RSS

Tag Archives: Ukristo

Michael Wolfe

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

“Muda wowote utakaochukulia dini mzaha, basi wewe ndio utakayechekwa.”

~ Michael Wolfe

Pamoja na kuwa Rais na prodyuza mkuu wa mfuko wa Unity Productions, Michael Wolfe (aliyezaliwa 3 Aprili 1945, Marekani) ni mtunzi wa vitabu vya kishairi, hadithi za kubuni, za masafa na historia. Pia ni mhadhiri wa masuala ya kiislamu katika vyuo vikuu nchini Marekani, vikiwemo kile cha Harvard, Georgetown, Stanford, SUNY Buffalo, na cha Princeton. Ana shahada ya fani ya fasihi (sanaa)  kutoka Chuo Kikuu cha Wesleyan.

Ana asili ya dini mbili, Uyahudi kutoka kwa baba na Ukristo kutoka mama yake. Hivyo alikuwa na fursa ya kusherehekea sikukuu zote Hanukkah na Krismasi. Anaandika:

“Baba yangu ni Myahudi, mama ni ni Mkristo. kutokana na uchotara wangu, mguu mmoja upo katika Uyahudi na mwengine upo katika Ukristo. Imani zote zilikuwa hazina mashaka kwangu. Hata hivyo, ile iliyokuwa inahamasisha ‘wao wao tu’ (waliobarikiwa) [Uyahudi] niliiona haiungani mkono nami, na ile nyengine iliyojaa mafumbo [Ukristo] haikunifurahisha

Kutembea kwake kwingi na kupenda vitabu kulimfanya kuufahamu Uislamu ambao kani (nguvu  ya uvutano) yake ilishindwa kuzuiliwa na Michael. Moja ya sababu iliyomfanya akubaliane na Uislamu ni kukuta katika Uislamu mambo yanayoendana na matakwa yake. Hivyo anasema:

“Sikuweza kuorodhesha mahitajio yangu yote, lakini angalau nilikuwa najua kipi nikifatacho. Dini niitakayo mimi ni dini itakayoweza nieleza kuhusu metafizikia (falsafa ya kuchunguza chanzo cha uhai na maarifa) kwani metafizikia ndiyo sayansi. Sitaki ile inayopongeza utumizi duni wa akili, au iliyojaa mafumbo ili kuwaridhisha wachungaji. Isiyokuwa na wachungaji (viongozi), isiyokuwa na tofauti kati ya uasili na vitu vyake vilivyobarikiwa. Ambapo kutakuwa hakuna vita na nyama. Tendo la ndoa liwe ni la asili tu na sio eti kutokana na laana waliyopewa viumbe. Mwishowe, nilitaka ibada ya kila siku itakayoongoza nidhamu yangu. Zaidi ya yote, nilitaka jambo lililo wazi na uhuru wa kweli. Sikutaka niwe katika mkumbo wa kufata vitu kibubusa.* Na kila nilivyokua nausoma Uislamu, ndivyo ulivyokuwa ukiafikiana na matakwa yangu.”

Michael wolfe amekuwa Muislamu akiwa na miaka 40, baada ya kushindana na imani tofauti tofauti kwa miaka 20. Ingawa inatosha kwa mtu kufanya Hijja mara moja tu katika maisha, Bw. Wolfe katika kugombania kwake kupata radhi za Mwenyezi Mungu, amehiji si chini ya mara tatu, Hijja yake ya mwanzo ikiwa mwaka 1991. Akiuona ukweli wa Uislamu na ujinga wa baadhi ya watu katika faida ya Uislamu, Michael aliona haja ya kuandika haya:

“Rafiki zangu walioathiriwa na siasa hawakuridhishwa na chaguo langu jipya. Wote walichanganya Uislamu na viongozi madhalimu wa Mashariki ya Kati waliodhaniwa kutaka kufanya mapinduzi ili watawale. Vitabu walivyosoma, habari walizotazama vyote vilichukulia dini hii kama mpango wa kisiasa tu. Halikuwapo linalosemwa kuhusu ibada zake. Napenda kumkariri Mae West kwao pale alivyosema: “Muda wowote utakaochukulia dini mzaha, basi wewe ndio utakayechekwa.” Kihistoria, Muislamu anaiona dini kama ni hitimisho, mmea uliopevuka ambalo ulipandwa tangu wakati wa Adam. Imejengwa kwa msingi wa kuabudu Mungu mmoja kama Uyahudi, ambayo mitume wake Uislamu unawachukulia kama ni ndugu waliotoka kumoja na kilele chao kikiwa Yesu na Muhammad. kusema kweli, Uislamu umefanya kazi kubwa katika hatua ya kuirudisha ladha ya maisha kwa mamilioni ya watu. Kitabu chake, Qur’an kilimfanya Goethe kusema, “Mnaiona hii, mafundisho yake hayashindwi abadan; pamoja na mifumo yetu yote ya kibinaadam, hatuwezi kufika, na huo ndio ukweli hakuna mfumo wa kibinaadamu utakaofanikiwa”.

