislam akiiacha dini yake eti kwa ajili ya dini nyengine. Ukijumuisha fedha zote walizo nazo, njia na uwezo wa kisasa, na zenye mipangilio mizuri watumiazo katika shughuli na jitihada zao za kimishenari, bado Ukristo hauwezi kuwaopoa Waislam katika dini yao kama vile Waislam wanavyowakomba Wakristo. Sanjari na hilo Peter Kreeft, mtetezi wa Kikatoliki, profesa wa falsafa katika chuo cha Boston na The King’s College, mtunzi wa vitabu zaidi ya 45, msomi na mzungumzaji anayehitajika katika makongamano mbalimbali, na pia ni mjumbe wa bodi ya ushauri wa Kituo cha Watoa Elimu cha Kikatoliki (Catholic Educator’s Resource Center) anasema: “Uislam una kiwango kidogo cha kupoteza waumini wake na kiwango kikubwa sana cha kuingiza waumini”.[2] Hilaire Belloc (1870-1953) ni Mkatoliki, mwanahistoria mzawa wa Ufaransa, na mmoja kati waandishi wenye vitabu vingi Uingereza alikumbana na kimbembe cha ugumu wa kuwatoa Waislam kutoka katika dini yao, hiyo ikiwa ni mnamo mwaka 1938:

Uislam ni dhahiri haubadilikiki. Jitihada za kimeshenari zilizofanywa na Wakatoliki ambazo zimekuwa na dhima ya kuwahamisha wafuasi wa Muhammad kwenda katika Ukristo kwa miaka takriban 400 kwa hakika zimefeli. Tumeweza kumuondoa kiongozi wa Kiislam baadhi ya sehemu na hivyo kuwarudisha watu wetu waliokuwa wametawaliwa na viongozi kama hao wa Kiislam, lakini tumeshindwa kuwavuta wale Waislam* wenyewe mmoja baada ya mwengine….”[3]

 

 REJEA


* Ingekuwa haturithi dini kutoka kwa wazazi wetu, ipi unafikiri ingekuwa dini yetu ya kufata? Bila shaka tungeifata ile dini inayokubaliana na sheria za kuzaliwa za Mungu kwa binadamu. Sasa kama umerithi kutoka kwa wazazi ubudha na ukaamua kuingia katika Uislamu basi utakuwa umerudi katika dini yako ya asili. Kutoka katika vyanzo vya Kiislamu, kila binaadamu huwa anazaliwa Muislam, na ndio maana tumetumia neno kurudi katika Uislamu. Mtume alisema, “Hakuna mtoto aliyezaliwa ila alikuwa Muislamu kisha ni wazazi wake ndio wanaomfanya awe myahudi, mnaswara au mshirikina.”[Muslim, Bk. 33, No. 6426]. Ali Mazrui, mwanasayansi mashuhuri wa siasa anaandika,”…Marekani kwa mara ya kwanza wamechagua mtoto wa Muislamu kuwa Rais. Hivyo ndivyo alivyokuwa baba yake japokuwa alikuwa mlevi. Hii inamaanisha Obama alizaliwa kama Muislamu japo baadae akalelewa Kikristo…” Tazama Mazrui, Ali. “Obama has chance to mend US-Muslim relations.” City Press 13 Dec. 2008.

*  Ikumbukwe kuwa wengi kati ya wafuasi Muhammad walikuwa ni wale watu wa chini katika jamii mathalan watumwa, mafukara, wanaokanyagwa na wengineo. Na mfano huu umezungumziwa na Heraclius katika kuujua ukweli wa dini. Hivi ndivyo Heraclius alivyodadisi: “Nilipokuuliza ‘Je wengi wanaomfuata huyo Mtume Muhammad ni maskini au matajiri?’ Ukajibu kuwa ni masikini ndio wanaomfuata. Ama kweli, wafuasi wa Mitume wa kweli walikuwa ni masikini.” [Angalia, Bukhari Vol.4, Book 52, Hadith Number 191.]

[1]. Hellen, Nicholas and Christopher Morgan. “Islamic Britain lures top people.” The Sunday Times 22 Feb. 2004. Also see: Whittell, Giles. “Allah Came Knocking At My Heart.” The Times  7 Jan.  2002.

