RSS

Tag Archives: Uingereza

Sarah Joseph

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Huyu anatokea katika familia ya Kikatoki ya Uingereza ambayo mizizi yake inatokana na uvamizi wa Norman (Norman Conquest). Mama yake alianzishaa uwakala wa kwanza wa mitindo Uingereza na Joseph anadai kuzunguukwa na watu wazuri zaidi hapo katika ofisi za mitindo mtaani kwao.

Mtoto huyu Mkatoliki babake akiwa mhasibu na mamake aliyekuwa mwanamitindo anakumbuka alivyokuwa na umri wa miaka 14 akimkimbilia Naomi Campbell akiwa na kadi ya biashara ya mama yake. Na katika kipindi kifupi baadae, kaka yake akawa Muislamu. Akijilazimisha kupingana na chuki zake kwa Waislamu, Sarah akaanza kusoma dini. “Taratibu, Uislamu uliendelea kunijibu maswali yangu ambayo yalinitatiza mpaka pale nilipoutaka Uislamu wenyewe,” anasema. Na alivyotimu miaka 17, Sarah alibadili dini kuwa muislam, akiukana Ukatoliki aliolelewa nao. Akaamua kuwa mvaaji hijab, vazi lililompa ukombozi na taadhima. “Nataka nihukumiwe kwa kile ninachosema, na sio kwa vile ninavyoonekana,” alishawahi kusema hivi.

Katika mahojiano na Gabrielle Procter, Sarah Joseph alisema:

“…Kuwa Muislamu kunakupa haiba nzuri lakini kubwa zaidi sasa ni binaadamu kikwelikweli. Nimeishi miaka 16 nikiwa sio muislam, sasa hivi mimi kama mwanadamu, mwanamke, mama, mhariri, na mwenyeji wa London- vyote hivi vinanisaidia. Lakini jukumu langu kama mama linanyooshwa na kuwa Muislamu; kazi yangu kama mhariri, na ufahamu wangu kama mmoja wa wanajamii vyote vinanyooshwa na falsafa yangu hii mpya… mimi ni mtu wa imani na naamini mtu wa imani yapasa awe na matumaini. Nawaona vijana wengi wanaojumuika katika jamii mbali mbali za kiengereza wakiwa waerevu, fasaha, wenye msukumo wa kuleta tija katika jamii yao na wakiwa sehemu ya jamii ya kiislamu. Nadhani Waislamu wana uwezo wa kuchangia pakubwa katika jamii. Na kama watu ikatokea wauone uislam ni sehemu ya utatuzi badala ya kuuona ni sehemu ya tatizo, wataishi kwa raha mustarehe.”

Sarah amepata shahada yake ya kwanza katika masomo ya dini kutoka Chuo Cha King cha London. Alifanya utafiti kuhusu Waingereza Wanaosilimu akisomea shahada yake ya pili. Pamoja na hilo, amekuwa mshindi wa 1999-2000 wa shani ya kusomeshwa bure kutoka katika mfuko wa King Faisal Foundation/ Prince of Wales Chevening. Ni mhariri wa jarida la Emel (jarida la kiislamu linalosomwa zaidi Uingereza- jina lake linasomeka M na L likisimama badala ya Muslim Life (Maisha ya Muislam), likimaanisha ‘tumaini’ kwa lugha ya Kiarabu). Pia ni mtangazaji wa British Muslims, na ni mwandishi. Sasa, akisomea shahada nyengine amekuwa akifanya kazi kwa muda kama mwalimu wa chuo ambaye amekuwa akifanya mihadhara mingi na sehemu  nyingi inayohusiana na masuala ya dini na wanawake. Mwaka 2004, alitunukiwa OBE (Tuzo ya Uingereza inayosimama badala ya Order of the British Empire), kwa mchango wake katika midahalo ya dini. Sarah kashajumuika katika vipindi vingi vya televisheni za Uingereza vikiwemo –Panorama na Johnathan Dimbleby. Pamoja na kufanya kazi kama mtafiti mzoefu katika kitengo cha kujifunza cha BBC 2001 Islam Series. Pia amekuwa mhariri mkuu wa kwanza mwanamke wa gazeti kubwa la Waislamu: Trends. Sara Joseph ni mhariri muanzilishi wa baraza la Waislamu la Uingereza The Common Good Consultant on Islamic Affairs– likishughulika na utafiti na mafunzo kwa wale wanaoihitaji kuajiriwa, kusoma, kuwa na afya bora, polisi n.k. katika misingi ya Kiislamu.