Akiongea na mtangazaji Bob Faw kuhusu imani yake mpya. Faw ‘alimpiga’ bwana Wolfe kwa swali hili: “Kwa kuwa ushakuwa muislamu, je kuna tofauti yoyote kwako labda!?” Wolfe akajibu: “Bila shaka ipo, umbile nilokuwa nalikosa zamani maishani mwangu lipo sasa nami. nalihisi kabisa.” Wolfe alivutiwa sana na mafundisho ya Uislamu kuwa kila mtu azungumze na Mungu mwenyewe, bila kuwa na kizuizi katikati:

“Hili jambo la kufanya mazungumzo na Mola wako mtukufu bila kuwa na balozi katikati, kusikohitaji jengo fulani au mtu maalum, kunanipendeza mno.”

Michael Wolfe anajulikana zaidi kwa filamu yake katika kipindi cha Nightline cha ABC iliyorushwa Aprili 18, 1997 ikijulikana kama An American in Mecca (Mmarekani Akiwa Makkah). Kipindi hiko kikateuliwa kuwemo katika tuzo za Peabody, Emmy, George Polk na National Press Club. Filamu ilishinda tuzo ya mwaka kutoka katika Baraza la Waislamu (Muslim Public Affairs Council). Michael Wolfe alishiriki kutengeneza, na kusimamia uhariri wa filamu ya masaa mawili iliyohusu maisha ya Mtume Muhammad iliyoitwa Muhammad: Legacy of a Prophet. Filamu hiyo ilioneshwa nchi nzima na PBS na baadae kuonyeshwa kimataifa na National Geograpghic International. Filamu ilituzwa na Cine Special Jury Award kwa filamu bora izungumziayo watu au mahali. Wakati wakutengeneza filamu hiyo, washiriki walihitaji kuperuzi kwingi katika maisha ya Mtume. Michael Wolfe mwenyewe anakiri kusoma Ibn Kathir na vitabu vyengine vya seerah (mwenendo wa Mtume). Kiukweli, kukawa na Wamarekani wengi ambao walisilimu baada ya kuona filamu hii. Katika mahojiano, Islam Online walimuuliza alichovuna  baada ya zoezi hili kubwa la kuandaa filamu hii ya Muhammad na alijibu kama ifuatavyo:

“Nimemjua Mtume vyema zaidi kuliko mwanzo kabla hatujaanza kutengeneza filamu hii japokuwa kumsoma kwangu ndio kwanza kulianza. Kuna mengi ya kujifunza. Wakati tunatengeza filamu hii, niliweza kuona na kufahamu hali ya Waislamu wa Marekani. Najua sasa wepi ni Waislamu na vipi tunafanya. Ni kifungua jicho kwangu mimi kama Mmarekani niliyezaliwa hapa, ni jambo la faraja sana kukutana na watu kutoka sehemu mbalimbali, watu wenye lugha tofauti na mengineyo. Ni moja ya hazina za kuwa Muislamu.”

Katika mahojiano tofauti, Michael Wolfe kama mmoja wa waandaaji wa filamu ya Muhammad: The Legacy of a Prophet, alisema:

Kwa Wamarekani wengi kutokuwa na uelewa wa imani yangu kunanishangaza sana. Japokuwa Uislamu ni dini inayokua kwa kasi zaidi, bado tabia nyingi za Wamarekani kuhusu Uislamu zimekuwa zikitawaliwa na chuki, kuelewa vibaya na hata wakati mwengine uhasama wa wazi. Wana uelewa mdogo tu kuhusu Mtume aliyefundisha dini hii na ipi ni misingi ya ibada zetu. Siasa na mila za watu wa mashariki ya Kati, gumzo la  ugaidi vyote vimeshiriki kukandamiza uelewa wao mzuri wa dini. Ukichukulia kwamba kundi kubwa la Waislamu haliko hata Mashariki ya Kati bali Indonesia, utambuzi huu sema kweli uanapotosha.”