[2]. Kreeft, Peter. “Comparing Christianity & Islam.” National Catholic Register May 1987.

* Uislam ndio dini pekee yenye lisilotokana na mtu au kabila. Uislam una maana ya kunyenyekea kwa Allah tofuati na ukrtsto ulioitwa baada ya Yesu kristo, Budha baada ya Gotama Buddha, Ukonfyushasi baada ya kumfata mwanafalsafa wa kichina Confucius, Umaksi baada ya kuwa wafuasi wa Karl Marx. Na hata dini kama Uyahudi na hindu ni baada ya ya makabila ya uyahudi na uhindi.

[3]. Belloc, Hilaire. The Great Heresies. New York: Sheed & Ward, 1938.

p. 98.

 
Leave a comment

Posted by on November 12, 2012 in Dini Inayokuwa kwa Kasi

 

Tags: , , ,

Hawa Ima ni Waerevu au Wajinga

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Sasa na tuangalie kwanini hawa watu wengi kama tutavyowaona wanakana imani zao na kuamua kuupokea Uislam, japokuwa wanakutana na vita ya kuzingatia dini hii kali na matokeo magumu kwao. Je! Hawa waliosilimu hawakuona kama sheria za Kiislam zinazotakiwa kuja kutawala dunia kuwa  ni za kibaguzi, za kinyama, na za kikatili?! Hawaoni kama ni dini ngumu na kali sana isiyoendana na dunia ya sasa?! Mtu yampasa aamke kabla ya alfajiri kuswali moja ya swala tano za kila siku. Kufunga mwezi mzima kila mwaka! Kusafiri kwenda Saudi Arabia kwa ajili ya Hijja japo mara moja katika maisha yako. Kinachoonekana kushangaza ni kuwa mtu anaehijji yampasa amrushie mawe shetani! Mwanamke anatakiwa kujifunika kuanzia kichwani mpaka kwenye vidole vya miguu, bila kuzingatia miguu yake mizuri na hali ya hewa ya joto. Na wewe kama ni mwanamke wa Kiislam, inakuwaje mmeo anao uwezo wa kukuletea mke mwengine. Uislam unampa haki isiyo ya kawaida ya kuoa mpaka wake wanne. Utahofishwa zaidi pale utapogundua Uislam umempa haki mme kumwadhibu mkewe kwa viboko kama akiwa hatii [Q 4:34]. Mtu atauliza, “Hivi hawa wanawake wanaoingia katika Uislam hawahofii kufanywa kama wafu kwa kuvalishwa maguo kutoka juu mpaka chini na  bado huyu mwanamke hahofii pale mme wake mwenye wake wengi anapompa ujauzito wa watoto sita kwa wakati mmoja (sextuplets)?!

Kuwa Muislam yapasa utoe zakaat kutoka katika kiasi chako cha fedha ulichokipata kwa tabu na mashaka. Yaani asilimia mbili na nusu (2.5%) ya mahifadhi yako ya mwaka yanaenda kwa maskini! Halafu usijaribu kuiba; mkono wako wataukata[Q 5:38]. Tumeshambuliwa na matangazo ya pombe halafu Qur’an inatuambia kuwa pombe ni kazi ya shetani[Q 5:90], na hivyo yapasa kujiepusha nayo, kwa yote haya ataishi vipi huyu?! Na kabla ya moyo kutulia kutokana na mshtuko ulioupata, bado unaambiwa sandwich  (hambaga) uipendayo zaidi yenye nyama ya nguruwe katikati ni haramu katika Uislam! Na isitoshe, hairuhusiwi kusilikiza miziki au kutazama MTV! Linachosha zaidi basi dini yenyewe imeongozwa na Muhammad “…Mtume, Nabii Ummy (asiyejua kusoma wala kuandika…)” [Q 7:157] Hivi wataweza kumuiga Muhammad, mfano wao wa kuigwa kwa kusugua meno yao kwa kutumia mti (miswak)! Vipi basi hawa wastaarabu, wavumilivu na wapenda amani wamfate Mtume huyu ambaye alisema “…Nimefanywa mshindi kwa (maadui zangu kupewa) uwoga [yaani Mwenyezi Mungu amefanya maadui wa Uislamu wamuogope Mtume hata kabla ya mapambano]….”[1] mtu huyo huyo aliyeshinda anawajaza roho ya Jihad wafuasi wake wakikumbana na maadui wa Uislam tangia Allah alivyomuamrisha “Ewe Mtume (wa Mwenyezi Mungu)! Wahimize walioamini (Waislamu) wende vitani.” [Q 8:65]. Hivi hawaoni kuwa Muhammad kaamsha hofu zaidi, chuki na dharau kubwa kwa Wakristo ulimwenguni kuliko mtu yeyote aliyewahi kutokea?!”[2]