Ameolewa na Mahmud ar-Rashid,  mwanaharakati wa haki za binadam. Miongoni mwa vyama vya vijana na jamii ambavyo ar-Rashid anaongoza ni: the Muslim Council of Britain (MCB), baraza kuu la kutetea Waislamu Uingereza na ni pia mwenyekiti Islamic Society of Britain. Wana watoto watatu tayari: Hasan, Sumayyah na Amirah.

Akiongelea kuhusu makundi ya watu wanaoingia katika Uislamu kila kukicha, hususan kwa kutumia makadirio ya watu 10,000 mpaka 50,000 wanaoingia katika Uislamu kila mwaka Uingereza, Sarah anadhani kufikia mwaka 2020, Uislamu itakuwa ndio dini inayofatwa zaidi Uingereza, “Sisi ni wa pili kwa kuwa na idadi ya wafuasi wengi Uingereza ila ifikapo 2020 tutakuwa tunaongoza rasmi kwa kuwa na waumini wengi wahudhuriaji ibada zao kama ukitumia uhudhuriaji wa kanisa na msikiti kama kigezo,” Alisema hayo kuiambia GDN.

Njia ya Mawasiliano:

Anuani: Studio 8,

The Whitechapel Centre,

Myrdle Street,

London E1 1HL

Tovuti:

http://www.emelmagazine.com

http://www.emelmagazine.co.uk

Barua pepe: info@emelmagazine.com

REJEA

[Wavell, Stuart. “Putting a good glossy on the Muslim lifestyle.” The Sunday Times 9 Oct. 2005; Joseph, Sarah. “Interview: Sarah Joseph, Emel magazine.” By David Rowan. Evening Standard 20 July. 2005; Joseph, Sarah. “The freedom that hurts us.” The Guardian 3 Feb. 2006; “Being Muslim shapes you, but first and foremost I’m a human being.” The Guardian 30 Nov.2004; “Emel’s Hope.” Saudi Aramco World. March/April 2004.]

Advertisements
 
1 Comment

Posted by on November 16, 2012 in Waliosilimu

 

Tags: , , , ,

Uislamu Unakuwa kwa Watu Kusilimu

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Ni muhimu kuelewa kuwa Uislam haukui kwa kiasi cha kuzaliana sana Waislam tu bali vile vile kwa watu kuupokea na wakaukubali. Marekani pekee, kutokana na gazeti la St. Petersburg Times, “Kila mwaka Marekani, takriban watu 20, 000 wanaingia katika Uislam, ukiachia wale wanaosilimia katika gereza…, halafu hawa wanaosilimu, wengi wao ni wanawake, na tena wengi katika hao ni vijana ambao bado hawapo katika ndoa….”[1] Shirika la habari la NBC liliripoti idadi hiyo hiyo ya wafuasi wa dini zengine wanaoingia katika Uislam mwaka hadi mwaka. Na kutokana na gazeti la New York Times, “Karibia asilimia 25 ya Waislam Wamarekani ni waliosilimu.”[2] Uingereza, gazeti la The Times liliripoti, “. . . katika idadi isiyo na kifani ya Waingereza, wengi wao wakiwa wanawake, wanaingia katika Uislam . . . .”[3] Na mwaka 2004, The Sunday Times lilisema, “…zaidi ya wazungu (waingereza) 14,000  washaingia katika Uislamu. . . .”[4] japokuwa, kutokana na utafiti wa kina uliofanywa na Kevin Brice wa Chuo Kikuu cha Swansea, inakadiriwa kuwa mwaka 2010, kulikuwa na Waingereza (wazungu) 100,000 waliosilimu Uingereza “. . . kukiwa na zaidi ya watu 5,000 wabadilikao, kila mwaka kitaifa.”[5] Utafiti huo ulifanywa na the inter-faith think-tank, iitwalo Faith Matters. Kusema kweli takwimu hizi zinatuhabarisha jambo fulani kuhusu muelekeo wa Uislam mbeleni..