Filamu nyengine alizoshiriki Wolfe katika uandaaji ni Cities of Light: The Rise and Fall of Islamic Spain (Miji ya Muangaza: Kupanda na Kuporomoka Kwa Dola ya Kiislamu Hispania) na Prince Among Slaves (Mfalme Miongoni Mwa Watumwa). Sanjari na hilo, Wolfe ameshiriki katika vipindi mbalimbali vya redio. Anaandika makala maalumu iitwayo “From A Western Minaret” kwa ajili ya jarida la mtandaoni Beliefnet.com.

Kazi zilizochapishwa za Wolfe ni pamoja na The Hadj: An American’s Pilgrimage to Mecca. (New York: Atlantic Monthly Press, 1993. Kina kurasa 352); One Thousand Roads to Mecca: Ten Centuries of Travelers Writing about the Muslim Pilgrimage, (New York: Grove Press, 1997. Kina kurasa 656) ; na Taking Back Islam: American Muslims Reclaim their Faith, (Rodale Press, Pennsylvania, 2003. Kina kurasa 256). Baadhi ya tuzo alizopokea ni pamoja na Lowell Thomas Award, “Best Cultural Tourism Article, 1998”; Marin County Arts Council Writers Award, 1990, na 1983; California State Arts Council Writers Award, 1985. Michael Wolfe alitangazwa mshindi wa Tuzo ya  2003 ya Wilbur Award kwa kitabu bora cha mwaka kuhusu dini. Anaishi mwishoni mwa mtaa salama, uliofungwa, huko Santa Cruz.

[* Kamusi ya TUKI imetafsiri neno ‘dogma’ (ububusa) kama imani inayofundishwa katika  kanisa unayotakiwa kuikubali bila kuisaili (kuhoji).]

Njia ya Mawasiliano:

Anuani:

Unity Productions Foundation (UPF)
P.O. Box 650458
Potomac Falls, VA 20165-0458
Fax (703) 738-7044

info@upf.tv

 

Tovuti:

http://www.michaelwolfeauthor.com

http://www.upf.tv/

REJEA

[Wolfe, Michael. The Hadj: An American’s Pilgrimage to Mecca. New York: Atlantic Monthly Press, 1993; “I Had Not Gone Shopping for a New Religion.” Turkish Weekly 10 May 2007; Marquis Who’s Who in America. 40th Edition; Stanley, Alessandra. “The TV Watch; A Portrait Of the Prophet Behind Islam.” The New York Times 18 Dec.2002; “Profile: Muslim Converts.” Religion & Ethics Newsweekly. Pbs.org. 8 Oct. 2004,   Episode no. 806 <http://www.pbs.org/wnet/religionandethics/week806/profile.html#&gt;; Wolfe, Michael. “Interview: Michael Wolfe, co-producer of Muhammad: Legacy of a Prophet.” Islamonline.net <http://www.islamonline.net/servlet/Satellite?c=Article_C&cid=1158658340050&pagename=Zone-English-ArtCulture%2FACELayout&gt;; Michael Schwarz, Michael Wolfe and Alex Kronemer. “Muhammad: Legacy of a Prophet: Interview with the Filmmakers.”kqed.org <http://www.kqed.org/press/tv/muhammad/interview.jsp>%5D

Advertisements
 
Leave a comment

Posted by on November 16, 2012 in Waliosilimu

 

Tags: , , , , ,

Takwimu Zitaongea Kwa Sauti Zaidi

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Tunaamini takwimu nyingi zitaongea kwa sauti yenye kusikika zaidi kuliko maneno tu ambayo tuliyokuwa tunayatumia. Kama ilivyonukuliwa kutoka katika Kamusi-elezo ya Kikristo ya Dunia (World Christian Encyclopedia: A Comparative Study of Churches and Religions in the Modern World) ikielezea tafiti ya makanisa na dini katika dunia hii ya sasa inasema:

“…Ukristo umepata upungufu mkubwa wa wafuasi katika pande la magharibi mwa dunia na katika nchi za kikomonisti kwa miaka 60 iliyopita. Katika Muungano wa Kisovieti (sasa Urusi), Wakristo wamepungua kutoka asilimia 83.6 mwaka 1900 mpaka kufikia asilimia 36.1 leo hii. Ulaya na Marekani ya Kaskazini, usaliti kutoka Ukristo kuingia katika dini nyengine au kutokuwa na dini kabisa zimefikia 1,820,500 kwa mwaka.  Hii ni hasara na upotezaji mkubwa….”[1]

Kulingana na jarida la Kikristo, The Plain Truth,[2] ambalo vyanzo vyake ni World almanac na Book of Facts 1935, Reader’s Digest Almanac na Yearbook1983, linatutanabaisha kuwa katika kipindi cha miaka hamsini (1934-1984):

Kutokana na takwimu tulizozipata katika jarida hilo, kama tukachukua dini tatu tu jedwali litakuwa kama ifuatavyo:

Makala iliyokuwa katika jarida la The Plane Truth la mwaka 1984 ilisema, “Kinyume na kupungua kwa waumini makanisani huku Magharibi, habari zinaripoti mwenendo na maendeleo ya Waislam yaliyo kinyume kabisa na sisi. Uislam unaweza kuwa ndio dini itakayokua na kuenea zaidi duniani….”[3] Na ni kweli kama ilivyotabiriwa, Uislam sasa ndio dini yenye kukua kwa kasi zaidi duniani. Hata Vatikani wanaukubali ukweli huo kuwa sasa Uislam umeupiku Ukatoliki, “Kwa mara ya kwanza katika historia, hatupo tena juu; Waislam washatupiku,” haya yalisemwa na Monsignor Vittorio Formenti katika mahojiano yake na gazeti la vatikani L’Osservatore Romano. Formenti ambaye ndiye mkusanyaji na mpangaji makala katika kitabu cha Vatikani cha kila mwaka alisema Wakatoliki wamefikia asilimia 17.4 ya watu wote duniani- asilimia isiyoongezeka- wakati Waislam washafika asilimia 19.2 sasa.[4]

Sanjari na hilo, The World Christian Database (WCD) na wale watangulizi wao World Christian Encyclopedia (WCE – Kamusi Elezo ya Kikristo Duniani) walifanyia utafiti wa idadi ya watu katika masuala ya kidini na kuachia matokeo ya chunguzi zao kwa mara kadhaa. Kutoka katika majedwali ya matokeo yao, malingano ya Ukristo na Uislam katika ukuaji yalikuwa kama ifuatavyo:

[Rejea za takwimu zilizotolewa fatilia katika: Barrett, David B., George Thomas Kurian, and Todd M. Johnson. 2001. World Christian Encyclopedia: A comparative survey of churches and religions in the modern world. New York: Oxford University Press. p 4. Pia pitia, “The List: The World’s Fastest-Growing Religions.” Foreign Policy 14 May 2007.]

Akielezea dini zisizikuwa za Kikristo, msimamo wa mtunzi wa WCE ni: “…tunaweza amini kuwa dini hizo ni za uongo na hazifai na tukajaribu kuzivuta katika imani ya Yesu Kristo….”[5] tukiamini kuwa takwimu hizi za ‘dini pingaji’ hazina upendeleo na haziko kwa ajili ya kuwashinda kuwavuta kuingia katika imani ya Yesu Kristo, wacha sisi tuzitumie katika uchambuzi wetu. The World Christian Encyclopedia inatupa idadi ya wote Waislam kwa Wakristo ya mwaka 1900 na ya mwaka 2000. Idadi ya Wakristo mwaka 1900 ilikuwa na 558 056 332 na mwaka 2000 ikawa 2 019 921 366 na idadi ya Waislam katika miaka hiyo hiyo ilikuwa 200 102 284 na 1 200 653 040.[6]

Kanuni rahisi ya kukokotoa asilimia ya ongezeko katika vipindi hivi ni hii ifuatayo:

Sasa, tukitumia takwimu tulizopewa kutoka WCE, tutapata ongezeko la Wakristo kiasilimia litakuwa:

Na baada ya kukokotoa,  ongezeko la Wakristo litakuwa 262%

Tukifanya mahesabu hayo hayo kutumia idadi ya Waislam katika vipindi hivyo.