Inakuwaje hawa wanaosilimu wanakubali kumuabudu Mungu wa Waislam aliyesema, “…Nitatia woga katika nyoyo za makafiri….”[Q 8:12] Na kama hiyo haitishi angalia Mungu huyo huyo anawaamrisha Waislam katika mapambano “…Basi  wapigeni (kwa panga) juu ya shingo (zao) na kateni kila ncha za vidole vyao.”[Q 8:12] Inakuwaje uonevu wote huo? “Hayo ni kwa sababu wamemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake.”[Q 8:13] asema Mungu wa Waislamu. Na isisahaulike kuwa dunia kiUislam imegawanyika katika “nyumba ya Uislam (Dar al-islam)” na “nyumba ya vita(Dar al-harb)”. Mgawanyo huo utamstaajabisha mtu: Kwani Uislam ni dini ya uvamizi na kukamata nchi nyengine kwa nguvu? Kufanya vitu viwe vibaya zaidi, wale woote waliosilimu wanatakiwa waelewe kuwa wale ndugu, jamaa na marafiki waliowaacha walipotoka wao sio zaidi ya kuwa ni makafiri tu.*

Ukiwa Muislam unapewa jina jipya: Gaidi! Kubadilika kuwa Muislam kunamaanisha kutia hasira na kuondoa utulivu kwa familia, marafiki, jamii, serikali na hata mashirika ya kimataifa!  Wakati mwengine, kuacha sifa na heshima yako, na hata uwezekano wa kuachishwa kazi yako pia! Kwanini waume kwa wanawake hawa waendelee kuikumbatia dini ambayo inaambatanishwa na serikali za kidekteta, ugaidi, unyanyasaji wa kijinsia, video za kukata watu vichwa, na imani yao ya kusambaza dini kwa upanga?! Na cha kushangaza zaidi, sheria yao imetoa kibali cha kuuliwa kwa yeyote aliyeasi (aliyeritadi) kisa tu Muhammad kasema: “Kama Muislam ataiacha dini yake, muueni.”[3] Lakini bado waume kwa wake wamekuwa wakiipokea dini hii. Wale tu waliozidi ujinga au waliozidi uwerevu ndio wangechukua uamuzi huo.*Lakini nani afahamuye, yawezekana uamuzi wao umekuwa rahisi sasa kwa kuwa utashi wao wa kumridhisha Mungu umezidi ule wa kuiridhisha dunia.

REJEA


[1].  Bukhari Vol. 4, Bk. 52, No. 220.

[2]. Hofmann, Murad Wilfried. Religion on The Rise: Islam in the Third Millennium. Maryland: Amana Publications, 2001.p. 54