Tugeukie Ulaya katika uchunguzi wetu, tutashuhudia vyanzo vya habari vikikiri Uislam utakuja kuwa dini itawalayo barani ulaya. Kutokana na The Washington Quartely:

“…Waislam watafanikiwa kujumuisha sio chini ya asilimia 20 ya wana ulaya wote ifikapo mwaka 2050. Baadhi washaanza kutabiri kuwa robo ya Ufaransa itakuwa ni Waislam ifikapo mwaka 2025 na kama mwenendo huu utaendelea, Waislam watawapiku wasio-Waislamu kwa idadi huko Ufaransa na hata Ulaya Magharibi yote ifikapo 2050.”[6]

 Patrick Buchanan ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa Marekani, mwandishi, mwanasiasa na vile vile ameshafanya kazi kama mshauri wa Rais (wa Marekani) Richard Nixon, Rais Gerald Ford, na Rais Ronald Reagan. Katika hotuba yake aliyoitoa tarehe 7 Desemba 2001, Buchanan alisema: “Msisahau kuuhesabu Uislam, kwanza ndio imani inayokuwa kwa kasi zaidi barani Ulaya na pia imeshaupiku Ukatoliki duniani. Na kama tunavyoona Ukristo unavyokufa katika mataifa ya magharibi, makanisa yanazidi kupoteza watu na misikiti lukuki kuzaliwa na kujaa.”[7] Mwaka 1999, ukaguzi wa Umoja wa Mataifa ulionesha kuwa kati ya mwaka 1989 na 1998, idadi ya Waislam barani Ulaya imekuwa kwa aslimia zaidi ya mia moja.[8] Kwa sasa, Waislam wanawakilisha karibu asilimia 10 ya watu wa Ulaya yote na tabiri zinaonesha ifikapo mwaka 2025 Waislam watakuwa washafikia asilimia hizo (kumi).[9] Cha kufurahisha sasa! Amsterdam na Rotterdam ndio majiji yanayotazamiwa kuwa wakwanza kwa idadi kubwa ya Waislam ifikapo 2015 tu.[10] Katika makala iliyobeba kichwa cha habari “Ulaya, usimamaji wa magorofa marefu yanaakisi kuinuka kwa Uislam” iliongelewa katika The Christian Science Monitor, Isabelle de Pommereau anaeleza: “Ulaya, Uislam kama dini ikuayo kwa kasi zaidi kuliko zote unajijengea nafasi yake wazi wazi sasa baada ya milongo ya kuswali na kuabudu kwa kujifichaficha kwenye uga na sehemu za nyumba zilizo chini ya ardhi (basements), na sasa unafanikiwa sio tu kabadilisha sehemu zao za kijamii bali pia mandhari ya majiji.”[11] Akijadili mwelekeo wa kubadili mienendo ya dunia, William Van Wishard anatoa taswira akisema, “Kanisa Katoliki linakumbana na uwezekano mkubwa wa kufunikwa na Uislam kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi barani ulaya kwa miaka inayokuja.”[12] Kuna sababu kubwa tatu zifanyazo bara la ulaya kuwa bara lenye Waislam wengi kuliko wafuasi wa dini nyengine, nazo ni 1) Uhamiaji 2) Kuzaliana sana kwa Waislam 3) Wanaosilimu.

Hapa tunavutika na sababu ya tatu kwa kuwa ndio sababu inayotokea kwa haraka na wepesi zaidi. Utabiri maarufu wa Bernard Lewis*unasema bara la Ulaya litakuwa la Kiislam ifikapo mwisho mwa karne hii.[13]

Mwaka 2005, The Christian Science Monitor lilisema: “Japokuwa hakuna takwimu za uhakika, ila kwa mchunguzi makini atagundua tu kuwa maelfu ya wanaume na wanawake wanasilimu mwaka hadi mwaka.[14]  Waislam waliokuwa Ulaya watawabadili wasio-Waislamu wa ulaya kuingia katika Uislam. Eidha Waislam watafanya jitihada kuzishinda roho za wasio-Waislam au watu wa bara la Ulaya watasilimu kufuatia lile shauri la “Nimeamua kubadili dini kutokana na kuvutiwa na tabia njema na nidhamu ya Waislamu” au wanaweza kusilimu ili waweze funga ndoa na Muislamu. Au uwepo wa Waislamu nchi za Magharibi, kutachokonoa wasio Waislamu waweze kujifunza yaliyo katika mila ya Uislamu na vipi waweze kuishi na Waislamu hawa wakali. Hivyo baadhi watatafuta vitabu kama  The Complete Idiot’s Guide to Understanding Islam cha Yahiya Emerick kinachoweza kumsaidia asiye Muislam kujifunza misingi ya Uislamu na kuishi nao. Vile vile, miongozo inayopatikana katika vitabu visivyowatisha kama Islam For Dummies pia vinaweza kuwasaidia wasio Waislamu kutambua misingi na masuala mengine ya Kiislamu. Wengine wanaweza kutumia vitabu vyengine vya kisomi zaidi vya Kiislamu na matokeo yake, wasio Waislamu watakuja kuuelewa Uislamu halisi, ambao ni tofauti kabisa na ule unaofundishwa kupitia vyombo vya habari na mwishowe waukubali kwa kuingia ndani yake. Hapa tunapata ile kanuni ya ‘Uwepo-wako-unavuta-fikra-zangu’. Pengine hii sababu ya tatu ndio iliyojumuishwa katika moja za hotuba za marehemu Gadhafi: “Tuna Waislam wapatao milioni 50 barani Ulaya. Kuna kila dalili zioneshazo Allah karibuni ataupatia ushindi Uislam katika bara hilo tena bila upanga, bila mtutu, na wala uvamizi. Waislam milioni 50 hao watabadilika kuwa bara la Kiislam miongo kadhaa baadae.”[15]