Tutapata ongezeko la Waislam kuwa ni 500%

Bado, Uislam unaongoza kwa kuwa na asilimia 500% na Ukristo kuwa na 262%. Mwaka 1997, mwanatakwimu kutoka US Center for World Mission alisema kuwa kiujumla idadi ya wafuasi wa Kikristo inaongezeka kwa asilimia 2.3 kila mwaka.[7] Kutokana na Ontario Consultants on Religious Tolerance Uislam unakuwa kwa asilimia 2.9 kila mwaka ambaye ni kasi kubwa kuizidi kasi ya ongezeko la idadi ya watu duniani ambayo ni asilimia 2.3 tu kwa mwaka.[8] Tukichunguza na kufikiri kwa makini, hakuna ugumu utakaibukia katika kukubaliana kuwa kwa mwenendo huu wa Uislam, karibuni kitafika kipindi ambacho Uislam utakuwa ushazivuka dini zote ulimwenguni. Mnamo mwezi Oktoba 2009, gazeti la Kenya The Standard liliibuka na makala ilobeba ujumbe: “Mmoja katika kila wanne ni Muislam katika kipindi hiki ambapo wafuasi washafikia bilioni 1.57 duniani.[9] Takwimu hizi ziliwekwa hadharani na Pew Forum on Religion & Public Life katika ripoti yao ambayo inaheshimika kwa machangunuo ya kinagaubaga kuliko zote inazofanana nazo. Kama mwaka 2000, WCE walisema Waislam walikuwa bilioni 1.2 na baada ya miaka tisa tu Pew Forum waseme Waislam washafika bilioni 1.57. vipi idadi ya Waislam itakuwa baada ya miaka hamsini?! Na tusubiri tuone.

 REJEA


[1]. Barrett, David B. World Christian Encyclopedia: A comparative study of churches and religions in the modern world, AD 1900-2000. New York: Oxford University Press, 1982.p. 7.

[2]. Stump, Keith. W. “A Crucial Half Century of Religion.” The Plain Truth Feb. 1984 p.11.

[3]. Stump, Keith. W. “A Crucial Half Century of Religion.” The Plain Truth Feb. 1984 p.20.

[4]. Richard Owen. “Islam overtakes Catholicism as world’s largest religion.” Times 31 March 2008; also see Kington, Tom. “Number of Muslims ahead of Catholics, says Vatican.” The Guardian 31 March 2008; “Muslims outnumber Catholics.” PRESS TV. 30 Mar 2008 < http://www.presstv.ir/detail.aspx?id=49503&sectionid=3510212&gt; ; Rizzo, Alessandra (Associated Press Writer). “Muslims More Numerous Than Catholics.” ABC News 30 March 2008; CBS News 30 March 2008.

[5].  Barrett, David B. Preface. World Christian Encyclopedia: A comparative study of churches and religions in the modern world, AD 1900-2000. By Barrett. New York: Oxford University Press, 1982.

[6]. Barrett, David B. World Christian Encyclopedia: A comparative study of churches and religions in the modern world, AD 1900-2000. New York: Oxford University Press, 1982.p. 6.

[7]. Greg H. Parsons, Executive Director, U.S. Center for World Mission, Pasadena, CA; quoted in Zondervan News Service, 21 Feb. 1997.

[8]. Robinson, B.A.  “Growth Rate of Christianity & Islam.” religioustolerance.org. 6 Nov. 2001. <http://www.religioustolerance.org/growth_isl_chr.htm&gt;; Pia tazama, Khan, Arshad. Islam, Muslims and America: Understanding the Basis of Their Conflict. Algora Publishing, 2003.p.29.

[9]. Gorski, Eric (AP Religion Writer). “One in every four is a Muslim as followers hits 1.57 billion worldwide.” The Standard 9 Oct. 2009. Pia tizama, Greene, Richard Allen. “Nearly 1 in 4 people worldwide is Muslim, report says.”CNN 8 Oct. 2009; <http://edition.cnn.com/2009/WORLD/asiapcf/10/07/muslim.world.population/index.html&gt;; Beaumont, Peter. “One in four people is Muslim, says study.” Guardian 8 Oct. 2009; Pew Forum on Religion & Public Life. “Mapping the Global Muslim Population: A Report on the Size and Distribution of the World’s Muslim Population.” 8 Oct. 2009.