* Kafir inamaana ya yule anayepinga. Kwa maana ya Kiislamu, Kafir ni mtu anyepinga ukweli wa Uislamu (kwa kizungu Non-muslim). Kiufupi, Kafir ni mpingaji. Hujawahi kupinga kuisoma Qur’an, kusoma vitabu vya Kiislamu au kusikiliza mafundisho ya Uislamu. Je huo sio upingaji? Na kama umepinga kuisoma qur’an kwanini ulalamike endapo Muislamu akikuita ni Kafir? Baada ya kuisoma hiyo Qur’an kuna mambo unaweza kuyapinga, je huo sio upingaji tena? Ni jambo sahihi kabisa kumuita Muislamu hivyo hivyo iwapo atayempinga Yesu Kristo ambaye katajwa katika vitabu vya Mungu  kama Qur’an na Injili. Kwanini imani zengine zinahisi kukashifiwa kama wakiitwa makafiri na Waislamu kwa kupinga kumkubali Muhammad! Je ikatokea wasio Wakristo wakaitwa makafiri na mungu wa Biblia, je Wakristo watamuhoji mungu wao kwa hilo?! Mungu ndio kashawaita wasio Waislamu kuwa ni makafiri na jambo la msingi hapa ni kujiuliza kama kweli hii Qur’an ni neno la Mungu! Kama ni neno la Mungu basi , “Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unafanya nini? Au kazi yako, Hana mikono? ” [Isaya 45:9]. Cha kushangaza Qur’an inakazia mkazo kauli hiyo kuwa siku ya kiyama, na wasio Waislamu watakubali na kujiita wenyewe ni makafiri. Aya inasema: “Enyi makundi ya majini na watu! Je, hawakukujieni Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakikubainishieni Aya zangu, na wakikuonyeni mkutano wa Siku yenu hii. Nao watasema: Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu. Na yaliwadanganya maisha ya dunia. Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri.” [Q 06:130; pia tazama Q 7:37] Mtume wa karne ya nane; Amosi anawaita wale wanaokataa sheria za Mungu kuwa ni ‘ngo’mbe’ [Amosi 4:1] na Mtume Yeremia anawaita watu hao ‘waovu’ (scoundrels) [Yeremia 5:26], Yesu anawaita waovu hao kuwa ni ‘wazao wa nyoka’ [Mathayo 12:34] na katika mahala kwengine aliwaita ‘kizazi kibaya na cha zinaa’ [Mathayo 16:4] Waislamu wa sasa kwa huruma zao kwa hawa waovu wanaokataa sheria za Mungu, hawawaiti ‘ng’ombe’, ‘wazao wa nyoka’, wala ‘kizazi kibaya na cha zinaa’ bali wamebaki kuwaita makafiri tu yaani wapingaji.

[3]. Bukhari, Vol. 4, Bk. 52, No. 260. Pia angalia, Bukhari Vol. 9, Bk. 83, No. 17. Na pia kutokana na hiyo hiyo Bukhari Vol. 9, Bk. 89, No. 271, kulikuwa na mtu ambaye alisilimu na baadae kurudi katika Uyahudi. Mu’adh bin Jabal, swahaba wa Mtume ambaye alipata kumuona mtu huyo na Abuu Musa, swahaba mwengine wa Mtume. Mu’adh akauliza ana nini huyu mtu? Abu Musa akamjibu,”Alisilimu kasha akarejea katika uyahudi.” Mu’adh akasema, “Sitakaa chini mpaka uwe ushamuua huyu mtu kama alivyosema Allah na mjumbe wake”.

* Kuna kueleweka ndivyo sivyo kwingi dhidi Uislamu. Hata hivyo kwa wale wanaonesha dira ya kutaka kuujua ukweli basi wanashauriwa walau wakisome kitabu cha Dkt. Zakir Naik, Answers to Non-Muslim common Questions About Islam (Majibu kwa Maswali Yaliyozoeleka  kwa Wasio Waislamu Kuuhusu Uislamu). Dkt. Zakir Naik ni mhubiri fasaha wa kimataifa wa Kiislamu. Ni mwanzilishi na rais wa Islamic Research Foundation (IRF). Kwa egemeo la maandiko (Qur’an , Biblia n.k) na utumizi wa akili ya kawaida, mantiki na sababu za kisayaynsi, Dkt. Zakir amefanikiwa kufuta uelewa huo mbovu wa Uislamu. Katika kitabu hicho, utaona majibu yanayoridhisha katika maswali kama kwanini Waislamu wana mume wanaruhusa ya kuoa zaidi ya mke mmoja? Kwanini Uislamu unawashusha thamani wanawake kwa kuwavalisha hijab? Kwanini Waislamu wengi ni magaidi? Kwanini pombe ikatazwe katika Uislamu? Na kwanini Waislamu wawakashifu wasio Waislamu kwa kuwaita makafiri? N.k unaweza kupata kitabu hiko bure kutoka mtandaoni : <http://www.islambasics.com/view.php?authID=154&gt;; Also see <http://www.ilovezakirnaik.com/misconceptions/index.htm&gt;