 Ulaya, Uislam unashika nafasi ya pili kwa kuwa na wafuasi wengi zaidi.[16] Kutokana na mazoea yetu maishani, mwanafunzi shuleni, kama kazoea kupata D anauwezo wa kupanda hadi C na halafu daraja la B. Na kama akiongeza juhudi na kujituma, bila shaka anao uwezo wa kufikia daraja la juu (A). Hivyo, katu haitashangaza kuona Uislam ukiusambaratisha Ukristo na dini zengine zote katika bara hilo la Ulaya. Kama Uislam ni dini ishikayo nafasi ya pili kwa sasa, bado ina nafasi ya kuwa dini itakayoshika nafasi ya kwanza hapo baadae. Katika mahojiano na balozi wa Sweeden nchini Uturuki; Ingmar Karlsson ambaye pia ni dokta wa kitaaluma katika masomo ya dini ya Kikristo katika Chuo Kikuu cha Lund. Pia ni dokta wa Falsafa katika Chuo Kikuu cha Vaxjo na ni mtunzi wa vitabu zaidi ya 10 ameuelezea Uislam kama dini ya nyumbani Ulaya. Alisema katika mahojiano yake hayo: “Wakati nilipokuwa nakua kule Sweeden baada ya vita kuu ya pili ya dunia, kulikuwa na Waislam watatu tu nchini mwetu, watatu huwezi amini!… Sasa hivi Waislam wanawakilisha asillimia 5 mpaka 6 ya wananchi wa Sweeden wote. Na inavyoonesha hii idadi inakuwa siku hadi siku, naamini punde watu watakubaliana nami kuwa Uislam ndio na utakuwa ndio dini ya ulaya.”[17] Pia alishangazwa na wale wasioona mabadiliko ya Uislam barani humo kwa kusema, “Eti watu bado hawajaujua Uislam! Inashangaza watu bado hawajangundua kuwa Uislam ndio dini ya ulaya…”[18] aliongezea.

Kutoka kwa mwanahabari wa Chicago Tribune Evan Osnos ambae alisema: “Kwa Ulaya,…swala sio kipikitakachotawala kati ya umagharibi na Uislam, lakini lipi kati ya madhehebu mengi ya Uislam ndio yatakayo tawala.”[19] Wengine wanaweza wakachukulia yafuatayo kama dalili ya zao la Uislam kushinda barani Ulaya: Bara la Yuropa (Ulaya) litakuwa na misikiti na minara yake mingi kuliko makanisa na majengo mengine ya dini hiyo; Adhana, wito kuwaita watu kufanya ibada ya swala, itavuma kutoka Paris mpaka Rotterdam, hadi Brussels na London; vijana wa Kiislamu wenye ndevu watafurika mitaani; Waislamu wawe viongozi wa nchi katika dola zote za bara hilo; Wakristo sasa wapiganie haki zao za wachache; uhuru wa kujieleza (freedom of expression) kiholelaholela uwe mashakani maana Shariah za Allah zitatawala; maduka ya nguo yanayouza nguo za kike yatakuwa hayakosi Niqaab (hijab ya kufunika uso), hijaab na nguo nyengine nzuri za Kiislamu; wanasesere waliovalishwa hijab nao kujaa masokoni kwa ajili ya watoto kuchezea; wafanyabiashara wanaopenda kuchunguza mahitajio ya wateja wao watashindana kufungua migahawa inayowapatia pizza halali; kuanzishwa kwa taasisi zinazowafikiana na Uislamu kama vyuo vikuu vya wanawake tu (na wala sio ule wa mchanganyiko baina ya wasichana na wanaume); wazungu kutoka Ulaya wengi wawe wazungumzaji Kiarabu kama lugha yao ya pili na pia lugha hiyo ya Kiarabu kufundishwa mashuleni; Madrasah (shule za kufundisha dini ya Kiislamu) za kisasa zitaenea kila kona ya mtaa…