 
Leave a comment

Posted by on November 13, 2012 in Dini Inayokuwa kwa Kasi

 

Tags: , , ,

Akili Yenye Kufikiri Kwa Kasi

————————————————————————————————————————————————————-

***** Ifuatayo ni Dondoo (excerpt) ya kitabu cha Salim Boss kiitwacho “Wao Ima ni Waerevu Mno au Wajinga Mno” chenye kurasa 672 zote zimechapishwa kwa rangi (full colour). Kinunue kwa Tshs 17000 na Kshs 900. Ni tarjama ya kitabu kilichouzika sana kiitwacho “They are Either Extremely Smart or Extremely Ignorant” *****

————————————————————————————————————————————————————-

Akili yenye kufikiri huwa inashtushwa na taarifa kama “Waislamu ndio kundi linalokuwa kwa kasi zaidi duniani….”[1] ambayo ilichapishwa na gazeti lililoenea na kusomwa na wengi Marekani, USA Today. Akili yenye kufikiri itashuhudia Hillary Rodham Clinton akisema, “Uislam ndio dini inayoenea kwa kasi zaidi Marekani, ni mwongozo na nguzo ya uimara kwa wengi wa watu wetu….”[2] na kushughulishwa. Na baada ya kusikia kutoka katika Shirikisho la Habari la Uingereza (BBC) ambapo Mike Wooldridge akiripoti kuwa, “Uislam ndio imani inayokuwa kwa kasi zaidi….”[3], bila shaka kwa mtu mwerevu na mwenye kutumia akili yake ipasavyo atajenga wazo akilini mwake kuwa “Huenda dini hii ikawa ndio dini ya kweli”. Kisha akisoma The Junior Encyclopedia of Canada ilotanabaisha: “Uislam ndio imani inayokua kwa kasi zaidi ulimwenguni”[4] atatafakari, akitumia akili zake vizuri na kulazimika kuweka chuki zake kando na kuutazama ukweli, hata kudiriki kuuona Uislam kuwa ndio badiliko la msingi, muhimu na la kweli. “…Sheria ya Muhammad imekutana na mapokezi yasiyofanana nayo kabisa hapa duniani….”[5] hii iliandikwa na George Sale, mmoja kati ya wa mwanzo kuitafsiri Qur’an kwa lugha ya Kiengereza, aliyejitunuku shahada ya mpingaji mkubwa wa Muhammad na mchukiaji wa dini ya Kiislam. Kuongezea hilo, “Hakuna dini nyengine ieneayo kwa kasi zaidi kuliko Uislam”[6] iliyoandikwa na James Michener, mwandishi mashuhuri na mshindi wa zawadi ya waandishi bora wa Pulitzer. Mtu mwenye chuki na dharau ya hali ya juu anaweza kusikia sauti ndogo kichwani mwake ikinong’ona, “ Wewe! Ni bora ukubali walau mara moja tu kuwa kuna jambo kubwa katika Uislam.” Na pale jarida la The Economist wanapoitanabaisha dunia kuwa “Wengi kati ya wasomi wa Kikristo wanakubali kuwa Uislam utaupita Ukristo kama dini yenye wafuasi wengi na inayoenea kwa kasi kabla ya mwaka 2050.”[7] inabidi watu waendelee kuwa wakimya wakipea mazingatio na kutafakari usukani.

Kama hiyo haitoshi, kipande cha habari kilichotolewa kutoka katika jarida la National Geography la mwezi wa kwanza (January) 2002 lilielezea kuwa “Khumusi (moja ya tano) ya wannadam sasa wanafata Uislam, dini inayokuwa kwa kasi zaidi japokuwa ndio dini inayoeleweka vibaya kuliko zote duniani.”[8]

Tarehe 17 Julai 1997, mkurugenzi wa Christian Futures Network, John Gary baada ya kupokea zawadi yake katika World Future Society (tamasha linalojadili jamii za kesho za kidunia), alisikika akiongelea “Matukio kumi ya dunia yahusuyo dini” na katika tukio la tatu alitamka “Miongoni mwa dini za hapa ulimwenguni, Uislam unashika nafasi ya juu kwa ukuaji wa kasi….katika takwimu za kipindi cha baadae, haitashangaza kuona Uislam ukiupiku Ukristo kwa kuwa na idada ya wafuasi wengi zaidi.”[9] Hiyo ni tabiri moja, lakini kwa akili isiyo na upendeleo wowote utauona Uislam kupitia lenzi yenye kuheshimika baada ya kusoma tabiri nyengine ya msomi mashuhuri Samuel Huntington akitabiri kuwa:

“Asilimia ya Wakristo duniani…utafikia takriban asilimia 25 ya watu wote duniani kabla ya mwaka 2025….Japokuwa Waislam wataendelea kuongezeka kwa kasi ya ajabu, kufikia asilimia 20 ya watu kabla mwanzo mwa karne ya 21 kufunika idadi ya Wakristo miaka kadhaa baadae na hata uwezekano wa kufiksha asilimia 30 ya watu kabla ya mwaka 2025.”[10]

Wakati Kitabu cha Maarifa cha Guinness (Guinness Book of Knowledge) kilikiri kuwa Uislam ndio dini inayokuwa na kuenea kwa kasi zaidi duniani[11], kwa yeyote muungwana, mpenda ukweli na mwenye fikra za haraka atakubali kuwa Uislam utakuja kutawala mambo yote ya kilimwengu. Lakini  mwishoni,  Guinness World Records 2003 , kitabu chenye mamlaka na chenye mauzo mengi kinachoangazia ukweli wa kushangaza na mafanikio yasiolingana ya kibinaadam, kinasema, “Katika kipindi cha 1990 mpaka 2000, takriban watu wapatao milioni 12 na unusu walibadili dini kuuelekea Uislam kuliko Ukristo”, kwa akili yenye udadisi mkubwa itahitaji maelezo na kutokana na hilo hii ni ambalo Guinness World Records 2003 ilirikodi:

Uislam ndio dini ieneayo kwa kasi zaidi, Mnamo mwaka 1990, watu milioni 935 walikuwa Waislam na idadi hii ikaongezeka hadi kufikia bilioni moja na laki mbili mwaka 2000, ikimaanisha mmoja kati ya watano duniani tayari ni Waislam. Ingawa dini hii ilianzia(tukiongelea kipindi cha Muhammad) Uarabuni, mpaka mwaka 2002, asilimia 80 ya waumini wake wako nje ya uarabuni. Katika kipindi cha 1990-2000, takriban watu milioni 12 na nusu wameingia katika Uislam zaidi kuliko wale walioingia katika Ukristo.[12]

Hermann Eilts (aliyezaliwa mwaka 1922) aliyekuwa balozi wa Marekani Saudia Arabia  na Misri ambaye baadae akajiunga na Chuo Kikuu cha Boston kama Profesa wa Masuala ya Kimataifa (International Relations), na hapo kuwa mkuu wa kitengo cha Sayansi ya Siasa (Political Science) na baadae kuwa mkuu wa kitengo cha Masuala ya Kimataifa alikuwa na haya ya kusema:

“Waislam duniani sasa wamekaribia billion moja*,hiyo ni takwimu ya kuvutia. Lakini kwangu mie linalovutia na kushangaza zaidi ni Uislam kuwa dini ikuayo kwa kasi zaidi katika dini zinazoabudu Mungu mmoja. Hili ni jambo lazima tulitilie mkazo. Kutakuwa na  jambo la kweli kuhusu Uislam kwani watu wengi wamekuwa wakivutika.[13]

REJEA


[1]. Kenny, Timothy. “Elsewhere in the World.” USA Today Final Edition 17 Feb. 1989: p.4A.

* Baada ya kumdadisi Abu Sufyan kuhusu wafuasi wa Muhammad, Heraclius alitoa maoni hayo. [Angalia Bukhari Vol.4, Bk. 52, No. 191.]

[2]. Stammer, Larry B. (Times Religion Writer). “First Lady Breaks Ground With Muslims.” Los Angeles Times Home Edition, Metro Section, Part B, 31 May 1996: p.3.

[3]. Wooldridge, Mike. “Islam: Faith under fire.” news.bbc.co.uk 14 Sept. 2001. 11:17 GMT 12:17 UK. <http://news.bbc.co.uk/1/hi/world/americas/1544071.stm&gt;

[4]. The Junior Encyclopedia of Canada. Hurting Publishers, 1990. Vol. 2, p.396.

[5]. Sale, George. Preface. The Koran. London: C. Ackers, 1734. A2.

[6]. Michener, James A. “Islam: The Misunderstood Religion.” Reader’s Digest American Edition. May 1955: p. 73.