 
1 Comment

Posted by on November 12, 2012 in Dini Inayokuwa kwa Kasi

 

Tags: , , , ,

Akili Yenye Kufikiri Kwa Kasi

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Akili yenye kufikiri huwa inashtushwa na taarifa kama “Waislamu ndio kundi linalokuwa kwa kasi zaidi duniani….”[1] ambayo ilichapishwa na gazeti lililoenea na kusomwa na wengi Marekani, USA Today. Akili yenye kufikiri itashuhudia Hillary Rodham Clinton akisema, “Uislam ndio dini inayoenea kwa kasi zaidi Marekani, ni mwongozo na nguzo ya uimara kwa wengi wa watu wetu….”[2] na kushughulishwa. Na baada ya kusikia kutoka katika Shirikisho la Habari la Uingereza (BBC) ambapo Mike Wooldridge akiripoti kuwa, “Uislam ndio imani inayokuwa kwa kasi zaidi….”[3], bila shaka kwa mtu mwerevu na mwenye kutumia akili yake ipasavyo atajenga wazo akilini mwake kuwa “Huenda dini hii ikawa ndio dini ya kweli”. Kisha akisoma The Junior Encyclopedia of Canada ilotanabaisha: “Uislam ndio imani inayokua kwa kasi zaidi ulimwenguni”[4] atatafakari, akitumia akili zake vizuri na kulazimika kuweka chuki zake kando na kuutazama ukweli, hata kudiriki kuuona Uislam kuwa ndio badiliko la msingi, muhimu na la kweli. “…Sheria ya Muhammad imekutana na mapokezi yasiyofanana nayo kabisa hapa duniani….”[5] hii iliandikwa na George Sale, mmoja kati ya wa mwanzo kuitafsiri Qur’an kwa lugha ya Kiengereza, aliyejitunuku shahada ya mpingaji mkubwa wa Muhammad na mchukiaji wa dini ya Kiislam. Kuongezea hilo, “Hakuna dini nyengine ieneayo kwa kasi zaidi kuliko Uislam”[6] iliyoandikwa na James Michener, mwandishi mashuhuri na mshindi wa zawadi ya waandishi bora wa Pulitzer. Mtu mwenye chuki na dharau ya hali ya juu anaweza kusikia sauti ndogo kichwani mwake ikinong’ona, “ Wewe! Ni bora ukubali walau mara moja tu kuwa kuna jambo kubwa katika Uislam.” Na pale jarida la The Economist wanapoitanabaisha dunia kuwa “Wengi kati ya wasomi wa Kikristo wanakubali kuwa Uislam utaupita Ukristo kama dini yenye wafuasi wengi na inayoenea kwa kasi kabla ya mwaka 2050.”[7] inabidi watu waendelee kuwa wakimya wakipea mazingatio na kutafakari usukani.

Kama hiyo haitoshi, kipande cha habari kilichotolewa kutoka katika jarida la National Geography la mwezi wa kwanza (January) 2002 lilielezea kuwa “Khumusi (moja ya tano) ya wannadam sasa wanafata Uislam, dini inayokuwa kwa kasi zaidi japokuwa ndio dini inayoeleweka vibaya kuliko zote duniani.”[8]

Tarehe 17 Julai 1997, mkurugenzi wa Christian Futures Network, John Gary baada ya kupokea zawadi yake katika World Future Society (tamasha linalojadili jamii za kesho za kidunia), alisikika akiongelea “Matukio kumi ya dunia yahusuyo dini” na katika tukio la tatu alitamka “Miongoni mwa dini za hapa ulimwenguni, Uislam unashika nafasi ya juu kwa ukuaji wa kasi….katika takwimu za kipindi cha baadae, haitashangaza kuona Uislam ukiupiku Ukristo kwa kuwa na idada ya wafuasi wengi zaidi.”[9] Hiyo ni tabiri moja, lakini kwa akili isiyo na upendeleo wowote utauona Uislam kupitia lenzi yenye kuheshimika baada ya kusoma tabiri nyengine ya msomi mashuhuri Samuel Huntington akitabiri kuwa:

“Asilimia ya Wakristo duniani…utafikia takriban asilimia 25 ya watu wote duniani kabla ya mwaka 2025….Japokuwa Waislam wataendelea kuongezeka kwa kasi ya ajabu, kufikia asilimia 20 ya watu kabla mwanzo mwa karne ya 21 kufunika idadi ya Wakristo miaka kadhaa baadae na hata uwezekano wa kufiksha asilimia 30 ya watu kabla ya mwaka 2025.”[10]

Wakati Kitabu cha Maarifa cha Guinness (Guinness Book of Knowledge) kilikiri kuwa Uislam ndio dini inayokuwa na kuenea kwa kasi zaidi duniani[11], kwa yeyote muungwana, mpenda ukweli na mwenye fikra za haraka atakubali kuwa Uislam utakuja kutawala mambo yote ya kilimwengu. Lakini  mwishoni,  Guinness World Records 2003 , kitabu chenye mamlaka na chenye mauzo mengi kinachoangazia ukweli wa kushangaza na mafanikio yasiolingana ya kibinaadam, kinasema, “Katika kipindi cha 1990 mpaka 2000, takriban watu wapatao milioni 12 na unusu walibadili dini kuuelekea Uislam kuliko Ukristo”, kwa akili yenye udadisi mkubwa itahitaji maelezo na kutokana na hilo hii ni ambalo Guinness World Records 2003 ilirikodi:

Uislam ndio dini ieneayo kwa kasi zaidi, Mnamo mwaka 1990, watu milioni 935 walikuwa Waislam na idadi hii ikaongezeka hadi kufikia bilioni moja na laki mbili mwaka 2000, ikimaanisha mmoja kati ya watano duniani tayari ni Waislam. Ingawa dini hii ilianzia(tukiongelea kipindi cha Muhammad) Uarabuni, mpaka mwaka 2002, asilimia 80 ya waumini wake wako nje ya uarabuni. Katika kipindi cha 1990-2000, takriban watu milioni 12 na nusu wameingia katika Uislam zaidi kuliko wale walioingia katika Ukristo.[12]

Hermann Eilts (aliyezaliwa mwaka 1922) aliyekuwa balozi wa Marekani Saudia Arabia  na Misri ambaye baadae akajiunga na Chuo Kikuu cha Boston kama Profesa wa Masuala ya Kimataifa (International Relations), na hapo kuwa mkuu wa kitengo cha Sayansi ya Siasa (Political Science) na baadae kuwa mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kimataifa alikuwa na haya ya kusema:

“Waislam duniani sasa wamekaribia billion moja*,hiyo ni takwimu ya kuvutia. Lakini kwangu mie linalovutia na kushangaza zaidi ni Uislam kuwa dini ikuayo kwa kasi zaidi katika dini zinazoabudu Mungu mmoja. Hili ni jambo lazima tulitilie mkazo. Kutakuwa na  jambo la kweli kuhusu Uislam kwani watu wengi wamekuwa wakivutika.[13]

REJEA


[1]. Kenny, Timothy. “Elsewhere in the World.” USA Today Final Edition 17 Feb. 1989: p.4A.

* Baada ya kumdadisi Abu Sufyan kuhusu wafuasi wa Muhammad, Heraclius alitoa maoni hayo. [Angalia Bukhari Vol.4, Bk. 52, No. 191.]

[2]. Stammer, Larry B. (Times Religion Writer). “First Lady Breaks Ground With Muslims.” Los Angeles Times Home Edition, Metro Section, Part B, 31 May 1996: p.3.

[3]. Wooldridge, Mike. “Islam: Faith under fire.” news.bbc.co.uk 14 Sept. 2001. 11:17 GMT 12:17 UK. <http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/americas/1544071.stm&gt;

[4]. The Junior Encyclopedia of Canada. Hurting Publishers, 1990. Vol. 2, p.396.

[5]. Sale, George. Preface. The Koran. London: C. Ackers, 1734. A2.

[6]. Michener, James A. “Islam: The Misunderstood Religion.” Reader’s Digest American Edition. May 1955: p. 73.

[7].  “The Bible v the Koran, the battle of books.” The Economist 22 Dec. 2007: p.62.