REJEA


[1]. Wiener, Jocelyn (Times Staff Writer). “Young, Female and Muslim.” St. Petersburg Times 7 Oct. 2002.

[2]. Elliott, Andrea. “Muslim Converts Face Discrimination.” New York Times 30 April 2005.

[3]. Berrington, Lucy. “Why Are British Women Turning to Islam?” The Times 9 Nov. 1993.

[4]. Hellen, Nicholas and Christopher Morgan. “Islamic Britain lures top people.” The Sunday Times 22 Feb. 2004.

[5].Taylor, Jerome. Morrison, Sarah.  “The Islamification of Britain: record numbers embrace Muslim faith.” The Independent 4 Jan 2011. Also see: Brice, Kevin. A minority within a minority: A report on converts to Islam in the United Kingdom. Faith Matters, 2011.

[6]. Savage, Timothy M. “Europe and Islam: Crescent Waxing, Cultures Clashing.” The Washington Quarterly Summer 2004. p.28.

[7]. Buchanan, Patrick J. “Coming Clash of Civilizations? Theamericancause.org 7 Des 2001. http://www.theamericancause.org/patcomingclashprint.htm.

[8]. Allen Jr., John L. “Europe’s Muslims Worry Bishops.” National Catholic Reporter 22 Okt 1999.

[9]. “The Intergration of Muslims In Europe.” Oxford Analytica 24 Feb 2009. http://www.forbes.com/2009/01/23/france-uk-muslims-business_oxford.htmllast iliyopitiwa tena 29 Aprili 2009.

[10]. Pipes, Daniel. “Europe or Eurabia?” Australian 15 Aprili 2008.

[11]. Isabelle de Pommereau. “In Europe, skylines reflect the rise of Islam.” The Christian Science Monitor 26 Julai 2007.

[12]. Van Wishard, William. “Major Trends Reshaping The Global context.” Worldtrendresearch.com  http://www.worldtrendresearch.com/major-trends.php baada ya kupitiwa tena 12/09/2009.

[13]. Lewis, Bernard. “Europe and Islam”. American Enterprise Institute. 7Machi 2007 (katika hafla ya chakula cha jioni ya AEI, alipofanya muhadhara Irving Kristol: Washington). Pia tazama Machils, David na Tovah Lazaroff. “Muslims about to take over Europe.” The Jerusalem Post 29 Jan 2007.

* Profesa Bernard Lewis alipokea tuzo ya AEI’s Irving Kristol mwaka 2007. Alifanya utabiri wake hapo juu mwaka 2004.  Hundley,Tom. “Article of Faith for some: Europe Goinng Muslim.” Chicago Tribune 25 Juni 2006

[14]. Ford, Peter. “Why European Women Are Turning to Islam.” The Christian Science Monitor 27 Des 2005.

[15]. Edwards, Ruth Dudley. “Will Britain one day be Muslim?” The Daily Mail 5 Mei 2007. Pia tafuta kupitia Al Jazeera Television. 10 aprili 2006.

[16]. Esposito, John L. “Introduction John L. Esposito.” Katika historia ya Uislamu Oxford. Ed. John L. Esposito. Oxford Islamic Studies Online. 11 machi 2009. Pia angalia: “Observing Islam.” Online Newshour. Pbs.org. 16 Nov.2001. http://www.pbs.org/newshour/bb/religion/july-dec01/islam_11-16.html

[17]. “Islam is and will be Europian religion” Today’s zaman 12 Machi 2007.

[18]. “Islam is and will be Europian religion” Today’s zaman 12 Machi 2007.

[19]. Osnos, Evan. “Islam shaping a new Europe.” Chicago Tribune 19 Des 2004

 
Leave a comment

Posted by on November 13, 2012 in Dini Inayokuwa kwa Kasi

 

Tags: , , , ,