[7].  “The Bible v the Koran, the battle of books.” The Economist 22 Dec. 2007: p.62.

[8]. Belt, Don. “The World of Islam.” National Geographic Jan. 2002.

[9]. Gary, John.  “Ten Global Trends in Religion.” wnrf.org < http://www.wnrf.org/cms/tentrends.shtml&gt; 17 July 1997.

[10]. Huntington, Samuel P. The Clash of Civilizations and the Remaking of World Order. New York: Simon & Schuster, 1996. pp. 65-66.

[11]. Guinness Book of Knowledge. p.195. [Kwa ushahidi zaidi kuonesha Uislamu ni dini inayokua kwa kasi soma: Baum, Geraldine. “For Love of Allah.” Newsday Nassau and Suffolk Edition, Part II, 7 March 1989: p.4 ; Goldman, Ari L. “Mainstream Islam Rapidly Embraced by Black Americans.” New York Times Late City Final Edition, 21 Feb. 1989: p.1; Kopel, Ted. Nightline ABC. April. 1998; Young, Gayle. “Fast-growing Islam winning converts in Western world.” cnn.com 14 April 1997 <http://edition.cnn.com/WORLD/9704/14/egypt.islam/&gt; ; Blank, Jonah. “Islam is growing fast in America, and its members defy stereotypes.” US News 12 July 1998. <http://www.usnews.com/usnews/news/articles/980720/archive_004363.htm&gt;; Seitz, Barr. “Fastest-Growing Religion Often Misunderstood.” BICNews. ABC. 13 Dec. 1997; Robinson, B.A. “University Dispute re: Islamic Book.” religioustolerance.org <http: //www.religioustolerance.org/isl_unc.htm.> 17 Aug. 2002 ; Ali, M.M. “Muslims in America: The Nation’s Fastest Growing Religion.” Washington Report on Middle East Affairs May/June 1996. pp. 13, 107.]

[12]. Guinness World Records 2003. p. 102. Pia katika Guinness World Records 2004 p.90. Katika ukurasa wake kuelezea haki za kunakili, kuna onyo madhubuti lililosema: “Kujaribu kuvunja rikodi au kuweka rikodi katika jambo Fulani ni hatari sana. Umakini na uangalifu wa hali ya juu unahitajika katika kuliendea hilo na kama lolote likikutokea basi dhima itakuwa ni yako mwenyewe. Kwa njia yeyote ile, kampuni ya Guineess World Records haitahusika na kifo au madhara yoyote yatakayojitokeza kutokana na kujaribu kuweka rikodi duniani.” Hapo ndipo mtu atapopigwa na butwaa  na kujiuliza hivi hizi dini nyengine zinajua yatakayo yakuta kwa kujaribu kuipiku rikodi ya Uislamu ya kuwa dini inayokuwa kwa kasi zaidi duniani.

[13]* Hiyo ilikuwa Juni 24, 1985, kwa sasa Waislamu wanafikia bilioni moja na nusu, angalia, “The Bible v the Koran, the battle of books.” The Economist 22 Dec. 2007.p.62. Pia tazama katika, “Major Religions of the World Ranked by Number of Adherents.” adherents.com <http://www.adherents.com/Religions_By_Adherents.html&gt; last retrieved 2 June 2009. ; na kutokana na jarida la Time, “Moja ya sababu ya kukua kwa uchumi halal ni hii idadi ya vijana bilioni 1.6 ambao sehemu zengine ni matajiri kuliko.” Tazama Power, Carla. “Halal: Buying Muslim.” Time 25 May 2009. p.38. Sanjari na hilo, Taasisi ya Pew Forum on Religion & Public Life ilifanya utafiti mkubwa mwaka 2009 na kukuta Waislamu duniani wakifikia bilioni 1.57. Tazama,  Pew Forum on Religion & Public Life.  “Mapping the Global Muslim Population: A Report on the Size and Distribution of the World’s Muslim Population.” 8 Oct. 2009; Beaumont, Peter. “One in four people is Muslim, says study.” Guardian 8 Oct. 2009.

* Katika hotuba kwa kamati ya mambo ya nje katika bunge la Marekani Juni 24, 1985

 
2 Comments

Posted by on November 11, 2012 in Dini Inayokuwa kwa Kasi

 

Tags: , , ,