[8]. Belt, Don. “The World of Islam.” National Geographic Jan. 2002.

[9]. Gary, John.  “Ten Global Trends in Religion.” wnrf.org < http://www.wnrf.org/cms/tentrends.shtml&gt; 17 July 1997.

[10]. Huntington, Samuel P. The Clash of Civilizations and the Remaking of World Order. New York: Simon & Schuster, 1996. pp. 65-66.

[11]. Guinness Book of Knowledge. p.195. [Kwa ushahidi zaidi kuonesha Uislamu ni dini inayokua kwa kasi soma: Baum, Geraldine. “For Love of Allah.” Newsday Nassau and Suffolk Edition, Part II, 7 March 1989: p.4 ; Goldman, Ari L. “Mainstream Islam Rapidly Embraced by Black Americans.” New York Times Late City Final Edition, 21 Feb. 1989: p.1; Kopel, Ted. Nightline ABC. April. 1998; Young, Gayle. “Fast-growing Islam winning converts in Western world.” cnn.com 14 April 1997 <http://edition.cnn.com/WORLD/9704/14/egypt.islam/&gt; ; Blank, Jonah. “Islam is growing fast in America, and its members defy stereotypes.” US News 12 July 1998. <http://www.usnews.com/usnews/news/articles/980720/archive_004363.htm&gt;; Seitz, Barr. “Fastest-Growing Religion Often Misunderstood.” BICNews. ABC. 13 Dec. 1997; Robinson, B.A. “University Dispute re: Islamic Book.” religioustolerance.org <http: //www.religioustolerance.org/isl_unc.htm.> 17 Aug. 2002 ; Ali, M.M. “Muslims in America: The Nation’s Fastest Growing Religion.” Washington Report on Middle East Affairs May/June 1996. pp. 13, 107.]

[12]. Guinness World Records 2003. p. 102. Pia katika Guinness World Records 2004 p.90. Katika ukurasa wake kuelezea haki za kunakili, kuna onyo madhubuti lililosema: “Kujaribu kuvunja rikodi au kuweka rikodi katika jambo Fulani ni hatari sana. Umakini na uangalifu wa hali ya juu unahitajika katika kuliendea hilo na kama lolote likikutokea basi dhima itakuwa ni yako mwenyewe. Kwa njia yeyote ile, kampuni ya Guineess World Records haitahusika na kifo au madhara yoyote yatakayojitokeza kutokana na kujaribu kuweka rikodi duniani.” Hapo ndipo mtu atapopigwa na butwaa  na kujiuliza hivi hizi dini nyengine zinajua yatakayo yakuta kwa kujaribu kuipiku rikodi ya Uislamu ya kuwa dini inayokuwa kwa kasi zaidi duniani.

[13]* Hiyo ilikuwa Juni 24, 1985, kwa sasa Waislamu wanafikia bilioni moja na nusu, angalia, “The Bible v the Koran, the battle of books.” The Economist 22 Dec. 2007.p.62. Pia tazama katika, “Major Religions of the World Ranked by Number of Adherents.” adherents.com <http://www.adherents.com/Religions_By_Adherents.html&gt; last retrieved 2 June 2009. ; na kutokana na jarida la Time, “Moja ya sababu ya kukua kwa uchumi halal ni hii idadi ya vijana bilioni 1.6 ambao sehemu zengine ni matajiri kuliko.” Tazama Power, Carla. “Halal: Buying Muslim.” Time 25 May 2009. p.38. Sanjari na hilo, Taasisi ya Pew Forum on Religion & Public Life ilifanya utafiti mkubwa mwaka 2009 na kukuta Waislamu duniani wakifikia bilioni 1.57. Tazama,  Pew Forum on Religion & Public Life.  “Mapping the Global Muslim Population: A Report on the Size and Distribution of the World’s Muslim Population.” 8 Oct. 2009; Beaumont, Peter. “One in four people is Muslim, says study.” Guardian 8 Oct. 2009.

* Katika hotuba kwa kamati ya mambo ya nje katika bunge la Marekani Juni 24, 1985

 
2 Comments

Posted by on November 11, 2012 in Dini Inayokuwa kwa Kasi

 

Tags: , , ,